Kwanza tunapenda kuwasalimu wakubwa Shikamoo na vijana wenzetu wote mambo vipi? Kwa Heshima na Taadhima timu nzima ya Matukio na wanavyuo tunapenda kuchukua nafasi hii ya Kipekee na kwa niaba ya Baraza la mitihani Tanzania kuweka hewani moja kwa moja matokeo ya kidato cha nne ambapo watahiniwa walifanya mitihani hiyo mwaka Jana 2011. 

Hongera sana kwa wote walio fanya vizuri na kwa wale walio Feli tunawapa pole na wafanye bidii kurudia tena mitihani hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. jamn watoto wamefeli sana kwakweli...cjaamini shule kama zanaki hakuna 1,11 eti 3 zipo 3 cjaamini

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru sana kwa taarifa.Kila mtu anabrowse humo sasa imekuwa balaa hata kufungua hiyo web ya Necta.

    David V

    ReplyDelete
  3. Michuzi, Asante sana kwa kutujulisha. Nakumbuka wakati matokeo yangu ilipotangazwa... Nawapongeza wote ambao wamefaulu na wasio pass msikate tamaa! Direct link: http://www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm

    Ndugu AF.

    ReplyDelete
  4. Nakubaliana na mtoa maoni wa kwanza hapo juu.Nilishawahi kutoa maoni kwamba siku hizi siyo kama zamani,watoto wanafeli sana.Enzi zile shule zilikuwa zinashindana kutoa Division one(za ukweli siyo za kuiba mitihani)sasa hivi eti unaangalia matoke Div 1=0,Div 2=0,Div 3=1,Div 4=78,FLD=162 yaani ni vichekesho.Sikatai kufeli ile waliosoma hizi sekondari kuanzia miaka niseme 1990 kurudi huko nyuma watakubaliana na mimi.Kuna tofauti kubwa

    David V

    David V

    ReplyDelete
  5. watoto wenyewe ni bongo flavour.Wao shule wapi na wapi! watoto wa maskini ndio wenye kutia bidii, na wale ambao wazazi wana ushirikiani na mawazo ya maendeleo ya watoto.

    Mie siwapi pole walioshindwa.

    ReplyDelete
  6. Nimesikitika sana kwa matokeo mabaya kama haya, lakini ifike mahali tujiulize tatizo ni nini? Wizara ya elimu inapoona matokeo mabovu kama haya hasa katika shule za Serikali inaridhika nayo? Mimi nionavyo Wizara ijipange upya hasa kuhusu mitaala ambayo inabadilishwa kila kukicha, pia walimu wanaotoka vyuo vya ualimu kuwepo na utaratibu wa kuwaandaa vya kutosha, tukizingatia tupo katika jumuia ya Afrika Mashariki, wenzetu wametuacha sana!!!!

    ReplyDelete
  7. Enzi zetu matokeo hadi usubirie shuleni kwako baada ya wiki kadhaa...Au kama una ndugu/mshikaji Dar akakuangalizie Makongo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...