Mmoja wa majeruhi waliogongwa na gari lenye namba T489 AGJ aina ya Toyota Bw. Elias Ngole almaarufu Ngoswe ambaye ni mpiga picha maarufu mkoani Tanga, aliyefika kwenye mahafali ya kidato cha sita katika shule hiyo ya Korogwe Girls akiwa amepakiwa kwenye bajaj kukimbizwa katika hospitali ya magunga kwa matibahu
Mkuu wa wilaya ya Korogwe (mwenye suti nyeusi) akiwa amemshika mwanafunzi Kibibi Mmasa (19) ambaye ndiye anayetuhumiwa kuendesha gari hilo kwa kuliweka gea kisha gari hilo kurudi nyuma na kuwagonga wanafunzi wenzake na kuwasababisha majeraha makubwa mwilini.
Mwanafunzi Renata Renatus anayesoma kidato cha sita katika shule hiyo, akiwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe akihudumiwa na muuguzi alipofikishwa katika hospitali hiyo.
Gari lenye namba T 489 AGJ likiwa limesimama katika eneo la shule baada ya kutuhumiwa kuwagongwa wahitimu wa shule hiyo waliokuwa wamesimama wakisubiri sherehe za mahafali hayo.
Picha na Mashaka Mhando wa Globu ya Jamii, Tanga
Hivi ina maana kaka wa huyo bint aliyetumwa kuchukua vitu katika gari aliacha gari likiwa silence au hi huyo bint alitaka kuonyesha manjonjo huku hajui gear za gari zinafanyaje kazi? ona sasa matatizo aliyosababisha sababu ya ubishoo wake na dereva yeyete haruhusiwi kuacha gari wazi huku likiunguruma lazima uzime na kufunga milango .huyo hakutumwa ni ubishoo sheria ishike mkondo ashike adabu
ReplyDeleteHuyu Kibibi mchawi nini? mambo gani haya huyo kaka yake asiachiliwe mpaka aeleze ni kwanini aliliegesha gari lake maeneo hayo, kwani hakuna magari mengine yaliyokuja kwenye maafali. kina mambo walitarajia kuyafanya yakishirikina. Na kwanini amtume mdogo wake asiende yeye mwenyawe? hapo inabidi wote wawe chini ya ulinzi mkali na watoe taarifa zote.
ReplyDeleteDah! Poleni sana.
ReplyDeleteLakini Kaka mbona nashindwa kuelewa?!?
Ina maana hilo gari Kaka yake aliliacha kwenye "silence", au Dogo aliliwasha, au?
Maana sipati picha gari kama limezimwa halafu uweke gia ya rivaz tu halafu lianze kwenda!
Hebu tuelezee zaidi hapo. Maswali ni mengi kuliko majibu.
Tafadhali
aliupata vipi huo ufunguo wa gari???hukumu ya huyu mwanafunzi ndio utajuwa majaji wa kiafrika hawana busara. wanaweza kumpiga hata miaka kwa walivyokosa busara.
ReplyDeleteDereva mzuri hawachi ufunguo kwenye gari. Jee ingekuwa jambazi si ndiyo angeondoka nalo kimoja?
ReplyDeleteHapo ni uzembe wa dereva kaka yake, aidha ametoa ufunguo kwa makusudi au amewacha kwenye gari.
Nakubaliana na mdau wa hapo juu jee alitoka ndani ya gari na huku inanguruma? Hapa kuna utata kidogo.
HAMNA LOLOTE, HUYU BINTI ALIKUWA ANATAKA KUONESHA MANJONJO NA UBISHOO KWA WENZAKE. !!l:@{{@@mbafff >?:@Psasana huyu.
ReplyDeletejamani acheni kuropoka ovyo. hii ni accident tu. huyo mwenye kumuita huyo mtoto wa watu mchawi hana aibu. one time nikiwa likizo tanzania niliingia kwenye gari la dada yangu ambalo alikuwa ameliacha kwenye silence then hilo gari likaanza ku move na mimi nilikua sijui kuendesha gari that time. kitu kilicho niokoa ni kwamba kulikuwa na watu karibu. mmoja wao aliweza ku jump into the car then akalisimamisha. thank you god for that.
ReplyDeleteHili ni tukio la kawaida kwa vijana..Mie nilikuwa naosha gari langu wakati wanangu wako ndani ya gari. Mmoja miaka 5 mwingine 3. yule wa miaka mitano akaliwasha . Mie mwenyewe sikujua lilirudi vipi rivas wakati huo nilikuwa nasafisha wind screen. bahati nzuri lilijikita kwenye matofari na kusimama. Haya mambo bwana kwa vijana na watoto ni kawaida ila tuchukue tahadhari kila mara .Poleni sana Mungu awape nguvu
ReplyDeleteAnkal
ReplyDeleteAjali imetokea ndiyo hatuwezi kukataa hilo, ila swali ni kuwa UDEREVA unasemaje unapolifikisha gari mahali pa kusimama? Waliosoma udereva wanajua na pia askari wanajua. Huyu binti kwa mujibu wa sheria za nchi yetu si mtoto hivyo atatakiwa kuiridhisha sheria kuwa hakuwa mzembe, na si yeye tu bali hata kaka yake. Tuache sheria ichukue mkondo wake ili kila mmoja wetu apate somo katika hilo. Hivi ukiacha silaha hovyo ikatumika vibaya inakuwaje?
Ajali ni ajali tu,mbona wabunge wapatapo ajali kelele kama hizi mbona hazipo?Mpeni binti pole na kumpongeza kwa kutoleta maafa makubwa.
ReplyDeleteDah! Poleni. Huu si wakati wa kulaumiana, imeshatokea. Tuwaombee majeruhi wapate nafuu na waweze kufanya mitihani yao salama. Enyi wenye imani haba mshindwex100, mnakimbilia kwenye uchawi kwa nini! Ilishawahi kutokea nyumbani kwangu ambapo gari iliwahi kutoka kwa kasi na kubomoa geti kisha lika ruka mtaro wa kwanza barabara ya lami mtaro wa pili na mwisho likaishia kuvunja kibanda cha mamalishe. ILIKUWA BAHATI WAKATI LIKIWA LINA CROSS BARABARA HAPAKUWA NA GARI LIKIPITA WAKATI ULE. Nakumbuka mamalishe hao walikuwa wanamaneno mpaka niliwajengea kibanda chao, BAADAYE WAZEE FULANI WALIWASEMA KUWA KUMLIPISHA JIRANI. WAPENDWA, MBONA TUMESAHAU KUWA TU WASAFIRI!!! TUSISHABIKIE LEO KWAKE KESHO KWAKOOOO...!!!
ReplyDeletejamani macheni lawama hiyo n ajali 2. 2simlaumu huyo mtt hata mm ilisha nitokea gari ikawa ina move 2kaokolewa na waliokuwa nnje. poleni sana mungu atawaponya namtafanya mtihani kwa amani
ReplyDeleteNI KWELI KABISA ULIYOYASEMA WEWE MDAU WA HAPO JUU. HATA MIMI MWENYEWE NI DEREVA LAKINI NILISHAWAHI KUPATWA NA BALAA LA GARI KAMA HILO. KWA HIYO TUSILAUMIANE JAMANI, LEO KWANGU KESHO KWAKO. SIJUI PIA UTAJIONA NI MZEMBE?
ReplyDeletejamani tusilaumu kuzidi kipimo,ni mpango wa mola wala hatupaswi kulaani kinamna hiyo,cha kuomba mungu awasaidie majeruhi wapone haraka.
ReplyDeleteasanteni,..
mi naona huyo bint alikua anajionyesha kwa wenzake nae wamuone anajua kuendesha gari matokeo yake ndio hayo
ReplyDeleteJamani naombeni msaada kwa hili...1: je hili gari lilikuwa ni Automatic au Manual? 2: Lilikuwa Silence au lilikuwa limezimwa kabisa? 3: Kama lilikuwa limezimwa inamaana huyu binti aliliwasha na kuweka gia maana lisingeweza kurudi nyuma bila kuwa switch on 4: Huyu binti alitumwa nini na kaka yake kwenye gari na hicho kitu alichotumwa kina uhusiano gani na kushika sehemu nyingine za gari kama gia au switch....yeye ametumwa akachukue kitu sasa hizo sehemu nyingine za gari zinamuhusu nini? Sheria ichukue mkondo wake na huyu binti afungwe miaka 30 ili iwe fundisho kwa watu wengine....kama gari ilikuwa imezimwa na kufugwa milango basi kaka mtu hana hatia yeyote
ReplyDeleteMDAU Kenny john
This is just an accident. The poor girl did not intend to hurt her schoolmates and others. She may be 19 but she's still a kid. This thing was not intentional. Wa kuulizwa maswali hapa ni kaka mtu. Ilikuwaje mpaka huyo binti akajaribu kuendesha gari wakati hajui kufanya hivyo?
ReplyDeleteThis is just an accident. The poor girl did not intend to hurt her schoolmates and others. She may be 19 but she's still a kid. This thing was not intentional. Wa kuulizwa maswali hapa ni kaka mtu. Ilikuwaje mpaka huyo binti akajaribu kuendesha gari wakati hajui kufanya hivyo?
ReplyDeleteHii ni ajali wacheni sheria ya nchi ichukue mkondo wake. je pale inapotokea baba amerudi kutoka safari ghafla mtoto akakurupuka na akalifuata gari uso kwa uso na baba yule kwa bahati mbaya zaidi akamgonga na kufa hapohapo. au anakuta maturubai yametandikwa kwa chini watoto wamejilaza then jamaa anarudi kutoka kazini na kuyakanyaga maturubai yale kumbe ndani watoto wanacheza bila kujua akamkanyaga mtoto wa jirani yake na kumbastisha hapo hapo akafariki dunia na wengine wakaumia vibaya. inasikitisha sana tena inauma kama una moyo mwepesi unaweza kufanya mambo................ jambo muhimu ni kumtanguliza mungu. Ila Tahadhari inatakiwa sanasana, jihadhari kabla ya hatari japokuwa ajali haina kinga. poleni sana majeruhi nanyi mliosababisha ajali, pamoja na familia zenu. Mungu awabariki.
ReplyDeleteanoy 8:35:00am gudpoints!
ReplyDeletePoleni walioumia na Mola awajalie mpate nguvu muendelee na ujenzi wa Taifa letu. Huyu anonymus wa Fri Feb 03, 08:35:00 AM 2012 mbona haieleweki kama hilo gari lilijiwasha lenyewe na kuondoka na kuruka mtaro au kulikuwa na mtu ndani ya gari aliyeliwasha. Ameeleza nusu nusu. Halafu jamani kila ajali mnamsingizia Mungu. Wewe hujui kuendesha gari unakwenda liwasha na kuanza kukanyaga mafuta. Ikitokea ajali eti Mungu alipanga hivyo. Wakati mwingine tukubali kuwa ni UZEMBE.
ReplyDeleteHABAR ZENU,sielew tatizo ila nakumbuka enzii hzooo ndio nakua kua age kama huyo bint nmepata akil na mm nataka kujua gar kilishawah kunitokea kisanga,kla siku namuomba kaka yangu anfundshe gar anaringa ringa,sasa nkamtegea siku moja kashuka tu katka gar anashangaa shangaa..nikaingia ndani,enzi hzo n manual!mnajua msala wa manual ktk gear lnakua kama lnaruka then lnatulia...tangia siku hyo kiherehere klntoka na nkasubr kufundshwa gar..so huyo bnt si kosa lake ,nahs altaka kutamba kwa friends kwamba she can drve..ikamcost...wamsamehe tu as n utoto fulan ambao akija kuhaddhiwa akiwa mkubwa hatataka kuamin
ReplyDeleteNAWAPA POLE WALE WOTE WALIOUMIA.
JAMAN NDUGU ZANGU HUYU BINTI HAKUZAMILIA KUFANYA KITENDO HICHO, KWANI HAPA DUNIANI HAKUNA BINADAMU ALIYEKAMILIKA LEO UNAMUTOLEA SHUTUMA NA MANENO KWA SABABU KAKOSA YEYE LAKINI KUMBUKA USEMI USEMAO LEO KWANGU KESHO KWAKO, HIVYO HATUNA BUDI KUSAMEHE KWANI HATA SISI SOTE TUNASAMEHEWA NA MWENYEZI MUNGU MAKOSA YETU HAIJALISHI NI KOSA LA NAMNA GANI LAKINI BABA YETU HUTUSAMEHE! MIMI NAOMBA TUMUSAMEHE NA TUWAOMBEE WALIOUMIA ILI WAPATE NGUVU NA WALEJEE KTK HALI ZAO ZA KAWAIDA.
ReplyDeleteAMEN!!!!!!!!