Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), Ephraim Mgawe (kulia) akimkabidhi Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga hati ya makubaliano ya kusaidia kupunguza msongamano wa makontena katika bandari ya Dar es Salaam kwa kuyahamishia katika Bandari Kavu. Hafla hiyo ilifanyika eneo la Bandari hiyo leo, ambapo taasisi nyingine nne zilipata hati hizo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Naibu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Patrick Kisaka (kushoto) akipokea hati hiyo.
Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage (1980) LTD, Ali Hussein Lilan akipokea hati hiyo kutoka kwa Mgawe.
Katibu Mkuu wa Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Peter Kirigini (kushoto), akipokea hati
Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia makabidhiano hayo
Viongozi hao wakitiliana saini mkataba huo
Wakitiliana saini mkataba huo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TICTS, Nathan Bissett akikabidhiwa hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa THA, Mgawe. 
Picha na Kamanda Mwaikenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ankal hivi sasa Bandari ni TPA yaani (Tanzania Ports Authority) na sio THA (Tanzania Harbours Authority)!

    ReplyDelete
  2. Hili wala halikustahili kuingia humu. Kulundikana kwa makontena hapo bandari ya Dar ni sababu ya ukiritimba usioisha na rushwa. Ukienda utaambiwa meli hiyo haijafika wakati ukiangalia kwenye mtandao unaona ilikwisha shusha mizigo na labda meli hiyo inaelekea Cape Town (Afrika Kusini). Hayo ndiyo matunda ya rushwa.

    ReplyDelete
  3. tunawaomba msitudanganye this time 1 months sio ideal kwa kutoa container. pull your soksi up

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...