Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dk.Diodorus Kamala akiagana na Mama mzazi wa Waziri mkuu,Mizengo Pinda,Albetina Kasanga mara baada ya kutembelea familia hiyo katika kijiji cha Kibaoni mkoa mpya wa Katavi leo,kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia,Dk James AlexMsekela,nyuma ni Balozi wa Tanzania nchini Misri,Mohamed Hamza,mabalozi hao wako katika ziara ya kutembelea Hifadhi za Taifa iliyoandaliwa na TANAPA kuongeza uelewa wa kuvutia watalii katika nchi wanazowakilisha.
Baadhi ya Mabalozi wanaowaiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja na mama wa Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,Albetina Kasanga(wa pili kushoto)na mdogo wake Waziri Mkuu,Wolfgang Pinda(kulia)waliosimama kutoka kushoto ni Balozi Dk.James Alex Msekela(Italia)Balozi Dk.Diodorus Kamala(Ubeligiji)Dk Ladislaus Komba(Uganda)na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,Dk.Rashid Rutengwe,waliokaa kushoto ni Balozi Philipo Marmo(China)na Balozi Mohamed Hamza(Misri)wakiwa nyumbani kwa Waziri Mkuu kijijini cha Kibaoni mkoa mpya wa Katavi leo,mabalozi hao wako katika ziara ya kutembelea Hifadhi za Taifa iliyoandaliwa na TANAPA kuongeza uelewa wa kuvutia watalii katika nchi wanazowakilisha.Picha na Filbert Rweyemamu
Naona Wolfgang kopi kabisa na Mizengo, si mchezo!
ReplyDeleteWe anony wa kwanza, elewa kuwa hawa wazee wetu wa zamani walikuwa hawana longolongo wala kuchakachua kwenye ndoa zao.
ReplyDeleteHata ukipima DNA za watoto 15 kwenye familia moja wote wanakuwa sawa.
Abiola Jr.
Mafia kiduka cha juice
Wolfgang acha kuvaa nguo za kaka yako!!!
ReplyDeleteTamim, Ohio
Hivi mbona TANAPA imewabagua Mabalozi wakike? Ama wao walisharipoti kazini na hawa jamaa wengine wanauswaga tu?
ReplyDeletewatujuze kama PM na Wolfgang ni twins!!
ReplyDelete