Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Sazi Salula akifungua Mkutano wa Tano wa Wataalamu wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika unaoshirikisha Nchi Nne za Tanzania,Zambia,Congo na Burund. mkutano huo unfanyika kwenye Hotel ya Tanganyika Mkoani Kigoma.Picha na Ali Meja.

Na Lulu Mussa-Kigoma

Mkutano wa tano wa Mamlaka ya ziwa Tanganyika unafanyika Mkoani Kigoma kwa lengo la kuweka mikakati madhubuti ya kunusuru Ziwa Tanganyika.

Awali akifungua mkutano wa wataalamu hao, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Sazi Salula amesema Ziwa Tanganyika ni chanzo kikubwa cha kukuza uchumi katika nchi zinazozunguka ziwa hilo.

Hata hivyo, Ziwa hilo linakabiliwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira ikiwa ni pamoja na kujaa kwa taka za majumbani na zile za viwandani, uvuvi haramu kutokana na ongezeko la watu, kilimo na ufugaji usio endelevu.
Hivyo, Bw. Salula ametoa wito kwa wataalamu hao kufanya kazi kwa pamoja katika kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo kwa maendeleo endelevu ya ziwa Tanganyika. “Ni vema kuwa na mjadala wa kina kujadili changamoto hizo na kutafuta suluhu za kukabiliana na uharibifu huo wa mazingira” alisisitiza Bw. Salula

Mkutano wa tano wa Mamlaka ya ziwa Tanganyika unakutana kwa siku mbili kujadili taarifa za utekelezaji na kutayarisha mpango mkakati wa kitaifa. Mkutano huo utafuatiwa na Mkutano wa tano wa Mawaziri wa Mamlaka ya Ziwa Tanganyika, utakaofanyika katika Hotel ya Lake Tanganyika, mkoani Kigoma.

Mamlaka hiyo ya Ziwa Tanganyika inaundwa na nchi za Zambia, Burundi, Congo (DRC) na mwenyeji Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. 100% confidence levelFebruary 26, 2012

    Congratulation for the work done to preserve our environments water bodies inclusive.My advice is that,the efforts should also be directed to preserve all lakes in the country especially those which provide the community with aquatic natural products.(fishery activities)to make these aquatic products be sustainable harvested.eg like victoria etc.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...