Janet akiwa na mdau wake wakifurahi mara baada ya kumaliza kurekodi kipindi.
Mtayarishaji wa kipindi cha Ongea na Janet TV talk show pichani kulia akiwa na mmoja wa mwanasumbwi hapa nchini Japhet Kaseba akifanya nae mahojiano kwenye moja ya kipindi chake.
Mtayarishaji wa kipindi cha Ongea na Janet TV talk show pichani kulia akiwa na mmoja wa wadau akifanya nae mahojiano kwenye moja ya kipindi chake.
Ongea na Janet ni Talk show ambayo inazungumzia mambo yanayotugusa katika maisha yetu ya kila siku,Inahusisha Jinsia zote na rika zote. Kipindi changu nilikitengeneza mwaka 2009 june 26 lakini bahati mbaya ilikuwa ni ngumu sana kupata airtime hasa ikizingatiwa ni kipindi toka nje ya kampuni husika,bado wahusika hawajakubali kubadilika ila hii "ishu" digital itasaidia sana. -Sijaajiriwa na Clouds Tv bali tumeingia Mkataba kama partiners .
Ni kipindi ambacho sitegemei kishuke bali kitakuwa kinapanda na watu wategemee mabadiliko,nimeanzia chini napanda juu katika kuleta changamoto,Natamani watu wenye talents wazitumie bila kuogopa na wasikate tamaa,kwa mfano,nimehangaika na kipindi changu kwa miaka mitatu na sasa ndio naanza kuona matunda ya uvumilivu,ubishi wa kutimiza ndoto na kutokukubali kushindwa kufikia malengo.
Wasijali maneno ya watu ya kukatisha tamaa,mtu asimame kwenye anachokiamini na akifanyie kazi haijalishi itachukua muda gani.Nategemea,kuelimisha,kushauri na kuburudisha.
Niliacha kazi ITV 2008,then nika-join NGO from Canada lakini damu yangu iko kwenye media...nimeamua kurudi na kuacha kila kitu nyuma. Nataka kukamilisha ndoto zangu zote zilizosimama kwa miaka 4.
-Kipindi kinaanza tarehe 8 March,alhamis saa 3 kamili.
Msimamo wako Janet ndio unaohitajika. Mimi napenda kusoma vitabu na maandishi mengine kuhusu ujasiriamali. Mambo yanayosisitzwa ni kama hayo uliyoelezea, ambayo ni kama kuwa na lengo na kulizingatia, kuwa mvumilivu na ngangari hata kama kuna vipingamizi, na hata kama inachukua muda mrefu kuanza kuona matokeo unayotegemea.
ReplyDeleteUnatakiwa kuwa daima katika kujielimisha kuhusu shughuli unayofanya. Kujielimisha huko ni pamoja na kuelewa namna ya kukidhi matakwa ya wateja na kuwafanya waridhike na wafurahie huduma yako. Katika dunia hii ya ushindani mkubwa, huu ndio msingi madhubuti wa mafanikio, sio ufunge safari kwa mganga akakupe dawa.
Halafu, unatakiwa kuachana na watu wenye fikra za kujirudisha nyuma, fikra za kukuruisha nyuma, fikra za kutafuta vipingamizi na kusema hiki hakiwezekani, au huna hiki au kile. Watu hao achana nao. Andamana na watu wanaojituma na wenye imani na mwelekeo wa maendeleo na mafanikio. Utajifunza mambo ya maana.
Nimevutiwa na taarifa yako, na nakutakila mafanikio tele.
Congratulations! Hopefully umesajili kazi yako l;aa sivyo Clouds itakuzengua tuu!. Jina lako kamili ingekuwa bomba manake umezungumzia kwa utatu but we don't know your name. Picha na caption zinaonyesha "mtayarishaji" - ina maanisha wewe ni host pia?
ReplyDeleteJaneth Sosthenes Mwenda Talawa, safi sana.
ReplyDelete