Siku niliyosikia Yanga wanaanza mchakato wa kutafuta WIMBO YA YANGA nilifurahi sana nikajua kwa sasa mabadiliko ya kimawazo ya viongozi wetu wa klabu yanaanza kuonekana,kwa hilo naomba niwapongeze kwa hatua hiyo ambayo klabu yetu kongwe kwa miaka mingi ilishindwa kuwa na WIMBO YA YANGA.
Pia niwapongeze Clouds Media kwa kujitahidi kutangaza na kutoa msukumo kwa wadau wote katika kuitikia mwito huo wa Klabu katika harakati za kutafuta WIMBO WA YANGA.

Hadi sasa nimeweza kusikiliza Nyimbo zisizo pungua 4 kupitia Radio ya Clouds FM,kwa uwezo wangu “Mdogo” wa uchambuzi nimegundua kuwa nyimbo hizo zote zimetengenezwa si kwa madhumuni ya
Kuwa WIMBO WA YANGA bali wamefanikiwa kutengeneza NYIMBO ZA KUISHANGILIA YANGA.

Tuangalie mfano wa WIMBO wa MANCHESTER UNITED,wimbo umepangwa ukapangika,unatoa ujumbe uliokusudiwa,mawazo yalioko ndani yanaeleweka,lugha iliyotumika pia ni lugha rasmi.

Kati ya Nyimbo hizo nne(Nilizo sikiliza hadi sasa),huwezi kuyaona mambo tajwa hapo juu,WIMBO WA YANGA,huwezi kutumia lugha ambayo hata mpenzi wa Yanga haielewi,huwezi taja majina ya watu ovyo ovyo(kwa hakika hayahitajiki,wimbo ya Yanga inabidi uwe umepangika kimawazo na kimantiki,mtiririko wake ni lazima uwe unaotoa mawazo/ujumbe makini,wimbo inabidi uwe na mtundo unaoleweka na sio wa kuiga toka nyimbo fulani fulani maarufu za ulaya au Marekani.

Wito wangu kwa uongozi wa YANGA,ni kuwa makini sana katika mchakato huu ili kupata nyimbo bora.
Kwa watunzi wa Nyimbo,naomba mtambue YANGA inatafuta WIMBO YA YANGA(YANGA ANTHEM) na sio WIMBO YA KUISHANGILIA YANGA.
Asante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. NAKUNGA MKONO MDAU WIMBO USIWE WA KUSHANGILIA KWA MAANA WIMBO WA UNATEGEMEA MAZINGIRA YA WAKATI.1974TULIPO MPAKA SIMBA NYAMAGANA MASHABIKI YA YANGA TUKIONGOZWA NA MAREHEMU TOKYO(ALIKUWA DEREVA WA BASI LA YANGA)TULIWAPOKEA WACHEZAJI WETU NA WIMBO....UBINGWA...UBINGWA WA YANGA KAJA MARA GOLI 9,NTOMOKO GOLI 7.MIEMBENI GOLI 2....NA SIIIIMBA YALEYALEEEE!!!!!!!!!!!KAMA KUIMBA WANA MFATA MANGA NJENJE HUKU SEMBULI KATIA GOLI HIZO NI NYIMBO ZA KUSHANGILIA.

    ReplyDelete
  2. Mkuu tupo pamoja hapo juu angalia tune za mwimbo huu
    http://www.youtube.com/watch?v=bMvhIIBuxhg&feature=related

    ReplyDelete
  3. Suala la msingi ni: Je, hao viongozi wetu walikusudia wimbo wa namna gani? Naamini wanawapatia wasanii hadidu za rejea na si jambo la kufanyika kiholela holela tu.

    Pia mjue Simba ataiga ili ashindane na sisi, na atasubiri hadi ausikie wimbo wetu ndio atunge wake. Hivyo tafuteni wimbo usiofunikika, hatutaki kushindwa na Simba kwenye wimbo, bora hata tushindwe na Villa Squad!

    La msingi, Yanga ina mashabiki Africa mashariki na kati, hivyo wimbo utakaopitishwa uimbwe rasmi na wasanii wa kanda nzima. Kwa mfano, najua Fali Ipupa (DRC)ni Yanga damu, pia Nonini/Jua Kali (Kenya), Kidum (Burundi) na Jose Chamelion (Uganda). Hivyo msicheze ghalasha!

    ReplyDelete
  4. Pepe Kale alishatunga wimbo. imbeni huo.

    ReplyDelete
  5. Hakuna sababu ya kupoteza muda kwa vile Yanga ni timu ya Serikali na Chama, wimbo unaofanana na wa Taifa ndio unaofaa!

    ReplyDelete
  6. YANGA KUNA WATU MAKINI. MAONI YAKO YAMEFIKA NA YATAFANYIWA KZAI MDAU.

    ReplyDelete
  7. Bodi ya Yanga iunde kamati ya wanazuoni wa muziki ili watengeneze viwango na masharti ya kuzingatiwa.Vinginevyo tutabakia hapa hapa.

    ReplyDelete
  8. 'CCM! CCM! CCM!' Huo ndio wimbo wa Yanga.

    ReplyDelete
  9. Mdau hapo juu ametoa kali. Eti Fally Ipupa ni Yanga damu! Sitashangaa tukiambiwa humu kuwa Justin Bieber na Rihanna nao ni mashabiki wa Yanga.

    ReplyDelete
  10. No, Justin Bieber na Rihanna ni Villa Squad. Ila wengine kama Dr. Dre, Snoop, X, Ice Cube, 50 Cent (wagumu wagumu tu) ni Yanga pure!

    ReplyDelete
  11. Sasa Fally Ipupa mpaka poda ana ugumu gani?

    ReplyDelete
  12. Ahaa, Fally Ipupa huwa anawazuga tu 'mashoga', ila jamaa chuma cha pua!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...