Meneja Biashara wa Kampuni ya TATA, Srinivas Nemalapuri akionesha baadhi ya mabasi ya UDA yaliyonunuliwa na Kampuni ya Simon G.

Na Oscar Mbuza

HATIMAYE Kampuni ya Simon Group imeanza mikakati ya kulifufua Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) baada ya kununua mabasi 30 yenye uwezo wa kubeba abiria 40 kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji jijini Dar es Salaam .

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa UDA kununua magari mengi kwa wakati mmoja tangu kuanzishwa kwa shirika hilo zaidi ya miaka 38 iliyopita.

Mwenyekiti Mtendaji wa Simon Group, Robert Kisena aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwamba kampuni yake imejizatiti katika kuifufua UDA kama ilivyoahidi wakati iliponunua hisa za kuliendesha shirika hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Taarifa hizi ni nzuri kwetu wakazi wa Dar. Lakini kiasi hicho cha mabasi ni kidogo mno. Tunahitaji magari makubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 60 na kuendele angalau itasaidia sana kwetu wakazi wa DSM.Tunaomba waongeze mengine na magari mabovu yote yakae pembeni. kwani kuna daladala nyingi ukiingia ndani seat zake hutamani hata kukaa; zimechakaa, ngumu,zimebana sana.hongereni tena na tena simon Group

    ReplyDelete
  2. UDA enzi hizo za Dar es salaam ya wastaarabu tulikuwa tunapanga foleni kupanda basi halafu unalipa nauli kwa kondakta mlango wa nyuma, kondacta amekaa kwenye kiti bila wasiwasi sio leo hii wakuja na mafisadi mmemaliza kila kitu

    ReplyDelete
  3. SIMON GROUP TENA!!!!????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...