Kwanza tunapenda kuwasalimu wakubwa Shikamoo na vijana wenzetu wote mambo vipi? Kwa Heshima na Taadhima timu nzima ya Matukio na wanavyuo tunapenda kuchukua nafasi hii ya Kipekee na kwa niaba ya Baraza la mitihani Tanzania kuweka hewani moja kwa moja matokeo ya kidato cha nne ambapo watahiniwa walifanya mitihani hiyo mwaka Jana 2011.
Hongera sana kwa wote walio fanya vizuri na kwa wale walio Feli tunawapa pole na wafanye bidii kurudia tena mitihani hiyo.


jamn watoto wamefeli sana kwakweli...cjaamini shule kama zanaki hakuna 1,11 eti 3 zipo 3 cjaamini
ReplyDeleteTunashukuru sana kwa taarifa.Kila mtu anabrowse humo sasa imekuwa balaa hata kufungua hiyo web ya Necta.
ReplyDeleteDavid V
Michuzi, Asante sana kwa kutujulisha. Nakumbuka wakati matokeo yangu ilipotangazwa... Nawapongeza wote ambao wamefaulu na wasio pass msikate tamaa! Direct link: http://www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm
ReplyDeleteNdugu AF.
Nakubaliana na mtoa maoni wa kwanza hapo juu.Nilishawahi kutoa maoni kwamba siku hizi siyo kama zamani,watoto wanafeli sana.Enzi zile shule zilikuwa zinashindana kutoa Division one(za ukweli siyo za kuiba mitihani)sasa hivi eti unaangalia matoke Div 1=0,Div 2=0,Div 3=1,Div 4=78,FLD=162 yaani ni vichekesho.Sikatai kufeli ile waliosoma hizi sekondari kuanzia miaka niseme 1990 kurudi huko nyuma watakubaliana na mimi.Kuna tofauti kubwa
ReplyDeleteDavid V
David V
watoto wenyewe ni bongo flavour.Wao shule wapi na wapi! watoto wa maskini ndio wenye kutia bidii, na wale ambao wazazi wana ushirikiani na mawazo ya maendeleo ya watoto.
ReplyDeleteMie siwapi pole walioshindwa.
Nimesikitika sana kwa matokeo mabaya kama haya, lakini ifike mahali tujiulize tatizo ni nini? Wizara ya elimu inapoona matokeo mabovu kama haya hasa katika shule za Serikali inaridhika nayo? Mimi nionavyo Wizara ijipange upya hasa kuhusu mitaala ambayo inabadilishwa kila kukicha, pia walimu wanaotoka vyuo vya ualimu kuwepo na utaratibu wa kuwaandaa vya kutosha, tukizingatia tupo katika jumuia ya Afrika Mashariki, wenzetu wametuacha sana!!!!
ReplyDeleteEnzi zetu matokeo hadi usubirie shuleni kwako baada ya wiki kadhaa...Au kama una ndugu/mshikaji Dar akakuangalizie Makongo...
ReplyDelete