Watoto wa Mitaani wanaosimama Mabarabarani kwa shughuli ya kuomba omba wakiwa wamelizonga gari lililokuwa limesimama kusubiri ruhusa ya Taa za kuongozea magari Barabara ya Morogoro road kutaka kupewa hela na mwenye gari hilo mchana wa leo.hali ya Watoto hawa kuongezeka mitaani ilazidi siku hadi siku na huku wengine wakifanya fujo iwapo hawapewi hela wanazozihitaji na wengine mpaka kufikia kupasua vioo vya magari hayo.sasa sijui kifanyike kitu gani ili kuweza kuwasaidia watoto hawa ambao wengine umri wao ni mdogo sana na wenye kutakiwa kuwa shule kwa wakati huu.
Wengine hawa wakiomba kwa abiria waliopo kwenye Daladala hili.
Kwanza,
ReplyDeleteStop calling them Watoto wa Mitaani because the last time i checked Mtaa doesn't conceive.
Tunachotakiwa ni simple, empower middle class across the board, that will increase the surplus and i bet majority of poor Tanzanian will move from bottom to somewhere in the middle.
Then this fiasco will be history, and it will be the Tanzania of everybody.
Mdau wa Texas
Bora umewaweka hadharani..Nilishawahi kuwasemehea humu kwenye Blog ya jamii lakini wapi.Hawa watoto wanasikitisha sana,wengi wako pale mitaa ya 'FAYA'.Ukiwauliza wazazi wao wako wapi bahadhi wanakasirika wanaondoka.Kuna na vibinti vya miaka 7-12 hivi.Wanatoka wapi??(Human trafficking?-Sidhani)
ReplyDeleteDavid V
Bad governing system. Learn from the West. Have all people get Personal Identification Numbers. Tanzania is capable of having this database. Make sure every one has a physical address and not P.O Box. Children at the age of 5 should be at kindergarten... New constitution must make this mandatory. Headteachers and educational consultants in the village or town make sure that all registered students attend school. Parents who are not responsible must face rule of law according to the constitution. These are future engineers, scientists, doctors to server the country one day.
ReplyDeleteWarudisheni Dodoma kama mwaka ule. au waombeeni kwa Mungu wapate utajiri ahem.
ReplyDeletekutatuwa hili tatizo ni kuwacha zina tu
ReplyDeleteKutowapatia fedha ndiyo msaada mkubwa zaidi kwani biashara inapoonekana inalipa wanazidi kuongezeka huku wengi wakiacha shule kwenda kuomba omba.
ReplyDeleteAsilimia ndogo zaidi ndiyo haswa wahitaji lakini hata kuwasaidia wakiwa barabarani siyo sahihi.
NGO kila kona wakilamba misaada kutoka kwa wafadhili bila kuwafikishia walengwa. Serikali inapaswa kuchukua hatua yenyewe, kuwapa makazi na elimu hawa vijana, maana wajasilia mali wa NGOs wanawatumia tu hawa maskini na kuwaacha mitaani!
ReplyDeleteWapelekwe kwenye nyumba za kulea watoto yatima ili wapate kuhudhuria shule na kupata elimu itakayowasaidia ukubwani.
ReplyDeleteJamii iwajibike. Jamii ya walikotoka na jamii wanamoishi. Hakuna mtoto aliyezaliwa mtaani, hivyo wanapaswa kurudi walipotoaka.
ReplyDeleteKuna watu wanaowatumia watoto kama chanzo cha kipato, hawa wachukuliwe hatua kali.
TUSILAUMU SERIKALI (WATZ TUMEZOEA KULAUMU KILA KITU..), SERIKALI HAIZAI WALA KUWAPA VIJISENTI AMBAVYO NI MOTISHA
Tatizo kubwa bongo na Africa ni lack of Parental Responsibility.
ReplyDeleteMtu anatakiwa kujua nini maana ya kuamua kuzaa au kuleta kiumbe duniani.
Tuna kasumba mbaya sana kufikiri kwamba kuzaa ni lazima au kuolewa na kuoa, watu wanafanya tu kama fasheni.
Mtu kama anaona hawezi kuwa responsible kwa malezi au ndoa. Matokeo yake ni kuzaa na kusema eti kila mtoto atakuja na riziki yake, huu ni upumbavu, matokeo watoto wanateseka kiasi hiki na wengine kujuta kwanini walizaliwa.
Tukumbuke duniani sio lazima kila mtu azae au aolewe au kuolewa, it is not for evrybody, sio kikombe cha chai jamani.
Serikali ingeweka kitengo maalum cha watoto wa mitaani kiwasaidie.
ReplyDeleteHaya wapendwa wote mpoo ?? omba omba hii ya watoto siyo tu ni aibu kwa nchi yetu bali na pia ni hasara kubwa kwa Taifa linalolilia maendeleo na kujitegemea. hawa watoto ambao ndilo Taifa letu la kesho-wanakua bila elimu ya msingi ya wazazi na pia bila elimu ya shule. Je ? watakuwa na faida gani kwenye Taifa la Mtanzania ? hawa watoto nao watakuja kuoa au kuolewa na kuzaa. Mimi naona , wakamatwe wapelekwe kwenye vituo vya watoto yatima ,huko watakula na watasoma na viwalo vya mitumba vipo watavaa na huko huko kwenye kambi za watoto yatima ,watatokamo madaktari na hata mawaziri. Mbona Ulaya hakuna watoto wanao omba omba barabarani ?? tatizo letu ni kwamba , wabunge wanalilia wajazwe mi-njolo njolo wakati kuna watoto wanahangaika barabarani kama hivi. asanteni- Chimile-Ndonho.
ReplyDeleteTatitizo kubwa la Watanzania wengi yani sisi tumekaa kulalama lalama kwa serikali hivi kama kweli wewe unataka kuondoka na hili tatizo jitolee kuchukua mtoto mmoja kamlee kama mwanao na pili hakuna serikali inayozaa watoto ,kwani ushawahi kufikiri ni mimba ngapi ulizozikataa hoo mimi siyo niliyekutia ujauzito je? unadhani mimba hizo zinaleta nini? au kulalama tu kwa kukimbia majukumu hatujambo.Tatu hata Nchi zilizoendelea kuna watoto kama hao.
ReplyDeleteJamani tuache lawama na tuangalie njia ya kutatua matatizo na siyo malawama kila siku kwa serikali.
MZIZI WA TATTIZO LETU:
ReplyDeleteMatekelezo ya mipango yetu ndio mzizi wa matatizo yote yanayotuzunguka ktk maisha yetu.
Mambo mengi yanaathiriwa na Siasa zaidi,Majungu zaidi, Ubinafsi zaidi, kuliko sayansi.
Inaweza kutokea jitihada za kuwakwamua watoto hawa zikafanywa na Wadau lakini cha kushangaza wakatokea wakwamishaji au watakaotaka wanufaike na mpango huo!
Ni jukumu la serikali kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili. Serikali ni asasi inayokusanya kodi kutoka kwa walipa kodi ili itoe huduma za kijamii (ambazo haziwezi kushughulikiwa na mtu mmoja mmoja). Nia ikiwepo, njia ipo! Lakini kwa mambo tunayosikia kutoka kwa wafanya maamuzi - kwa mfano, kwamba 'pale bungeni kuna umasikini wa kutupwa'- hatuwezi kutarajia nia ya serikali kutatua tatizo hili. Mbunge naye anadai ni maskini wa kutupwa, mtoto yatima naye anadai ni maskini wa kutupwa. twafwa!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKitu kinachonisikitiza sana ni pale mzazi anapomtumia mtoto kwenda kutafuta hela. Niliwahi kuhoji watoto hawa kadhaa na wengi wana wazazi. Mwishoe wanaishia kula madawa ya kulevya na kujiuza (kuanzia watoto miaka 5).
ReplyDeleteKulikuwa na kipindi kimpoja cha Hoyce Temu, kilicover hii. Na mtoto mdogo (wakiume) alisema kwamba alijikuta asubuhi amebakwa na watoto walio wakubwa (wakiume) na kamuachia Tshs.1000 kwahiyo akaona kama inampatia hela basi aendelee. That broke my heart!
Wengi hawa wametoroka vijijini, wengine hawana wazazi but majority wanawazazi wasiokuwa na uwezo na hao wazazi ndio wanaowatumia. Pia nimeona vituo vinavyowatelekeza watoto hawa kwahiyo kuwafanya watafute wenyewe kwa njia mbali mbali zisizo kuwa nzuri kwao.
Juu ya hapo, watoto hawa wamekuwa wakiambukizana magonjwa mbali mbali ikiongozwa na Ukimwi.
I say, government and society as a whole has to look at this from a bigger picture sio mtu unaongee ovyo ovyo tu bila kujua the circumstance inayowatoke watoto hao.
P.S. Ulaya wapo watoto wa Serbia/Macedonia wengi tu na wanaosha vioo vya gari kama hawa wetu na wakike wanazaa iliwaombe tu (huruma eti)! Sad Sad Sad
acheni hizo si tatizo la serikali wala nini hii ni deal bwana kuna watu wanatengeneza pesa kwa watoto hawa wanatumwa bwana na watoto hawa wana wazazi wao either mmoja au wote wawili ambao hawana uwezo na kuna wafanya biasha wana wajiri ikifija jioni wanawapelekea mapato yao acheni hizo fungueni bongo zenu wabongo eeeh wadanganyika.
ReplyDeletena la pili ni responsibility ya wazee kuzaa na kutojua kutunza kazi kuzaa tu au kumtia mtu mzigo wa mbele halafu ana mkataa unadhani mzazi mmoja ataweza kweli kulea hata majuu wanashindwa.
acheni kulalala kila kitu serikali
tunza familia yako bwana uwe responsible bwana siyo ukae bwete na ulaumu serikali
Tatizo ni wazazi kutokuwajibika. Kama watoto wamekushinda kulea kwanini uwatumie kuombaomba. Hii ni hatari sana. Wanaishi mazingira ya hatari kwa afya na usalama. Kumbukeni watoto wa mitaani hawatabaki kuwa watoto milele.Kama hawana wazazi ijulikane wepelekwe vituo vya kulea watoto yatima wapatiwe chakula, elimu na sehemu ya kuishi na watoto wenzao. Kama wazazi wako hai itabidi wazazi wachukuliwe hatua kali, maana wanawanyima haki watoto haki zao za msingi na kuepuka wajibu wao ambao ni kuwapatia mahitaji ya watoto wao, na si watoto kuwapatia mahitaji!! Responsibility and accountability is key. Haki ya nani itabidi watu wawe na leseni kuruhusiwa kuzaa. Kuzaa rahisi lakini kulea taabu. Hivi tutafika kweli? Vigogo hamuoni watoto mitaani , au mnatumia helicopter kufika maofisini? Wanaosema si tatizo la serikali, ni kweli, ila wajibu ni wao kutilia mkazo juhudi za kuhakikisha kila mtoto anapata elimu haraka iwezekanavyo. Hawa watoto ni taifa la kesho.
ReplyDeleteUjengeaji wa miji haswa inapokuwa jiji kubwa kama Dar es salaam ndiyo chanzo cha matatizo yote(India ni mfano).
ReplyDeletePia vituo vya watoto wa mtaani viwe mbali na miji ilikuwezesha watoto wawe karibu na mazingira hasili (Nature).
Cha msingi ni kuongeza uwezekano wa maisha ya vijijini haswa unaozingatia maadili ya Taifa.
Familia kujuwa haki ya mtoto kama mtoto, na mtoto kujuwa haki yake kama mtoto.
Kunafamilia zinasababisha watoto kutoroka nyumbani kutokakana na migogoro ama kumshirikisha mtoto kwenye utafutaji wa fedha ili familia ijikimu.
Tuna mazingira mazuri na tukiyatumia basi watoto wanaweza kuridhika na kutokomeza hofu waliyo nayo ambayo mfano wake ndiyo huo wa kutafuta ela ya muda na kujitenga na familia.
Hili ni Suala 'nyeti' na linauma sana kwa Watoto wa Umri kama huu 'Chekechea' waliostahili kuwepo Darasani wakisoma kwa raha na kusubiri uji wakati wa Mapumziko ya Masomo yao matokeo yake inawakuta wapo Mtaani pembeni ya barabara wakiomba!
ReplyDeleteWapigaji ma Bosi wa NGO's wakivuta mapesa ($$$) ndefu kwa Wadhamini Majuu wananunulia magari ya hela ndefu ma VOGUE RANGE ROVER na HUMMERS, wanajengea Ma BAA na ma PUB badala ya kujenga hata Majumba ya kuwatunzia watoto hawa.
ReplyDelete