
Mchezaji Haruna Moshi (kushoto) wa Simba, akichuana na Sunday Paul wa JKT Orjoro katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Haruna maarufu kwa jina la Boban alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kipepsi mchezaji wa Orjoro.

Kikosi cha Simba, kilichopambana na Orjoro leo. Simba imeshinda mabao 2-0

Kikosi cha Orjoro kilichochuana na Simba leo. Picha na Kamanda Mwaikenda
huyo mwenye kapelo sio mkweche??
ReplyDeleteBoban alichezewa rafu nyingi sana za makusudi kwa nia ya kumchokoza na refa kwa sababu anazojua yeye hakufanya lolote, baadae akapata hasira na kufanya alivyofanya. Ni kweli alifanya kosa ambalo alistahili adhabu hiyo ila kama binadamu alitegemea atetewe na refa kabla hajajitetea mwenyewe.
ReplyDeleteKumfunga Askari katika mpira sio kigezo cha kuujua mchezo!
ReplyDeleteAskari hana mazoezi, mazoezi yake ni Gwaride kama mazoezi ya kukimbia ni mapaka kumfukuza Mhalifu aliyetoroka, na zaidi Mhalifu anakimbizwa meta chache anakuwa ameshakamatwa kwa msadaa wa Wananchi Raia wema anabidhiwa kwa Askari!
SIMBA fungeni mkanda!,,,mtafungwa na YANGA mkifanya mchezo!