Baada ya kumaliza degree yake ya sheria mlimani Bwana Rwegoshora aliamua 
kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya 
kuhudumia clients(wateja) .

Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake,alimuona kijana 
mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake.Hapo ndipo alipoanza 
kunyanyua mkono wa simu ya TTCL,wakati anajizungusha kwenye kiti cha kuzunguruka
.
 
Wakati kijana alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha wakati 
anaongea na simu,alisikika akiongea ''No.no, no, Absolutely no, You 
tell those clowns in New York that I won't settle this case for less 
than one million. (pause)

Yes, yes . The Appeals Court has agreed to hear that case next week,
I'll be handling the primary argument and the other members of my team 
will provide support. Okay. Pliz dont forget to tell the State 
Prosecutor that I'll meet with him next week to discuss the details."

Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora 
anajinyonganyonga kwamuda zaidi dakika 5.
 
Baada ya kumaliza kuongea na simu,bwana Rwegoshora alielekea kwa huyu jamaa.
''Samahani sana, kwa kukupotezea muda wako, unajua tena kazi zetu hizi 
unaumiza kichwa sana,kama unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani niko 
busy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka mwenyewe. enh by the way,
what can i do for you?Jamaa alijibu.

'' Mimi ni mfanyakazi wa TTCL,nimekuja kuunganisha line yako ya simu
kwani haipo hewani''

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. wakati simu zinaingia sistaduu mmoja akazuga kwamba ye mda wote yupo hewani kumbe hamna kitu,sasa ile anatuzuga anaongea simu ikaita kweli wakati ipo sikioni acha aitupe

    ReplyDelete
  2. yaani hujakosea. hawa ndugu zetu wanahitaji maombi!

    ReplyDelete
  3. hahahahah, mbavu zangu mie!

    ReplyDelete
  4. maombi??? maombi gani?

    ReplyDelete
  5. hahahaha siku moja moja tucheke jamani sio kila siku malalamiko

    ReplyDelete
  6. Hiki ni kichekesho kama vingine. Lakini kuna mafunzo: Inawezekana wizi wa line za simu upo na hili ni funzo kwa watu wa namna hiyo. Zao ni arobaini. Pia inawezekana kuwa ni njia ya kuji-promote kwa Mwanasheria huyu ili aonekane mbele ya yule kijana kuwa ni learned brother kweli kweli. Sikubaliani na maoni kuwa'Hawa ndugu zetu wanahitaji maombi'. Kila kabila lina matatizo yake. Wengine hawajui uongozi, wengine ni wavivu, wengine ni viazi tu lakini warembo sana, n.k.

    ReplyDelete
  7. Anonymous wa Wed Feb 29:07:34:00 AM 2012

    Nakuunga mkono!

    Mdau umemaliza kila kitu nilchotaka kusema,,,wizi,,,majigambo unajua Ukanda wa Ziwa haswa BK kule,,,kila mtu anataka ajulikane amesoma na anazungumza Kiingereza hata kama hajasoma!

    Heheheh,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...