
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA), Ephraim Mgawe (kulia) akimkabidhi Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA), Stephen Ngatunga hati ya makubaliano ya kusaidia kupunguza msongamano wa makontena katika bandari ya Dar es Salaam kwa kuyahamishia katika Bandari Kavu. Hafla hiyo ilifanyika eneo la Bandari hiyo leo, ambapo taasisi nyingine nne zilipata hati hizo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Naibu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Patrick Kisaka (kushoto) akipokea hati hiyo.

Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage (1980) LTD, Ali Hussein Lilan akipokea hati hiyo kutoka kwa Mgawe.

Katibu Mkuu wa Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA), Peter Kirigini (kushoto), akipokea hati
Baadhi ya wageni waalikwa wakishuhudia makabidhiano hayo

Viongozi hao wakitiliana saini mkataba huo

Wakitiliana saini mkataba huo

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TICTS, Nathan Bissett akikabidhiwa hati ya makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa THA, Mgawe.
Picha na Kamanda Mwaikenda
Ankal hivi sasa Bandari ni TPA yaani (Tanzania Ports Authority) na sio THA (Tanzania Harbours Authority)!
ReplyDeleteHili wala halikustahili kuingia humu. Kulundikana kwa makontena hapo bandari ya Dar ni sababu ya ukiritimba usioisha na rushwa. Ukienda utaambiwa meli hiyo haijafika wakati ukiangalia kwenye mtandao unaona ilikwisha shusha mizigo na labda meli hiyo inaelekea Cape Town (Afrika Kusini). Hayo ndiyo matunda ya rushwa.
ReplyDeletetunawaomba msitudanganye this time 1 months sio ideal kwa kutoa container. pull your soksi up
ReplyDelete