Namshukuru sana mwenyenzi mungu (S.W.T) kwa kutufikisha siku ya leo tarehe 14/2/2012 (valentines day),ambapo leo tumetimiza miaka miwili ya ndoa na kujaaliwa watoto wawili,Lemmysa alizalliwa tarehe 25/9/2010 na bahati pia alizaliwa tarehe 5/12/2011.Hatuna cha kumlipa Mungu,bali ni kumshukuru na kumuomba atupe maisha marefu ya ndoa na niendelee kumpenda Mke wangu Zeenat milele na wanangu awape malezi mema na maisha marefu. Asanteni,Nawatakia Happy Valentines Day njema.
Bahati sigh.
Bahati sigh.
God bless this family, Happy Valentines to you. bll
ReplyDeleteDU HII KALI KILA MWAKA MTOTO, ??? HONGERA
ReplyDeleteNikiangalia hesabu ya hizo birthdays za watotot wako mmmmh! Inabidi muumwone mama Ushauri haraka.
ReplyDeleteNa mkeo akupende pia....Great familly
ReplyDeleteDuuh jamaa kiboko, kwa muda wa mwaka 1 na miezi miwili na nusu mmepata watoto wawili!! Hii speed ni kali mno.
ReplyDeleteMhn!.......COMMENT RESERVED!.
ReplyDeletehongerani kwa kutimiza miaka 2 ya ndoa, mmependeza kwa kweli
ReplyDeleteInapendeza sana tunawashukuru kwa kutukumbuka...sisi ndoa zetu ni vita kila kulicha. ndugu wa mume wamefanya ndoa yetu kuwa jehanamu.
ReplyDeleteKAKA umependeza sana na familia yako, ila kama wewe ni Muislam, valentine day ni haramu kusherehekea.
ReplyDeletekaka, nitakuwa sijaangalia vizuri au macho yangu yananiongopea? naona kama miaka 2 ya ndoa watoto 2! mbona kama mmekwenda haraka? mtoto anatakiwa anyonye at least miaka 2 kamili halafu jitihada za kutafuta mdogo wake ndio zinaanza, hongera!
ReplyDeletemiaka miwili ya ndoa ,watoto wawili!!!!!???? kali lakini hongera!
ReplyDeleteInsha'Allah Mwenyezi Mungu akukuzieni watoto wenu na wawe kizazi bora,,na mja'aliwe kuongezewa tena wengine wawili waje kucheza na hao wenzao
ReplyDeleteMimi nimewapendaje!jamani Nice couple!mwanzo juzi niliwaona katika 8020fashion nikamuuliza sister wangu aangalie mlivyotoka vizuri katika picha,,
Duah yenu Mola akupokeleeni,,na sisi pia!
Ahlam,,,UK
inamaana huyo wa kwanza ulimzaa kwa miezi saba au uliibeba kabla ya ndoa.
ReplyDeleteKama wewe ni muislam, basi valentain sio desturi ya waislam ni mila za makadiyani.
Inshallah AMIIIIIN,
ReplyDeleteMwenyezi Mungu atawajaalia!
Cha msingi katika Uzazi ni afya bora ya watoto na sio hatua au muda kati ya mtoto anayefuata aliyemtangulia kuzaliwa.
Katika picha hapo Wadau mnaona wenyewe watoto wote wawili wapo bukheri wa afya na hakuna dalili zozote za hitilafu ya kiafya kwa watoto.
SASA KWA TAARIFA YENU HUU NDIO UZAZI WENYE TIJA!
Lovely family! like that endeleeni hivyo hivyo msiache gap mpaka mmalize mliopanga kazi ibaki kulea sio mtu anakaa miaka kibao ndo anawaza tena jinsi y akufunga nepi that one is marvelous.
ReplyDeleteMungu awajalie maisha yenye furaha na amani.
jamani hongereni sana,pia kama wazazi wa kisasa au wasomi,tumieni uzazi wa majira msiwe kama watu ambao hawajachungulia shule kabisa.
ReplyDeletemmependeza sana, Bahati naona kama umevaa chain ya dhahabu, kama ni kweli mwannaume sio vizuri kuvaa. Vaa silva na mama mnunulie dhahabu za kutosha.
ReplyDelete