Uncle
 
Samahani, najua wewe ni kada lakini naomba leo uwe kitaifa zaidi..kwa maslahi ya taifa na umma. Naomba usinitie kapuni, uirushe hii iwafikie TBC na wadau, hata kama hutaiweka hapa mifikishie kwa email yao, kwenye website sijaipata.
 
Kuna kitu TBC 'Taifa' wanakifanya ambacho ni cha hatari. Shirika hili ni la utangazaji la taifa. Lakini cha ajabu, huwa lina-ripoti sana habari za chama kimoja cha siasa kuliko vingine kana kwamba vingine vimelala. Sio kweli kwamba ni chama kimoja tu cha siasa ambacho kiko active hivi sasa. 

Sio kweli kwamba hawana waandishi wa habari nchi nzima ambako vyama mbalimbali vinazunguka kujijenga na kufanya shughuli za maendeleo kitaifa. Kwanini TBC wana-report chama kimoja tu? Sasa hivi ni mfululizo kila nikiangalia taarifa za channel hii naona lazima kuwe na taarifa za chama hiki, jana katibu mwenezi alikuwa kanisani, pia katibu wa umoja wa vijana alikuwa Kigoma, juzi juzi waziri mmoja alikuwa na shughuli ya kichama huko Lindi, pia Meya fulani mstaafu wa manispaa mojawapo ya Dar nae alikuwa anaendesha shughuli ya chama huko mikoa ya kusini, mkutano wa halmashauri kuu Dodoma ndo ulikuwa kama sherehe za miaka 50 ya uhuru, yani kama jambo la kitaifa, sio la kichama, mwenyekiti wa kampeni za uraisi wa chama hicho uchaguzi uliopita nae hivi karibuni ziara yake ya kichama jijini Dar ilitangazwa sana. 

Sikatai kwamba kweli inawezekana ki-habari, habari hizi zina mvuto na wasikilizaji na watazamaji wengi, lakini JE, vyama vingine navyo haviko 'busy' namna hiyo? Je ni kweli kwamba habari zao hazina maslahi? Je ni kweli kwamba habari za 'ngangari' na 'nguvu ya umma' hazipo? Mbona kwenye magazeti tunaona mikutano na ziara vikiendelea huko Tanga na Pwani, je mtu asiyepata magazeti haya au asiyejua kusoma hatafaidika habari hizi zikitangazwa na chombo cha kitaifa? Je wanachama wa vyama hivi hawalipi kodi kama watanzania wengine kuendesha shughuli na taasisi za kiserikali ikiwemo TBC? Je, TBC hawaoni kuwa hawawatendei haki wananchi hawa wasipopata habari za maendeleo na shughuli za vyama vyao na kauli za viongozi wao kuhusu mambo mbali mbali kupitia chombo 'huru' cha kitaifa? TBC acheni u-chama. Nyie ni taasisi ya kiserikali inayoendeshwa kwa kodi ya wananchi ambao wana itikadi tofauti-tofauti. Acheni ukada. Kama mko kama yule mwenzenu aliyeenda jimboni Kondoa, ni bora mkajiweka wazi, wengine mwende kule kwenye redio ya chama, acheni uchama msiamshe hisia na hasira za wananchi wenye itikadi tofauti na hiyo ya chama chenu mnachokipigia debe kila siku, hatukitakiiiii!!!
 
Mwananchi Makini.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Hao wakurungezi wa TBC wana mawazo mgando,wanadhani CCM haiwezi kutoka madarakani.Ni jana tu niliuliza swali dogo kuhusu BBC kurusha mazishi ya Whitney Houston.Kukawa kumezuka mjadala kuhusu haya mashirika ya utangazaji ya kama BBC na TBC,mjadala ulikuwa umeanza kuchukua kasi..Nadhani hapa ndipo mahala pake haswaa.
    David V

    ReplyDelete
  2. Ni heri yako umeamua kusema. sisi wengine tulishaacha kuangalia TBC siku nyingi. Enzi za Tido Muhando aliweza ku-balance habari za vyama vyote. Huu uongozi wa sasa wameirudisha TBC enzi za chama kimoja. Wakati wananchi tayali feeling zao zipo kwenye vyama vingi, TBC bado ipo enzi ya chama kushika hatamu matokeo yake imeanchwa nyuma na wananchi.

    ReplyDelete
  3. tido aliruhusu mdahalo tu ,ccm wakasusa ye akaendelea,wakamwesabia siku, sasa ni mkuurugenzi gani arudie kosa la mwenzie kila mtu anataka ugali bwana vyama badae,nusu ya viongozi wa upinzani walikua ccm ugali ulipobanwa walihamia upinzani sasa wanabwinya,hata wapinzani ulaji ulipobanwa walirudi ccm

    ReplyDelete
  4. 100% confidence levelFebruary 20, 2012

    kwanza mtoa mada una bahati kwani kibaraka wa ccm ameiweka hii habari kwenye blog yake.
    pili nadhani tuwe wawazi tu,mkurugenzi wa tbc amepachikwa ili atetee uovu na uozo wa ccm baada ya jembe Tido kufanyiwa zengwe.kwa hali hiyo tuachane na tbc tuungane kuimarisha private media outlets zitakazo waabarisha wananchi kinacho jili ndani na nje na chenye maslahi kwao.

    ReplyDelete
  5. Wewe namba tatu mbona umejichanganya sasa..kama vyama baadae basi wasirushe habari za chama chochote,ndicho anachosema mtoa mada au ulimaanisha vyama vya upinzani??

    ReplyDelete
  6. Nafikiri kosa kubwa ambalo TBC inalolifanya ni hili la kuwa biased kwenye habari za vyama vya siasa. Tido alikuwa ana-inaitransform TBC kuelekea kuwa shirika linaloaminiwa na watanzania bila kujali itikadi zao.

    Unapo win trust ya wananchi wote unakuwa unajenga chombo endelezi na kuongeza watazamaji. TBC ichukue mfano wa BBC, jamaa huwa wanakusanya maoni ya wananchi katika vipindi mbalimbali na vipindi vinavyoonekana vinakera wananchi vinafutwa. Hii inawapatiwa wananchi ownership.

    TBC inatakiwa kuendeshwa kisayansi siyo kisiasa. Siasa inaliangamiaza Taifa, tutabaki tunalalamika tu. TBC wasidhani kuwa kwa kuwa na coverage kubwa inawafanya wasikilizwe na watu wengi la, utapata watu fulani lakini ujue kuwa hutapata watu makini wa kukusikiliza. Matangazo ya biashara ni muhimu sana na ili uendeshe kibiahsra unatakuwa kuwa na targted audience, unatakiwa kuwa na wasikilizaji wa kada zote siyo kati ya chini tu. Watu makini wengi hatuipi umuhimu TBC siku hizi kwa sababu kama hizi za UKADA. Sawa mnaendeshwa kwa kodi lakini TBC ijue kuwa kodi haitopatikana kama uchumi haujawa imara, leo hii tunaona wafanyakazi serikali wanacheleweshewa mishahara yao kwa ajili ya ukata unaoikumba nchi. TBC iangalie hilo suala, maana watu makini wanauliza kama kweli wahariri na watunga sera za utangazaji ndani ya TBC wana-qualification za kuendesha shirika au ni political cronyism, ambayo kihistoria huko nyuma iliua mashirika mengi ya umma.

    TBC wawe na kitengo cha utafiti ili kujua ni nini hasa wananchi wanahitaji kutoka katika chombo cha umma?. Nachelea kusema kuwa Chema chajiuza na kibaya chajitangaza, kujitangaza sana hakukufanyi wewe uonekane mwema zaidi. Tuwe makini na matumizi ya ofisi za umma, ukada una sehemu zake.

    Ninapenda kutoa pendekezo kuwa suala la TBC nalo liwekwe wazi katika katiba mpya ili kupunguza wanasiasa kutishia professional kufanya kazi zao. Mpaka leo sijaona kosa la Tido japo kwa wanasiasa wanaogawa madaraka watamuona msaliti kwa kusimamia taaluma.

    Michuzi nimetumia dk 15 kuansika hii I hope na wewe utaacha ukada kama mdau alivyosema na kutoa hii constructive comment.

    ReplyDelete
  7. Duh? naona bangi ya Malawi au ya Gambia imeshaingizwa Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Kabla ya Tido, hakuna aliekuwa anaangalia TBC, amekuja akaiweka vyema aka balance na vyama vngine wakamtema..heh heh..heh..! Sasa hivi TBC haiitaji ze comedy, yenyewe tu ze comedy...! Mara matangazo yamekatika...mara habari ikosewe bas ile mradi tuuu, na kwakua wameigamia chama kimoja basi mambo yanaenda na picha ya kichina isio na mbele wal mkia.

    KIBAYA zaidi, TBC imewekwa mfukoni na LOWASA. Kila mahali na kanisa atakapo enda au kutoa hotuba, TBC wanamtoa hewani. Kwani nchi hii ina mawaziri wakuu wastahafu wangapi? Mbona wao hawarushwi na TBC? Mara Lowasa kanisa hili, mara lile, kulikoni? Wrioba, Malecela na Salima Ahmed Salim Mbona hatuwasikii? TBC, acheni unafiki kwani mnaelewa fika kuwa Lowasa hakustaafu.....!

    Maafisa wanao mlinda Lowasa ni wengi kuliko anavyolindwa waziri mkuu yeyote mstaafu, nini kipo nyuma ya pazia na amacho TBC mnaendana nacho?

    No body lives forever, amani kwa wa Tanzania.

    KIbanga Msese

    ReplyDelete
  9. TBC ni TV ya walipa kodi inayoshindana na tv channels nyingine kupora matangazo ili wapromoti CCM. Hii ni kazi ya mkurugenzi wao mpya. Siku hizi hata michezo haioneshwi live tena hawana muda. Ze comedy yenyewe ni marudio tu wameacha kuonesha vipindi latest ila kokote chama kinapoenda wao wamo

    ReplyDelete
  10. POLE MDAU UMETWANGA MAJI KWENYE KINU. AU UMEMPIGIA MBUZI GITAA. HIZO BLOG ZENYEWE ZIMEJAA U CCM MTUPU. TATIZO SI CHAMA...WAANDISHI NJAA KALI AU MSHAHARA HAULINGANI NA KAZI ZAO ND'O MAANA WANAFATA UPEPO. SAWA NA POLISI DKS NURSE. HIVYO NDG YANGU VUMILIA TUU. UNLESS APATIKANE KIONGOZI WA KWELI WA UPINZANI ATKAELETA MABADILIKO YAKWELI. NCHI HIYO NI SAWA MTU KWENYE CHRONI CANCER. JIBU UNALO.

    ReplyDelete
  11. NYOTE MWAMPIGIA GITA MBUZI, HASIKII NA HATA AKISIKIA HAWEZI NA HAJUA JINSI YA KULICHEZA

    ReplyDelete
  12. MUUNDO wa TBC:/VYOMBO vya TAIFA:

    -Kwa kuwa vyombo vya Utangazaji vya Taifa inatakiwa viwe mali ya Wananchi wote na sio Mali ya Taifa au Serikali kwa vile tatizo kubwa Duniani Serikali nyingi zipo chini ya mikono ya watu wachache wanaohesabika tena wenye Itikadi moja kama Chama fulani badala ya Wananchi wote ambao wana itikadi tofauti.


    MENENDO wa TBC:
    -Siku moja asubuhi katika Kijiwe cha Kahawa hapa Dar tuliwahi kaa kwa Maongezi na Maswali na mwana Kijiwe mwenzetu ambaye ni Afisa wa Idara Masoko wa TBC ,Mtaa wa Zanaki, Zaidi ya Kituo kuelemea zaidi ktk Chama kimoja tuliuliza mabadiliko yaliyo jiri kwa vile TBC mwanzoni ilikuwa inatangaza mambo ya Kipaumbele zaidi kama hapa chini:

    TBC ya MWANZONI:
    1.-(DOCUMENTARIES) MAKALA ZA MAENDELEO YA UZALISHAJI MALI KTK SEKITA ZETU ZA UCHUMI NCHINI, KILIMO, UVUVI,MADINI,MISITU NA MALI ASILI, UTALII NA VIWANDA.
    2.-HAKI ZA BINAADAMU NA KIRAIA
    3.-MIDAHALO YA ITIKADI MBALIMBALI ZA KISIASA BILA KUJALI UPENDELEO
    4.-MAHUSIANO YA KIMATAIFA NA MAHOJIANO NA WAKILISHI WA BALOZI MBALIMBALI NCHINI.
    5.-MAKALA ZA USHIRIKISHWAJI WA MAENEO YA KIKANDA ,SADEC AFRIKA YA MASHARIKI N.K

    Isipokuwa sasa TBC imejikita zaidi ktk mambo haya:

    TBC ya SASA:
    1.-HARUSI
    2.-BETHI DEI NA VIPAIMARA
    3.-MAADHIMISHO YA SIASA (CHAMA KIMOJA)
    4.-SEND OFF PARTY
    5.-PROMOSHENI ZA KIBINAFSI
    6.-MAHAFALI YA ELIMU

    JE, WANDUGU KWA MABADILIKO HAYA YA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA NCHI CHINI YA WANANCHI KUTOKEA TBC YA MWANZO NA TBC YA SASA TUTAFIKIA LENGO?

    ReplyDelete
  13. Hellooooo!!!???,
    Raisi ni m'CCM pamoja na asilimia kubwa sana ya baraza lake la mawawaziri. TBC ni ya umma, lakini inaendeshwa na serikali.

    Nilienda shule TZ miaka ya '80. Hakukuwa na TV, ukiondoa ile ndogo ya Zenji. Kulikuwa na magazeti mawili tu. Daily News na Uhuru, haya yakimilikiwa na serikali, na CCM.
    Kulikuwa na Radio moja, RTD, yenye idhaa mbili, hii pia ya serikali.

    Sasa kuna uhuru wa habari. Kuna TV's, radio, blogs, magazeti kila kona , yasiyo ya serikali wala CCM.

    Wapinzani sasa wana nyanja kibao za kutuletea habari bila kutegemea TBC. Tusidanganyane, wapinzani wakipata uongozi wa nchi, wataitumia TBC kama vile CCM inavyofanya.

    ReplyDelete
  14. Mimi sipo na yeyote 'TOA KWANZA BORITI KWENYE JICHO LAKO NDIPO UONE KIBANZI KWENYE JICHO MLA MWENZAKO'

    Sijaona comment ambayo haiko biased hapa wote tunaugua ugonjwa huo huo tunaoukosoa.

    Wewe ni nani aliyekwambia itikadi yako ndiyo sahihi unapomsimanga mwenzako. Tupeane uhuru wa mawazo.

    Mdau hapa kaleta hoja ya kuikosoa TBC kama chombo cha Taifa kwamba kiache siasa kihudumie Taifa sasa jamaa zangu naona mmeshapanda jazba mnaleta tena yale yale badala ya kujadili mada.

    Hebu tuwe na uvumilivu wa kutofautiana itikadi ili tutoke hapa tuliponasa.

    tuwe waangalifu kwamba tunataka kujinasua kutoka kwenye tope lakini tumesimama kwenye tope hilo tunalotaka kilikimbia tutakesha tusipokuwa waangalifu Ohooo!!!

    ReplyDelete
  15. i like this mada; nafurai kwamba watanzania sasa tumekuwa watafiti hii inaonyesha nchi hii ina watu makini ambao tukiwatumia vizuri tutapata mafanikio.hongera sana mtoa mada uko makini kufuatilia mambo,tbc ujumbe mmeupata acheni ubinafsi toeni haki sawa kwa watz.Mkumbuke chombo hichi si mali ya chama ni jasho la watanzania wote so kila mtu ana haki ya kukitumia

    ReplyDelete
  16. TBC sasa imerudi enzi za Radio Tanzania Dar es Salaam baada ya kuondolewa Tido Mhando. This is very sad. Tido aliibadilisha kabisa TBC na kukifanya ni chombo kinachowatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasi. Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa kwa sababu TBC inaendeshwa na fedha za walipa kodi wote na si ruzuku ya CCM. Ninadiriki kusema kwamba enzi za Tido TBC ilikuwa ni namba moja miongoni mwa vituo kwa televisheni na redio nchini katika kutoa habari zisizoegemea upande wowote. Hakuna kituo chochote binafsi cha redio au televisheni kilichokuwa kinaikaribia TBC katika 'professionalism', lakini sasa TBC imerudi kuwa ni kipaza sauti cha CCM na serikali yake. TBC ijifunze kutoka KBC ya Kenya ambayo ilipata fedheha kubwa baada ya Kanu kushindwa na kung'olewa madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2002. TBC ibadilike tunapoelekea uchaguzi wa 2015 kwa kuwa hakuna anayejua kitakachotokea.

    ReplyDelete
  17. TBC Taifa mimi nasikiliza vipindi vya Masoud Masoud tu. Vingine vyote ni utumbo mtupu.

    ReplyDelete
  18. kama nyingi wenye kutaka utajiri wa harakaharaka hamuangalii TBC basi wengi tunaangalia iwa taarifa yenu. Na tunaipenda. Kwa nini ITV inaonyesha biased hivi hivi. Tuacheni na TBC yetu. Nakwambieni 2015 hamuoni ndani. Kama m;po vijana wa CHADEMA na vijana wa CCM tupo.

    ReplyDelete
  19. Ndugu Michuzi, hongera sana kwakuweka habari hii pamoja na comments zake. Nimeona baadhi ya comments zinakuponda moja kwa moja ila umekuwa jasiri wakuweka na kuruhusu watu watoe maoni yao. Huu ni uzalendo na kuheshimu freedom of information hata kama kipindi fulani si favourable kwako. Congratulation!

    ReplyDelete
  20. TBC ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  21. Na Tanzania Daima je? Chadema chadema chandema. But you dont mention it at all? Wakiingia madarakani nao wataonyeshwa hewani..

    ReplyDelete
  22. Anany..wa Tue Feb 21, 01:27:00 PM 2012 unaonyesha wewe ni msoma udaku tu...hujui kwamba Tanzania Daima ni mali ya Freeman Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA? Kile ni kipaza sauti chao, sawa na Uhuru na Radio Uhuru ya CCM. Hapa tunazungumzia shirika la utangazaji la Taifa, sio chama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...