Madaktari mabingwa leo wamekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, Dk. Njelekela, kujadiliana kuhusu mgogoro wa madaktari, kwa lengo la kufikia muafaka wa suala hilo, ili kunusuru maisha ya wagonjwa nchini. Katika mkutano huo wanahabari hawakuruhusiwa kuingia.

Madaktari hao mabingwa wameazimia kwenda kukuktana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ili Serikali ikae meza moja na madaktari kufikia muafaka huo.



TAMKO LA CCM MGOMO WA MADAKTARI, POSHO ZA WABUNGE
 Kwa muda sasa nchi yetu imepitia kwenye tatizo kubwa la mgomo wa madaktari katika hospitali nyingi hasa za umma ambao kwa kiasi kikubwa mgomo huo umekuwa na madhara makubwa kwa watanzania masikini ambao ni wengi, kiasi cha kugharimu hata maisha yao.

Chama Cha Mapinduzi kinachukua nafasi hii kuwapa pole sana wale wote walioathiriwa kwa namna moja ama nyingine na mgomo huu. Na kwakweli tunasikitishwa sana na hali inayoendelea!

Chama Cha Mapinduzi kinawapongeza na kuwashukuru madakitari walioonyesha ubinadamu na uzalendo kwa kuamua kurudi kazini na ambao hawakugoma kabisa. Tunawashukuru na kuwapongeza kwani hakuna masilahi yanayovuka thamani ya uhai wa binadamu mwenzako!

Tunachukua fursa hii pia kuwashukuru sana na kuwapongeza askari wetu wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kizalendo wa kuamua kuitikia wito wa serikali kwenda kwenye baadhi ya hospitali kusadia kuwatibu watanzania wenzao. Moyo huu ni wa kizalendo na wa mfano. Tunajivunia uzalendo wa jeshi letu!

Tunachukua nafasi hii kuwaomba madaktari wanaoendelea na mgomo kurudi kazini huku wakiendelea na mazungumzo na serikali. Tunaamini madai yao yanawezekana kushughulikiwa ikiwa pande zote mbili zitaamua kukaa chini kwa dhati na kuzungumza.

Serikali kwa upande mmoja watafute kwa makini chanzo cha mgogoro huu na kutafuta majibu, na madakitari nao kwa upande wa pili, wawe tayari kukaa mezani na kuzungumza. Tunasisitiza thamani ya maisha ya binadamu ni kubwa kuliko masilahi na madai wanayoyaomba!

Serikali ni vizuri ikajenga utamaduni wa kushughulikia matatizo haya ambayo yanaathiri wananchi wengi kwa uharaka na udharura unaostahili badala ya kusubiri hali inapokuwa mbaya zaidi.

POSHO ZA WABUNGE
Kwa upande mwingine Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa juu ya swala la posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka zinazohusika na mchakato wa swala hili kuliangalia upya na kutumia busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa.

CCM inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya kuwawakilisha bungeni.

CCM inaendelea kuwasihi waheshimiwa wabunge walitafakari upya swala hili na busara itumike katika kuliamua huku wakifungua masikio kusikiliza sauti za Watanzania kwani huko bungeni  wana wawakilisha hawa Watanzania, ni vizuri kusikiliza hiki kilio chao! Si busara kupuuza kilio cha waliokupa dhamana ya kuwawakilisha.

Msimamo wa Rais Kikwete kama sehemu moja ya mamlaka inayohusika na mchakato huo ni uthibitisho wa usikivu wake kwa wananchi anaowaoongoza, yeye katimiza wajibu wake, tunawasihi waheshimiwa wabunge wetu nao walitafakari hili na kuona busara ya kuachana nalo kwasasa.

Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM
Itikadi na Uenezi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. NAPE NAKUPONGEZA SANA KWA CAMPAIN YAKO YA KUWA MKWELI NA MUWAZI HII POSHO YA WAPUNGE NI USHUZI MTUPU POSHO YA KWENDA BUNGENI YA NINI? KWANI MBONA WATU WENGINE HAWAPEWI POSHO KWENDA KWENYE VIKAO? ANKAL MICHUZI KWANI AMEUZULIA VIKAO VINGAPI KATIKA KIPINDI CHOTE CHA KULITUMIKIA TAIFA MBONA HAPEWI POSHO? DAWA NI KUWAMBIA WABUNGE WAENDE MUHIMBILI WAFANYE KAZI HATA YA KUOSHA WAGONJWA AMA KUPIGA DEKI HOSPITAL ILI WAPEWE HIYO POSHO. UKIPIGA HESABU WABUNGE JUMLA 300ZIDISHA MARA SHS. 330,000 HALAFU ZIDISHA MARA VIKAO 50 KWA MWAKA MZIMA UTAKUTA NI MAMILIONI YA SHILINGI YANAPOTEA.WATU WENYEWE WAKIFIKA BUNGENI NI KULALA NA KUSOKOTOA MENO NA TOOTH PICK. SAFI SANA NAPE BIG UP

    ReplyDelete
  2. KUACHANA KABISA NA SUALA LA POSHO NI MUHIMU.SUALA LA MADAKITARI LIPEWE KIPAU MBELE IS A PROFFESSIONAL AND IS THE HUMAN LIFE INVOLVED.asanteni

    ReplyDelete
  3. Kwani waheshimiwa wabunge walipokuwa wanaomba kuchaguliwa kuwa wabunge hawakujua kuwa ofisini kwao ni Dodoma ambako watatakiwa kuhudhuria vikao vya bunge?
    Kama walikuwa wanalijua hilo sasa posho ya kwenda kazini ya nini?

    Kwenda Bungeni ni sawa na mfanyakazi yoyote kuamka asubuhi na kwenda kazini sasa kila mtu alipwe posho kwenda kazini?

    Ndugu zangu wabunge tamaa inawaponza mnaonekana hamna maana na wananchi waliowachagua.

    Hongera sana Nape kwa kuwa mkweli na muwazi.

    ReplyDelete
  4. JK akimwaga wino wabunge wanakomba posho zaidi. Asipomwaga wino hawakombi. Ule usemi wa 'the buck stops here' ndio maana yake hiyo. Kama poooote huko busara ilikosekana busara itapatikania pale wino utakapokuwa haumwagiwi kwenye sheria.

    ReplyDelete
  5. Chonde chonde, Fanyeni haraka acheni Siasa angalieni hali halisi ya Wananchi na muokoe maisha yetu ambayo yako ukingoni!

    ReplyDelete
  6. KASIMBI WILLY aka GATUSOFebruary 02, 2012

    JAMANI EBU KILA UPANDE TIMIZA WAJIBU WAKE TAHASISI ZISIZO ZA KISERIKALI NA WANANCHI WOTE KWA UJUMLA EBU PAZA SAUTI KILA UPANDE ILI TUWEZE KUWASAIDIA NDUGU ZETU MADAKTARI NA SI KWA MADAKTARI TU ILA KWA PANDE ZOTE ZINAZOPIGANIA MASLAHI YAO IKIWA NA WALIMU KUHUSU POSHO ZA WABUNGE STOP STOP EMBU TUPIGE KELELE WOTE KWA PAMOJA SOTE NI WATANZANIA INAKUWAJE WAFAIDIKE WAO NA NCHI NI YETU SOTE?

    ReplyDelete
  7. Nape 4 President

    ReplyDelete
  8. Kuna kijiwe sehemu fulani walikuwa wanasema ooooo JK kaagiza suala la mishahara lirudi bungeni likajadiliwe kwa busara, mwingine akasema oooo watu wameshaanza kukomba posho mpya. Ukweli wa watu hawa ni upi?????? kwa waliokaribu na sehemu nyeti naomba msaada

    ReplyDelete
  9. Sasa hivi kwa Tanzania posho ndio wimbo wa Taifa, na tusipokuwa makini hata watoto wetu wakitaka kwenda shule watasema tuwalipe posho
    Madaktari wembe ni huo huo mpaka kieleweke na hakuna kiongozi kwenda kutibiwa nje, wote tuumie na huu mgomo, potea mbali acha tufe lakini haki ya madaktari ipatikane,m kazi zao ni ngumu na sio tu haki ya wafanyakazi wote zipatikane kwa wakati na sio msubiri mpaka wagome

    ReplyDelete
  10. Frank Shanel MdimiFebruary 02, 2012

    Tamko hili limeandaliwa vema na limejaribu vizuri sana kuchagua maneno yanayostahili kutumika. Kwa kweli limekaa vizuri. Ni ukomavu wa fikra na mtizamo. Daima tulenge kujenga lakini hatua zinatakiwa kuchukuliwa kwa upeo mpana zaidi. kwa mfano Taifa letu kwa sasa ni "net importer of commodity goods". Ili Tuweze kuwa na maslahi mazuri taifa lilenge kujikita katika kuongeza mauzo ya bidhaa nje ya nchi ama kwa kuuza bidhaa na mazao ghafi/yaliuyoongezwa thamani na bidhaa mbalimbali, au kuwaalika wawekezaji kuja kuzalishia hapa nchini kwa masharti nafuu na vivutio vizuri zaidi bidhaa zinazoagizwa zaidi kutoka nje. Pia tuimarishe miundombinu ya reli ili kujiunganisha kikamilifu na nchi za maziwa makuu. Hii itaibua ukuaji wa kasi wa uchumi mzima wa Tanzania na kuliwezesha taifa kupiga hatua katika kila nyanja ya maendeleo. Tujielekeze hivyo.
    Frank Shanel Mdimi.

    ReplyDelete
  11. Woooi, kilichobaki wote tuwe wabunge. Profesheno hazilipiiiiiii.? mnabisha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...