Wadau, mimi ni mwanafunzi nipo Uingereza na ninasoma shahada ya uzamili ya Uongozi na Biashara [ Master of Business Administration (MBA or M.B.A.) ], na ninategemea kumaliza course work Nov 2012, na Dissertation mnamo March 2013.

Katika kufikia  ndoto zangu za kumaliza hii kozi, pamoja na mambo mengine ni pamoja na ulipaji wa ada, ambayo inaniwia vigumu kwa sasa kwani upatikanaji wa kazi ni mgumu.

Hivyo basi imenibidi nifikirie chanzo kingine cha fedha, ombi langu hapa ni kwa yeyote anayefahamu any financial  firm huko nyumbani ambapo ninaweza kukopa, ninahitaji £2000 (5,200,000/=)ili niendelee na masomo bila wasiwasi na bughudha ya kusimamishwa.

Kwa firm yeyote itakayoweza kunikopesha nitakuwa na uwezo wa kulipa kwa mwezi around 350,000/=.Ahsanteni naomba muandike hapa hapa kwenye blog au pia unaweza kuniandikia kwa kutumia email: bemk28@yahoo.co.uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Pole sana ndugu yangu.jitahidi uwasiliane na Haruna Mbeyu maarufu kama Meya wa London.Atakupa mwongozo.Nami nitakutumia email yangu.
    Latifah Uk.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa MBA suala lako ufumbuzi umo humu humu katika Blogu yetu ya Jamii wasiliana na WEZESHWA kwa namba 0763600041.

    Katika Matangazo ya Blogu tangazo la 7 kutoka juu utawaona ingawa wapo kibiashara zaidi unaweza wasiliana nao wakaangalia ni vipi watakuwezesha.

    Isipokuwa matatizo makubwa kwa ninyi wa Majuu ni Dhamana kwa vile akili zenu ziko na matarajio zaidi ya maisha ya huko kitu ambacho inakuwa vigumu kuaminiwa Mikopo na Taasisi za huku Bongo kwa vile inaonekana ukisha kopa ukafikia lengo halafu hurudi Bongo au kukwepa kulipa Deni la Mkopo.

    ReplyDelete
  3. Kaka, mbona hujaandika uko college gani ili tukusaidie kwa wepesi? isijekuwa mabo ya wanaijeria tena hapa.

    ReplyDelete
  4. Jamani, mbona hizo course zipo hapa Nchini? mpaka uende huko mbali na uwezo hauna ndugu yangu! Bank za Tanzania wakikukopesha ujue utalipa mara 3 ya hiyo amount.

    ReplyDelete
  5. kwanza itabidi uwe na collateral, na pia uwepo mwenyewe physically. Vinginevyo uwe na mtu wa kukuchukulia mkopo kwa jina lake na collateral yake. Kwa situation yako, its a bit tricky. Riba huku ni kubwa, up to 30%, which means itabidi ulipe 1.5m kila mwezi. hata ukipata ya riba ya 10%, bado utalipa laki tano kila mwezi. Lifikirie upya hili

    ReplyDelete
  6. Dr. KungumileFebruary 14, 2012

    Achana na mikopo ndugu yangu. Itakupotezea muda. Chukua visa ya ubatani nenda istanbul, chukua vyombo peleka kwa mama, uza lipa ada, piga shule.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kabisa kutaka kumpotosha kijana wa watu..yeye yake shule sio mambo hayo

      Delete
  7. rudi bongo wewe .....unatafuta hiyo hela wanakutumia cheti ...wabong kukopesha shughuli afu mtu akukope we uko uk

    ReplyDelete
  8. Mbona unahangaika na kitu kidogo sana kama hicho ? Nenda bank kachukue mkopo uendelee na masomo.Au rudi tz utafute mkopo kwenye mabank ya home kama unaona huko bank zitakutalia.Otherwise rudi usome bongo kwani course kama hiyo ni less than hiyo 5.2m na hutakuwa na stress yoyote ukiwa nyumbani. Pia home wadhamini kama unataka kuchukua mkopo ni wengi ukilinganisha na huko. Masomo mema.

    ReplyDelete
  9. £4000 zingekutosha kusoma kozi yote Malaysia. Badala ya kuwapa faida waingereza.

    ReplyDelete
  10. MAELEZO YAKO HAYATOSHELEZI ISIWE UNATAKA KUTAPELI KWA NJIA YA KUWA UNASOMA.

    ReplyDelete
  11. Mdau pole.
    hilo ni wazo zuri, kwani hata ma firm hayo ukwama wakati mwingne na kuomba kusaidiwa na benki, na benki hukwama na kusaidiwa na serikali kwa hela ya walipa kodi.
    sasa kiasi hicho sio kikubwa kwa walio ughaibuni kama wewe. kwa hiyo rekebisha ombi lako ili ujumuishe na watu binafsi wao weza kukusaidia na ukalpa ukirudi. mfano kama unamjua mwansheria bongo anayeweza kuandika barua ya mkataba, au waliopo UK. Ni vizuri usema kama hela unahitaji yote kwa mkupuo na ni lini au unataka nusu na nusu, yote inawezekana.
    naweza kusaidia kuanzia mwezi wa sita kiasi chote na ukarudisha ukishamaliza shule tena kwa chini ya hiyo laki tatu unusu uliyosema, kwani hauombi pesa ya maraha, ila ni elimu ambayo sio tu itasaidia familia yako lakini pia taifa(utalip kodi, utato utumishi kwa umaa nk). an kutaki ala heri ufanikiwe na kama utaweka watu binafis wakudhamini, naweza kujitokeza kwa sababu kiasi kidogo hicho n awewe unataka kusoma.

    ReplyDelete
  12. Mmmh?hiii ni challenge..kusoma kwa mawazo ya Ada ni ngumu.vp huko vibarua vya kubeba box hamna?nduguzo je hawawez jikusanya kusanya kama tunavyochangiaga harus bajiet milioni 20?!!!inawezekana ukachangiwa hizo mil tano ..Na je ukikopeshwa utaweka security gan??

    ReplyDelete
  13. Kwa nini usijaribu kwenda katika ubalozi wa tanzania ili uongee nao waweze kukutafutia sehemu ya kupata mkopo nyumbani,,mimi naona hiyo ingekusaidia sana ukiwapelekea na vyeti vyako vya utambulisho kuwa unasoma kweli hapo,,kazi kumbwa nyingine ya kibalozi ni kuangalia watu kama nyinyi,,jamani msaada huwo unahitajika haraka ili asipoteze masomo yake huyo kaka,,,sijuini dada!,,nakutakia kila la Kheri
    Ahlam,,,Uk

    ReplyDelete
  14. Nani wa kukukopesha hela!.Rudi tu bongo.

    ReplyDelete
  15. Nani wa kukukopesha hela!.Rudi tu bongo.

    ReplyDelete
  16. Ebana kaka pole sana najua unachopitia. Mwenzio nilikua na deni la pauni 8000 nimepangua lote na saivi nimegraduate niko street napiga boksi. Nakushauri utafute rafiki au ndugu wa kitanzania umuulize wapi unaweza kukopa kwa mtu ukalipa kwa riba kidogo hiyo ni bora kuliko kuleta humu kwenye hili jukwaa wengi ni waosha vinywa tu hawana msaada wamekaa kulaumu tu na sio kutoa solution. Usikate tamaa mwana komaa tu utatoka hiyo 2000 sio kitu wengine tumekamua mara nne yake sa ivi freeshi!!

    ReplyDelete
  17. Wadau Suala la Hadhi ya Elimu ndio sera ya sababu kwa nini ameamua kusoma Uingereza.

    Mtambue kuwa Viwango vya Elimu vinatofautiana kati ya nchi na nchi hadi chuo na chuo.

    Hapa hapa nyumbani vyuo nina hadhi tofauti kwa ulinganisho na ndio maana hata ile 'Admission Copmetition'' ina tofautiana kulingana na hadhi ya chuo.

    Sasa mfano Degree ya OXFORD UNIVERSITY, CAMBRIDGE UNIVERSITY, au LONDON SCHOOL OF ECONOMICS, ni tofauti na Degree kutoka UNIVERSITY OF CHAMBERLAIN huko Uswazi ya UK,,,pia hapa Bongo Degree ya UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM zipo mbali maguu kibao tofauti na Degree ya ECKENFORDE UNIVERISTY...Ndio maana Mdau amepanda ndege kwenda kusoma UK mpo hapo?

    ReplyDelete
  18. MBONA UK KUNA MIKOPO KIBAO NJE NJE TU. INAJULIKANA KAMA LOAN SHARK KAMA UMEKOSA MKOPO TOKA KWENYE BENKI YAKO.
    HALAFU UNATAKA £2000 MDAU KWA KOZI GANI UNAYOSOMEA WAKATI WENYEJI WENYEWE MWAKA HUU WANATAKIWA KULIPA UP £9000 NA WATOTO HAWAENDI UNI. WAZAZI HAWANA HELA!!! UKATA.
    WEWE UNAOMBA HELA HUWEKI PICHA YAKO WATU WAKAKUJUA KAMA KWELI NDIYE WEWE AU HEWA. PENGINE ULISHAWAHI KUKOPA SEHEMU NA HUJARUDISHA KWA HIYO AMANA YAKO NI PICHA HAPA BWANAAAA HUTUELEZI KITU WEWE MAANDAZI CHAI KWA MAHARAGE MAINI YA SUKARI!
    KAMA UNAWEZA KULIPA 350K/M, MBONA NYINGI SANA HIZO KWA MKOPO WA 2000. MIMI NIMELAMBA 5000 BANKI NA NINALIPA 80 QUID KWA MWEZI. WEWE UNATAKA KULIPA ZAIDI PAUNDI 100.

    WEKA PICHA HAPA.

    ReplyDelete
  19. Inawezekana Mdau Msomi amepiga Box huko UK sasa amechemka anawageukia Wandugu avute chache (£££) kiasi cha mboga ili apumzike kidogo,,,muelewe mkubwa akizidiwa na mzigo kati kati ya Msafara wa safari ndefu, hawezi kulia mtamcheka, huaga kwenda kujisaidia kidogo kichakani!,,,baridi ni kali na kifua kimembana kwa Mizigo!

    ReplyDelete
  20. Wandugu Msomi ameelemewa na Ma BOX mgongoni hadi ameota sugu sasa, amewapiga bomu kidogo (kwa njia ya usanii kuwa anasoma) ili apozee apumzike kupisha Majira ya Baridi la Ulaya.

    nataka ajifungie ndani angalau siku mbili tatu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...