Asalaam aleykum kaka,
Hongera na pole kwa kazi za kila siku katika harakati za kupasha uma wa Watanzania kokote pale duniani. Tafadhali naomba unirushie maoni yangu kuhusu ufanisi wa shule za Kata.
Naomba nichangie kuhusu hili suala la shule za kata na ukosefu wa walimu. Binafsi ninayo maoni tofauti na wengi wanaozibeza kwamba ni mzigo na hazina tija hata kidogo katika maendeleo ya elimu Tanzania.
Kusema ukweli wengi tunakumbuka enzi zile ambazo kulikuwa kuna uhaba wa shule za sekondari kiasi kufaulu darasa la saba ilikuwa ni ndoto za alinacha. Kwa vile wakati ule shule za sekondari hazikuwa nyingi nap engine kila mkoa ulikuwa na walau shule moja au mbili, na kulikuwa na shule zile za kitaifa zilizochukuwa wanafunzi kutoka kila kona ya nchi. Hapo utataja shule za Mazengo, Mkwawa, Ilboru, Msalato, Tabora Girls, Tabora Boys na Mzumbe kutaja chache.
Nafikiri ni kwa kutambua uhaba wa shule za sekondari za kutosha na pia ile hamu kubwa ya kukata kiu ya kupata elimu kwa kila mtanzania ndio serikali yetu ikaja na mpango wa kupanua elimu kwa kuongeza idadi ya shule kwa kuanza na mpango wa shule za msingi na baadae kufuatia na ule mpango wa shule za sekondari.
Kwa bahati mbaya katika utekelezaji wa mipango yote hiyo kumekuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa walimu na vifaa vya kufundishia kwa ngazi zote. Na kutokana na hili ndio maana watu wengi wamekuwa wakikashifu na hata kutoa kejeli kwa mpango mzima ambao mbali na mapungufu hayo umekuwa na mafanikio ya wastani lakini ambayo ninayo matumaini yatakuwa endelevu.
Kwanza kabisa ni dhahiri kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na sekondari tangu kuanzishwa kwa mpango huu. Na hapa wengi wanakosoa kwamba hili halina tija kwa kuwa kwa changamoto zilizopo katika shule zinafanya elimu itolewayo kuwa ya chini na isiyo na tija.
Katika hili sipangani na wanaotoa kasoro hizi ingawa naamini bado hata katika hilo kundi la shule za kata wapo baadhi ya watoto wetu wanaofaulu na kuendelea mbele na elimu za juu, tofauti na namna ilivyokuwa zamani wakati ambapo hata upenyo wa kuingia kwenye mfumo wa elimu haukuwepo.
Baada ya kujaribu kutoa hayo maelezo machache sasa naomba nieleze jambo moja ambalo mimi nafikiri linaweza kusaidia kupunguza changamoto ya ukosefu wa walimu katika hizi shule. Nimejaribu kupitia mfumo wa ukopeshwaji wa miko[o kwa ajili ya elimu ya juu na suala la kujiunga na mfumo wa Jeshi la Kujenga Taifa (National Service) na hapa ndio nikaona kuna mwanya wa kupata suluhu ya tatizo hili.
Nionavyo mimi serikali inapaswa iandae mpango ambao utwalazimisha wanafunzi wanaohitimu katika vyuo mbalimbali nchini kwenda kufundisha katika hizi shule za kata kwa walau kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa kufanya hivi serikali itatakiwa kuwapa posho za kujikimu wahitimu hawa na kwa kiasi fulani cha mshahara, kiasi kinaweza kukatwa kufidia mkopo ambao wahaitimu walikopeshwa na serikali kugharamia elimu za chuo kikuu.
Wapo wanaoweza kuona mpango huu hauna mantiki, lakini kiukweli katika wakati tulionao hatuna suluhisho la haraka na la unafuu kama hili. Wanaweza kuja wasemaji, kwamba wahitimu hao hawatakuwa na weledi wa kiualimu, lakini jawabu ni kwamba katika Tanzania tumekuwa na programu nyingi za kuwapika walimu kwa muda na baadhi zimeweza kutoa walimu ambao wengi tumepitia kwao. Tunakumbuka mpango wa UPE, Mama Sita Programe (VODA FASTA) nk.
Lakini mbali na hilo serikali pia itatatua kwa kiasi tatizo la wahitimu wa vyuo vikuu kukwepa kulipa mikopo baada ya kuhitimu.
Ili kutekeleza na kusimamia mpango huu serikali inapaswa kuwa na mpango wa kutoa vyeti maalumu vitakavyotolewa kwa wale watakaomaliza vyema muda wao kufundisha na hicho ndio kiwe kibali kwa taasisi kumuajiri mhitimu wa chuo.
Najua viongozi wetu wanao nafasi ya kujifunza zaidi namna bora ya utekelezaji wa mpango na mipango zaidi ya kukwamua sekata ya elimu na nyinginezo, kwa hiyo kwa kujifunza zaidi namna ya utekelezaji wanaweza kujifunza katika nchi ya Ghana namna hizi programu zinavyoendeshwa.
Naomba kuwakilisha
Mdau wa Elimu
Kama minimum Salary itakuwa TZS 2Million, ni dhahiri wengi watakuwa tayari kujitolea na matokeo ya baada ya miaka minne tangu kuanzishwa mpango huo yatakuwa ni record high.
ReplyDeleteWewe umeongea point kwani wahitimu wa vyuo vikuu wanazurula mijini kutokana na tatizo la ajira hiyo itasaidia wanafunzi na hata hao wanavyuo walio hitimu ambao wana zurula mitaani wapate ajira kwani ni hatari kwa taifa kkukutana na jambazi msomi au changudoa msomi
ReplyDeleteMheshimiwa nafikiri ana wazo zuri, linastahili kupewa nafasi ya kujadiliwa.
ReplyDeleteUalimu ni wito sio kulazimishwa hata kidogo. Mtu anapofanya kitu anachopenda matokeo siku zote huwa ni mazuri, anakuwa mbunifu na anaboresha kazi yake kadri muda unavyoenda. Watu wengi wangependa kuwa walimu ila kwa vile hakuna malipo na kazi yenyewe inabezwa ndo maana tunahangaika.
Kwahiyo mi naona tuwe na mipango ya muda mrefu. Kwanza walimu walipwe mshahara wa maana, I mean millions. Ukiwalipa vizuri hata kama shule iko tandahimba watu wataenda tu
Hoja ni nzuri kwa kuwa imeangazia hata nje ya nchi, lakini...
ReplyDeleteSerikali ikiwalazimisha wahitimu wa vyuo kufundisha ni kujichimbia shimo! Kufundisha inahitajika saikolojia zaidi si kama Jeshi ambapo kila kitu ni amri (hakuna mjadala).
Wale wa VODA FASTA wanaenda kwa hiari yao. Walimu walipogoma kwa kudai maslahi yao, serikali iliwalazimisha kufanya kazi, wengi wakaingia madarasni na kupiga stori, kukejeli serikali n,k matokeo yake ZERO.
SULUHU: serikali iwe na mipango sahihi ya kuboresha sekta ya Elimu ili kuwa na Taifa imara. Maboresho yahusu vitendea kazi, kushughulikia madai n.k. Kuna wahitimu wa Ualimu wanaoenda nje kufundisha kwa kuwa MAZINGIRA YA KAZI NA MASLAHI YANARUHUSU. Hapa Tanzania Ualimu unaonekana kama adhabu, fani yenye watu wasio na uelewa n.k
Hii mipango ya muda mfupi ndio inayoligharimu Taifa. Jaribu kufuatilia mifumo ya kuandaa Waalimu utagundua tatizo. Ukweli ni kwamba, maboresho yanafanyika kisiasa zaidi.
Baba wa Taifa aliwahi sema "tunakoelekea tutakuwa na shule za sekondari zisizo na waalimu, vitabu..."
UALIMU ISIWE NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU:
ReplyDeleteKama Wadau waliotangulia suala kubwa inabaki ni ''Maslahi'' yaani MSHAHARA KUTOKANA NA KAZI YENYEWE!
Serikali inaajiri wahitimu wote wanaomaliza vyuo, ambavyo kwa juhudi zilizofanyika pamoja na kutoa mikopo kwa kozi zote za education, wapo kibao! Kuwepo shule ni hatua moja, kuziboresha ni hatua nyingine, na Roma haikujengwa siku moja! Na serikali yetu inajitahidi saaana kusema kweli katika elimu. Hebu linganisha tuseme na 1995 tu!
ReplyDeletekwakweli namimi nakubaliana na mdau aliye toa ushauli huu ila ni wakati wa serikali kulifanyia kazi,mawazo kama haya ndo yanaitajika ili tuweze kusogeza taifa letu kwenye point ya mafanikio,nathani mda umefika wa kuipa kipau mbele elimu.asanteni.
ReplyDelete