Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akimuapisha Mhe. Musa Francis Esanju kuwa Hakimu Mkazi, katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, anayeshuhudia (katikati) ni Mhe. Francis Mutungi, Msajili Mahakama ya Rufani Tanzania.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (katikati) , Jaji Kiongozi,Mhe. Fakih Jundu (Kushoto) na Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Francis Mutungi (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mahakimu waliokabidhiwa hati ya uteuzi na kuapishwa.Mhe amewaasa kuwa na maadili na kazi yao na kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati.




naomba kusaidiwa na wanaojua itifaki katika mhimili wa mahakama. hivi msajili wa mahakama naye huitwa mHeshimiwa?
ReplyDeleteMsajili wa mahakama huitwa Mheshimiwa mdau, ndio itifaki ilivyo. Na mara nyingi msajili huwa ameshapita hatua ya kuwa hakimu,msajili ni juu ya hakimu. Ngazi inayofuatia kwake ni kuwa Jaji...
ReplyDeleteNafikiri mutu yeyote anayestahili heshima anaweza kuitwa Mheshimiwa fulani...Hata ww bila shaka ni Mheshimiwa -:)
ReplyDeleteHivi mheshimiwa ni nayetumika, au ni anayetumikiwa? Kwa maoni yangu, anayetumikiwa ndiye mheshimiwa!Wewe mtumishi tu huwezi kuwa mheshimiwa! Angalia hata katika familia zetu! Housegirld hawezi kuwa mheshimiwa, maana ni mtumishi. Anayemlipa mshahara (mwajiri) ndiye mheshimiwa! Kwa maelezo haya, mheshimiwa/waheshimiwa ni mwananchi/wananchi.
ReplyDelete