Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk.Diodorus Kamala akiagana na Mama mzazi wa Waziri mkuu,Mizengo Pinda,Albetina Kasanga mara baada ya kutembelea familia hiyo katika kijiji cha Kibaoni mkoa mpya wa Katavi leo,kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia,Dk James AlexMsekela,nyuma ni Balozi wa Tanzania nchini Misri,Mohamed Hamza,mabalozi hao wako katika ziara ya kutembelea Hifadhi za Taifa iliyoandaliwa na TANAPA kuongeza uelewa wa kuvutia watalii katika nchi wanazowakilisha.
Baadhi ya Mabalozi wanaowaiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja na mama wa Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,Albetina Kasanga(wa pili kushoto)na mdogo wake Waziri Mkuu,Wolfgang Pinda(kulia)waliosimama kutoka kushoto ni  Balozi Dk.James Alex Msekela(Italia)Balozi Dk.Diodorus Kamala(Ubeligiji)Dk Ladislaus Komba(Uganda)na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Dk.Rashid Rutengwe,waliokaa kushoto ni Balozi Philipo Marmo(China)na Balozi Mohamed Hamza(Misri)wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu kijijini cha Kibaoni mkoa mpya wa Katavi leo,mabalozi hao wako katika ziara ya kutembelea Hifadhi za Taifa iliyoandaliwa na TANAPA kuongeza uelewa wa kuvutia watalii katika nchi wanazowakilisha.Picha na Filbert Rweyemamu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Naona Wolfgang kopi kabisa na Mizengo, si mchezo!

    ReplyDelete
  2. We anony wa kwanza, elewa kuwa hawa wazee wetu wa zamani walikuwa hawana longolongo wala kuchakachua kwenye ndoa zao.
    Hata ukipima DNA za watoto 15 kwenye familia moja wote wanakuwa sawa.

    Abiola Jr.
    Mafia kiduka cha juice

    ReplyDelete
  3. Wolfgang acha kuvaa nguo za kaka yako!!!

    Tamim, Ohio

    ReplyDelete
  4. Hivi mbona TANAPA imewabagua Mabalozi wakike? Ama wao walisharipoti kazini na hawa jamaa wengine wanauswaga tu?

    ReplyDelete
  5. watujuze kama PM na Wolfgang ni twins!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...