Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiingia ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini kuongoza kikao cha tisa cha mkutano wa sita wabunge ambapo bunge linahitimisha shughuli zake mjini Dodoma.
Mbunge wa Bumbuli January Makamba akiwasilisha Hoja binafsi kuhusu sheria ya udhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi aliyoitoa chini ya kanuni ya 54 (1) ya kanuni za bunge toleo la 2007 ya kuliomba bunge kuazimia kwa kauli moja ,kuitaka serikali katika mkutano ujao wa saba kuleta Muswaada wa Sheria ya kudhibiti Upangaji wa Nyumba na Makazi kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wanaoishi mijini kutokana na adha wanazopata katika kutafuta nyumba za kupanga au kuishi kwenye nyumba hizo.
Mbunge wa Singida mjini Mohammed Dewji akimsikiliza kwa makini Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Stephen Wasira ndani ya ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Same Mashariki Anna Kilango akijadili jambo na Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema ndani ya ukumbi wa Bunge leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa (kushoto) , Pindi Chana (wapili kulia) na Catherine Magige (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyrli Chami kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Siasa, William Lukuvi akizungumza na Mbunge wa zamani wa Kasulu, Profesa Joseph Mbwiliza kwenye Ofisi za Bunge Mjini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Katibu Mtendaji wa jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu aliyemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula (kulia) akisalimiana na kubadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Bungeni Dodoma leo.
Balozi Mulamula akiwa na afisa wa Bunge Bw. Prosper Minja kabla ya kuanza kwa kiako cha Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.
Balozi Mulamula (kulia) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb) mjini Dodoma leo. Balozi Mulamula alifika Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo.
Spika Makinda akifurahia jambo na Mbunge wa Simanjoro Mhe. Ole Sendeka (kati) na mdau wa michezo nchini,Wakili Imani Madega.
Balozi Mulamula (kulia) akisalimiana na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) leo katika viwanja vya Bunge Dodoma leo. Katikati ni mdau Prosper Minja wa Bunge
Katibu Mtendaji wa jumuiya ya nchi za Maziwa Makuu aliyemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula (kulia) akisalimiana na kubadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda Bungeni Dodoma leo.
Balozi Mulamula akiwa na afisa wa Bunge Bw. Prosper Minja kabla ya kuanza kwa kiako cha Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.
Balozi Mulamula (kulia) akijadili jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb) mjini Dodoma leo. Balozi Mulamula alifika Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati hiyo.
Spika Makinda akifurahia jambo na Mbunge wa Simanjoro Mhe. Ole Sendeka (kati) na mdau wa michezo nchini,Wakili Imani Madega.
Balozi Mulamula (kulia) akisalimiana na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah (kushoto) leo katika viwanja vya Bunge Dodoma leo. Katikati ni mdau Prosper Minja wa Bunge
Huyu Mama ni mchapa kazi sana. Tunashukuru sana kwa mchango wako Balozi Mulamula.
ReplyDeleteMichuzi do u really proof read your headlines? you said Spika Anne Kilango??? since when did she become a speaker? hujatutendea haki wasomaji wa blog ya jamii..
ReplyDeleteMakamba ni Mbunge wa Bumbuli au wa Dar es Salaam ? Naomba majibu, make kila nionapo yupo Bungeni anatetea masilahi ya Mijini, Kuliko Vijijini Bumbuli??
ReplyDeleteNdio maana hatuendelei
Focus young Men and Show us what you got!
Naomba kuuliza wajameni, hivi wakigoma WABUNGE kuingia 'mjengoni' kuna athari gani kwa mtu wa kawaida? mfano waseme hatuingii mjengoni hadi rais asaini posho zetu? Au wagome walimu kama walivyogoma Madactari athari ni wapi zaidi?
ReplyDeleteinaonekana kabisa hao wabunge kinamama kila kunapokuwa na mapunziko au kumalizika kwa kikao cha bunge huwa wanamtafuta kwa makusudi mh.pinda ili wapigenae story
ReplyDeleteinaonekana mh.pinda ana mastory sana na ni mtu wa watu kiongozi anaekubalika kwa jamii sana maana anacheka na kila mtu hana majungu mtoto wa mkulima safi sana.
hao kina dada wabunge ,acheni hayo manywele ya bandia au kushinda saluni, nyie sasa ni viongozi so kuweni natural jamani, bado iko siku mtajiongezea makalio, angalieni wabunge wanaume , wako vile vile tu na nywele zao za kipilipili au kipara.
ReplyDeleteSasa wewe nae unataka kuleta mambo ya ujima hapa..nywele ya bandia inakunyima raha gani? Kwa hyo unataka wanyoe kpara km hao wanaume? Acha ushamba..ni stara kwa mwanamke kufnka kchwa kwa nywele au mtandio vitabu vya dini vnasema..afterall hela ya kufanya hvo wanayo..acha roho mbaya waache wadada wa watu wajiachie..
ReplyDeleteHongera sana January Makamba kwa mawazo yako chanya katika hili. Sijawahi kuwa shabiki wako sana, ila kwa hili unanifanya nikupende sana.
ReplyDeleteNashukuru kwa kuliona tatizo hili, huyo aliyepinga hapo nadhani ni mmoja wa wale wenye nyumba wanyanyasaji. Biiig Uuup January.
na wanaume mnapenda sana wenye manywele ya bandia, wengine mnaona ni washamba na natural hair zao! acha tu waweke nywele za bandia maana midume mnaona ndio zinapendeza
ReplyDeleteNywele Bandia kwa anayejua Vigezo vya Uzuri hawezi pendekeza kuzikubali!
ReplyDeleteUzuri upo pale pale hata kama mwanamke atanyoa Kipara!...wenyewe mnaona baadhi ya Warembo (Ma Miss) wanatoka na Vipara na vinawapendeza sana wakibaki Asilia!
Hivyo, kwa Ngazi ya Mtu kama Mbunge au KIONGOZI WA JAMII ni aibu kubwa kuwa na uzuri au Urembo wa bandia!
Hiyo kutumia nywele bandia ni dalili mbaya ya kutokujiamini kuwa vile ulivyo ndio Halisi zaidi!
mimi mke wangu siku akikaa minywele ya bandia ajue ndio talaka yake inakuja, yananuka kwanza kwenye daladala hewa hamna
ReplyDelete