Ankal akianiaka Ze Fulanazzzz a.k.a Kauka nikuvae jijini
Bonn March 11, 2008
 Ankal akila konozzzzz na malkia wa utangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani B. Ummy oumilkheir Hamidu alipotembelea kituo hicho cha redio ya Kimataifa jijini Bonn, Ujerumani March 11,  2008.
Jikumbushe zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Ankal,
    huku hivyo vijumba vya gorofa ni vya council tenants! sasa wewe walia vekesheni council tenants flats? Siku nyingine afadhali ulie visiga/nanyumbu/songea/tunduma nk kuliko hapo ndugu yangu. Usitangaze umaskini wako ankal!!!
    Jose.

    ReplyDelete
  2. Mithupu, nimecheka nilipoona hii. Jamaa ukujua wapi kuna mashine za kukaushia nguo?! Watu hawajakushangaa kuona unaanika nguo juani? Dah hii kali.

    ReplyDelete
  3. Sio bure, mganga wako atakuumiza

    ReplyDelete
  4. MADAKTARI WAMJIBU KIBONDE
    Ephraimu kibonde hii ndiyo shukrani yako kwa madr Nakumbuka sana mwaka 2007 , ukiwa hoi bin taabani wewe na mkeo namna madaktari walikuwa wanakuhudumia kwa huruma bila kukata tamaa! wakati we na mkeo mkiwa mmekata tamaa kabisa ya kuishi lakini madaktari wale walipigana kufa kuokoa maisha yako kimwili na kisaikolojia!
    wakati huo ulikuwa huwezi hata kutembea ukiwa umenyonyoka hadi nywele, tena siku moja daktari mmoja alisaidia kukubeba kutoka juu kukupandisha kitandani huku ukitoa udenda kwa udhoofu, daktari yule hakujali hali hiyo mbaya uliyokuwa nayo kwani alikubeba bila hata kuvaa gloves wakati nesi aliyekuwa anakuhudumia alipokuwa akihangaika kutafuta gloves ili aweze kukubeba, unajua ni kiasi gani daktari yule alirisk maisha yake ?? ungeweza kumuambukiza ugonjwa wako lakini alisahau hilo kwa huruma yake na kukuhudumia kwa roho moja.
    jitihada hizo hatimae ziliza matunda na maisha yako yaliokolewa!!

    sasa wewe kibonde ni fadhila gani kubwa sana au ni kiasi gani cha pesa ulichopewa na serikali hadi kusahau wema wa madaktari na kuweza kukaa na kuropoka ropoka ovyo hapo redioni?? wewe kweli kibonde of all the people ni wa kuwatukana madaktari tena hadharani??
    au umeshaahidiwa kutibiwa india maisha yako yote?? wewe na familia yako?? kumbuka kuwa wewe essentially we na mkeo bado ni wagonjwa na bado maisha yenu yako mikononi mwa madr! Hivi next time utakapoenda clinic pale.......... utaweza kumtizama dr wako usoni??
    Kibonde wewe kweli of all the people ?? mteja wa kudumu wa madr wa kila mwezi where the hell did u get the guts??
    KIBONDE DOMO NA NJAA VITAKUPONZA

    ReplyDelete
  5. Hahahaha Walahi niacheni nichekeeee!

    Ankal mara zote huwa unatuacha midomo wazi kwa aina ya maisha unayoishi!

    Hehehe sasa Mjomba hapo ndio Ujerumani kwenye kitovu cha Dunia kwa Viwanda,,,je wenye Viwanda vya Washing and Drying Machines wakale wapi?

    ReplyDelete
  6. KWELI MIDOMO MALI YENU NA KUAMUA KUSEMA CHOCHOTE PIA HIARI YENU, HIYO FULANA NI ICON AU SYMBOL (KIASHIRIA) CHA KAKA MICHUZI NA SI KWAMBA HANA NGUO ILA INA WAKATI WAKE WA KUVAA NA MWENYEWE NDIO ANAJUA LINI NA WAPI AIVAE, KWA NYONGEZA NIMECHUNGUZA HIYO FULANA SIO ILEILE YA AWALI(KWANZA) ILA ZAFANANAAAAAA..........

    ReplyDelete
  7. wewe mdau wa pili wacha ushamba wako wa kuona vitu ukubwani
    machine za kukausha nguo sio kila mtu anatumia na sio nzuri kutumia sana kwani zinaharibu nguo

    tena wakati wa summer ni nzuri kutumia juwa kukaushia nguo na sio machine

    nyie ndio wale mkiona nyumba ina machine ya kuosha vyombo basi mpaka sufuria la ugali mnataka kuosha na machine hehehehehe

    safi sana ankali mimi huwa namzimia sana huyo mama mtangazaji wa ujeru kiswahili sauti yake hana mpinzani.


    mdau tehran iran.

    ReplyDelete
  8. hivi siri ya ze fulanaaaazzzz ni nini Ankal? au ndio yale mambo ya maconfidence. bila hiyo mambo hayaendi? just curious!

    ReplyDelete
  9. Ankal wasikuyeyushe, kukausha nguo kwa mashine mara kwa mara kuna chakaza nguo. Wabongo kwa ulimbukeni!

    ReplyDelete
  10. Michuzi naona wayaendeleza mambo ya 'Kauka Nikukae'. Picha ya juu fulanaz imefuliwa, mara picha nyingine ushaikausha tayari umeivaa.

    ReplyDelete
  11. Mdau wa pili kwani hufahamu kuwa maschine za kukausha zinaharibu nguo haraka kuliko kuianuka na Ankali the fulana ndo hiyo hiyo ikiharibika itakuwaje?

    ReplyDelete
  12. Huna Nguo Nyingine?

    Hii Uniform?

    Au Mmasai Haahci Asili?

    ReplyDelete
  13. The Fulanazzzzzz.....oyeeeeeee!!!!!!!!

    ReplyDelete
  14. FULANA YA KIGANGA KWISHA.

    ReplyDelete
  15. hiyo ni library pic hiyo fulana ilisha chakaa na kakosa replacement. Hamto iona tena humu.

    ReplyDelete
  16. Anonymous wa Thu Feb 02, 11:03:00 AM 2012 toka tehran iran.

    Naomba unisamehe kama nimekukwaza. Hamna haja ya kuongea kwa kejeli na kashfa kwani hatufahamiani. Umeandika hivi;
    "wewe mdau wa pili wacha ushamba wako wa kuona vitu ukubwani"

    Ni kweli mie natoka shamba, nakukupendaga sana kwetu. Na wewe unatoka mji ghani vile!!? Tehran?.

    Kujibu hoja yako ni kwamba Ulaya(Ujerumani ndani) na Marekani wanatumia mashine kwa sababu ya kuokoa gharama. Vile vile wanajaribu kusave maji ili kusaidia mazingira, (maji waliyooshea yanaweza kwenda kutumika chooni vile vile. Na ushamba wangu wote huku nakoishi sijawi kuona watu wanaosha nguo kwa mikono, mpaka pale naporudi nyumbani Bongo, na nadhani ili ni kwa vile hatuna mashine nyingi kama zilivyo huku na umeme wa kuaminika.
    Na swala kuharibu nguo, ndiyo inawezekana zinaharibu. Lakini ukiangalia kwenye lebel ya nguo asilima kubwa zinakwambia uoshe kwa mashine au Dry Cleaner na nichache zinasema usafishe kwa mikono.
    Na ni kweli ukiosha nguo kwa mikono huku wanakushangaa kwani hali yenyewe sasa hivi ni baridi(winter) sio kama Bongo kusema utaanika nguo juani.(sijui,labda Iran)
    Asante kwa hoja zenu tushindane kwa hoja na vielelezo na si kejeli, matusi au kashfa, hayo ndiyo maendeleo.

    ReplyDelete
  17. Asalaam alaykhum ankal wajina safi sana kweli nimekusifu kwa kuitunza fulana hii kama kitambulisho chako inapendeza sana na we kweli ni mtunzaji keep it up ikifika miaka 10 kwa umaarufu wa hii fulana utaiuza kwa dola nyingi sana.

    wasalaam Chef Issa

    ReplyDelete
  18. Dah! kaka Michuzi sijui ulijuaje kumuweka Oumilkheir mana nilikuwa nataka sana kumuona anafananaje kwani nimeanza kumsikia toka niko primary school miaka ya 1990.. keep it up mama.

    ReplyDelete
  19. Michuzi hiyo fulana ikiibwa nina hakika utajinyonga.

    ReplyDelete
  20. Ankal hahaha inaelekea ukiwa hata Majuu huwa unauliza Wenyeji Mtoni au Kisimani ni wapi,,,nikafue?

    Kwa kweli inaonyesha bado unatumia kirungu na jiwe ktk kupiga nguo ukifua pamoja na majani ya mpapai mipango ya mwaka 1978 hukooo!

    Mjomba ubanaji matumizi wako ni hatari sana!

    ReplyDelete
  21. Hahahah Mjomba,

    Ukiwa Majuu unawakumbusha huko Wandugu maisha ya zamani wakiwa Bongo!

    Kwa Uasilia wako kwenda Bafuni unaweza omba upewe ndoo ya maji mkononi na kopo la kuogea!

    ReplyDelete
  22. Duhh aisee Ankal , Mjomba mipango yako ya ubanaji matumizi kiuchumi ni mpela mpela!

    ReplyDelete
  23. HETI !TUSIKIE MTU KAFIKA BEI ZE FULANAZZZZZZZZ,Tutakuja kumvua mtu mitaani,tena tunatoa onyo fulanazzz haiuzwi,
    Wadau
    FFU Ughaibuni

    ReplyDelete
  24. Ni kawaida yetu mtu akifikwa na matatizo ananyemelea banda la kuku, mbuzi au ng'ombe anachagua aliyenona amuuze kukidhi matatizo!

    Mjomba unaonaje Fulanazzzz yako tuiuze katika Mnada ili:

    1. Pesa tuchangie Waathirka wa Mafuriko Mabwe Pande?

    AU

    2.Pesa iongezewe katika fungu la nyongeza ya posho ya Madakitari waliogoma?

    Hilo ni wazo tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...