Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi wakati alipofika kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba 14 za Watumishi eneo la Lugongwe, Utete Wilaya ya Rufiji leo alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Pwani. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asli ya kabila la Kisukuma, wakati wa makaribisho yake alipowasili mji mdogo wa Utete Makao Makuu ya Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kuanza ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Nyumba 14 za watumishi, zinazoendelea kujengwa eneo la Lugongwe, Utete Wilaya ya Rufiji, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameanza ziara ya mkoa wa Pwani ambapo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo.
Makamu wa Rais kama mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)ni mlezi wa CCM mkoa wa Pwani na kwamba atatumia fursa hiyo pia kuhamasisha uhai wa chama.
Ziara yake hiyo itakayochukua siku nne inaanzia katika wilaya ya Rufiji baadaye Mkuranga,Bagamoyo na itamalizikia wilaya ya Kibaha Februari 4,2012.
Hata hivyo,siku inayofuata Makamu wa Rais atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM zitazofanyika Mlandizi mkoani Pwani.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
Februari 1,2012
Mhhhh ngoma ya kisukuma rufiji tena katika ziara ya mkoa wa rufiji. kazi kweli kweli
ReplyDelete