AZANIA BANK LIMITED
Uongozi wa Benki ya Azania, (Azania Bank Ltd) unapenda kuwataarifu wateja wake na umma kwa ujumla kwamba kuna ujumbe wa simu (sms) unaotumwa kwao kutoka simu namba 0023222291029 ya kwamba wameshinda zawadi na wapige namba hiyo kufuatilia hiyo zawadi.
Benki ya Azania inawajulisha watu wote kuwa haihusiki na ujumbe huo na yeyote atakayeupata ujumbe huo asiujibu na aufute mara moja wakati tukiwasiliana na mamlaka husika kwa ufumbuzi zaidi.
Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.
IMETOLEWA NA UONGOZI WA AZANIA BANK LTD.
Usanii mwingine Jamani, kama huu wa simu na meseji watampata nani?
ReplyDeleteSi bora waende shamba wakalime tu?