Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya shs Bilioni moja kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya mahususi ya kutafuta fedha na kutoa mikopo ya muda mrefu ya nyumba (TMRC), Rished Bade ikiwa ni kiasi cha kununua hisa za asilimia 10.87 ndani ya TMRC. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari akiweka sawa baadhi ya mambo katika tukio hilo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru na CEO wa TMRC, Rished Bade.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Rished Bade akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru (kushoto, walioketi) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni mahususi ya kutafuta fedha na kutoa mikopo ya muda mrefu ya nyumba (TMRC), Rished Bade (kushoto kwake) wakiwa pamoja na baadhi ya maofia wa TMRC na wa benki hiyo katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. huyu Rished Bade ana akili sijapata kuona maishani mwangu. kila shule aliyopita alikuwa akiongoza mpaka kufika chuo kikuu.

    ReplyDelete
  2. Alikuwa akiongoza kwenye Masomo gani?"Historia,Jiografia,Kiswahili na Kiingereza au Fizikia,Kemia,Baiolojia na Hisabati au yote??

    David V

    ReplyDelete
  3. ila hana akili ya maisha alioa mke wa mtu! akiwa chuo, sijui ameishia wapi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...