MBUNGE wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), amesema kati ya uamuzi wa makosa uliowahi kuchukuliwa na Serikali ya chama chake cha CCM, ni kuuza nyumba za umma hivyo akataka zirejeshwe Serikalini mara moja vinginevyo atawasilisha hoja binafsi Bungeni.
Hii sio mara ya kwanza kwa wabunge kuhoji kuuzwa kwa nyumba za serikali wakitishia kutoa hoja binafsi bungeni kutaka mchakato huo ukome.
Aprili 5 mwaka 2008 aliyekuwa mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), alitishia kutoa hoja binafsi bungeni kutaka watu ambao si wafanyakazi wa serikali ambao wameuziwa nyumba za serikali wanyang'anywe nyumba hizo.
Na jana Ole Sendeka aliibua tena hoja hiyo alipokuwa akichangia hoja binafsi iliyowasilishwa na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (CCM), akitaka Serikali kutunga sheria ya kudhibiti wa shughuli za upangaji nyumba za makazi.
Sendeka alisema kutokuwapo kwa sera ya nyumba kumesababisha waliokuwa na madaraka kugawana nyumba za Serikali kama chakula cha njaa na kwamba, kama kuna sehemu Serikali ya chama chake ilifanya makosa ni uamuzi huo.
“Nataraji kuja na hoja ya kulitaka Bunge liamuru nyumba hizo zirudishwe… napingana na Waziri (John) Magufuli aliposema waliovunja mkataba wamenyang’anywa nyumba, siyo kweli,” alisema Sendeka na kuongeza:
“Nina ushahidi hata wale waliopata kwa sababu ya undugu wa waliokuwa na madaraka bado hawajarejesha.”
Awali, akiwasilisha hoja hiyo, Makamba alisema inatakiwa kutungwa sheria ya kudhibiti shughuli za upangaji nyumba za makazi kwa sababu, sheria iliyokuwa ikiwalinda ilifutwa mwaka 2005, ambayo ilikuwa inatoa ulinzi kwa wanyonge ambao ni wapangaji.
“Nchi nyingi za kibepari ikiwamo Kenya, zina Sheria za Kudhibiti Pango ambapo chini ya Sheria namba 296 ni makosa kudai pango la zaidi ya miezi miwili, na Uganda, chini ya Sheria yao namba 231,” alisema Makamba.
Makamba alisema katika mageuzi ya uchumi zimeundwa taasisi nyingi zinazdhibiti bei za bidhaa mbalimbali, huku akitoa mfano wa Sumatra, Ewura na TCRA.
Alisema kama inaonekana ni sahihi kuweka udhibiti kampuni za simu za mikononi zisipandishe bei holela, lazima kuwapo kwa udhibiti wa hitaji muhimu la maisha ya mwanadamu, ili mmiliki wa nyumba asipandishe kodi holela kwa kiwango cha wakati wowote.
“Vilevile, ni muhimu nikaweka wazi kwamba sheria ninayopendekeza siyo sheria ya kuwakandamiza wenye nyumba. Sheria itakayolinda maslahi ya wote; kwani ni dhahiri kabisa wapo wapangaji ambao nao hawatimizi wajibu wao,” alisema.
Mbunge huyo alisema sheria ya hivi sasa mmiliki wa nyumba hana haja ya kwenda mahakamani kupata haki yake ya kimkataba, anaweza kuuza kitu chochote cha mpangaji, lakini mpangaji ili apate haki yake lazima aende mahakamani ambako kuna mlolongo mrefu.
Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), alisema Serikali haijatambua kuwa sekta ya makazi ni chanzo kikubwa cha mapato na kutoa mfano wa Dubai inayopata zaidi ya asilimia 20 ya mapato yake kutoka sekta ya makazi, huku mafuta yakichangia asilimia sita.
“Kuna mapato makubwa kwenye hii sekta, lakini hakuna kinachokusanywa ndiyo maana hakuna sera ya nyumba miaka 50 tangu tupate uhuru,” alisema Mbowe.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alisema hoja hiyo ni muhimu na kwamba, kabla ya kutengeneza sheria inahitajika kuundwa sera ya nyumba ambayo hadi sasa haipo.
Profesa Tibaijuka alikiri tabia iliyoanzishwa na wamiliki wa nyumba kutaka kulipwa kodi ya pango kwa miezi sita au mwaka mmoja, ni kinyume na viwango vya kimataifa kuhusu makazi na kuomba Serikali ipewe muda kuifanyia kazi hoja hiyo.
Historia ya nyumba za serikali
Nyumba za watumishi wa serikali zilianza kujengwa na watawala wa Kijerumani na Waingereza. nyumba hizo ambazo sasa idadi yake inakadiriwa kufikia 10,000 ziko za daraja la tatu, pili na kwanza kulingana na nyadhifa za watumishi wa serikali.
Nyumba hizo zimejengwa maeneo mbalimbali ya nchi ikiwamo katika jiji la Dar es Salaam ambako nyumba mashuhuri ni zile zilizoko maeneo ya Upanga na Oysterbay.
Lengo kubwa la nyumba hizo ni kurahisisha usafiri kwa wafanyakaziwa serikali na kuwaondolea kero ya makazi, gharama za kuwalipia kodi za kupanga na kuwavutia wafanyakazi ili wafikie ufanisi kiutendaji.
Wazo la kuziuza nyumba hizo lilianza katika utawala wa serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa ambaye baada ya mwenyewe kuchukulia nyumba iliyoko Sea View jijini Dar es Salaam, zingine zikaanza kuuzwa kwa mawaziri, majaji, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa jeshi, polisi na magereza.
Sababu za kuuza nyumba hizo
Sababu za kuuza nyumba hizo hazikuwekwa bayana. Wakati maelezo mengine yanasema kuwa hatua hiyo imefikiwa kuwasaidia watumishi wa serikali kuwa na nyumba, mengine yanasema nyumba hizo ziliuzwa kwa kuwa ni mzigo kwa serikali. (Chanzo;Gazeti la Mwananchi)
Kwa kweli awamu ya tatu ilisababisha maafa makubwa lkn. kama wanavyosema waswahili "ukimpenda mtu, hata kama ana chongo utasema ana kengeza"
ReplyDeleteWatz. kwa makusudi kupitia vyombo vya habari wameamua kuipaka matope awamu ya nne. na kusahau yale yote yaliyotokea kabla.
Ununuzi wa rada, mikataba ya madini, uuzwaji wa nyumba za serikali, watu kuuwawa ktk. harakati za kisiasa na mengi mengine.
leo hii 'vipofu' wanadai hawajawahi kuona awamu mbaya kama hii ktk historia ya nchi yetu..sijui wanazungumzia nchi yao ipi, manake hapa pana wageni wengi wanaojiita raia!
Makubwa!! Baada ya Mkulu mwenyewe kujichukulia nyumba sea view!
ReplyDeleteHata hivyo, wabunge kama wewe Sendeka, si mlikuwepo wakati uporaji huo unafanyika? Shughuli ya kuwanyang'anya watu waliojigawia nyumba hizo 'kihalali' sio ndogo! Inahitaji Diktator kama Idd Amin hivi, ambaye hatuna! Vinginevyo italeta ufisadi mwingine tena, maana hao itabidi walipwe mabilioni ya fedha kama fidia!
Isiwe kwa Dr.Blandina Nyoni na Mtasiwa tu hata hao waliouza hizo nyumba watafutwe,wawajibike,wanafahamika.Tukiacha kuoneana aibu Tanzania baada ya Miaka 20 itakuwa imesogea hatua kadhaa mbele.Na hasa yule aliyeanzisha hilo wazo la kuuza hizo nyumba.Nyumba zirudishwe mara moja.
ReplyDeleteDavid V
Uuzaji wa Majumba ya Serikali:
ReplyDeleteHii ilikuwa ni Sera ya Wana CCM wachache wenye malengo ya Ubinafsi ambao ni hatari sana kwa Hatma ya Nchi yetu!
Bomoa ,Bomaa ehh, Bomoa mama tutajenga kesho ,Imamaa!
ReplyDeleteTutajenga kesho ,we Imamaa!
KUSEMA KWELI AWAMU YA TATU NDIYO ILIYONIFANYA MIMI NIIONE ILE NCHI NI KUTI KAVU. NIMEKIMBIA NCHI MIMI KWA ILE KHALI ILIYOKUWEPO KILA KITU KILIBADILIKA.
ReplyDeleteNakubaliana na mtoaji mada wa kwanza hapo juu. Nafikiri hatumtendei haki JK na awamu zake katika uongozi. Maskini hajaua, hajamkaripia wala kumdhulumu mtanzania binafsi. "I like his Personality, Interpersonal Character and his "wait a bit and see model of leadership so far".
ReplyDeleteMapungufu kwa binaadamu yapo, ila ya kwake, hayazidi yaliyofanywa na maraisi waliopita
kuhusu ufisadi wake mpaka hivi sasa binafsi sina data zozote zile bado.
Labda ninachoweza kumlaumu ni jinsi alivyothubutu, kujaribu na hatimaye kuyumbishwa namna ya kuyashughulikia yale MACHAFU aliyomuachia Chimkapa; ambayo yamemshinda kuyakabili maana ni mengi mno kama mlivyoona hiyo list hapo juu, ijapokuwa mdau naye alisahau uuzwaji wa benki yetu ya Taifa kwa makaburu (nasikia kulia haki ya MUNGU).
Kosa ambalo ningempa JK nikutokujipanga vizuri mwanzo wa utawala wake kushughulikia UOZO aliomuachia Chimkapa. otherwise, bado ni kipenzi tu cha Taifa. kuhusu nyumba za serikali, yes, ingetakiwa zirudi kimtindo na kama ni kuuzwa ziuzwe kwa utaratibu usio na ufisadi. "ila kuna riski kubwa ya kufanya hivyo", ni bora tukafikiria kuirudisha benki ya Taifa mikononi mwa Wananchi wa kitanzania na serikali yao na kuwanyang'anya mafisadi ambao tunawajua mali zetu (including migodi iliyouzwa bila utaratibu).
Mkapa, kama raia wa Tanzania, akae akijua kuwa Watanzania tunamdai, yeye na kizazi chake, leo, kesho na hata milele.aliyowafanyia wa-bongo si ubinaadamu ijapokuwa anaenda kanisani.
Nimewakilisha tu
la nakumbuka marehemu baba yangu alikuwa serikalini, akiishi mtaa wa kaunda oysterbay alitumikia taifa zaidi ya miaka 40 kwa uaminifu alipokufa hakuwa hata na kibanda, alikuja tolewa kwenye nyumba ya serikali kama mbwa baada ya mwaka mmoja aliehamia pale aliuziwa hiyo nyumba na hakuwa mtumishi wa serikali ila mtu mwenye mapesa na ana nyumba nyingine nyingi alizonunua kimtindo huo
ReplyDeleteMichuzi sisi tuko huku porini tunaomba matokeo ya Manchester na Liverpool
ReplyDeleteMdau wa Blog ya Jamii
..huu ni upuuzi, hiyo issue ilishapita.. Watu wengi waliochukua hizo nyumba walizibomoa na kujenga zao yale yalikuwa magofu.
ReplyDeleteDu!! Ukiona hivyo Sendebuka naye analilia kutulizwa maana dili mpeto lilipopita alikuwa bado muumini swaaafi wa" zidumu fikra sahihi" lakini nikimuangalia leo mmmmh!7
ReplyDeleteMichuzi tupe habari za Bwawa la maini bwana mbona kimya?
ReplyDeletewadau wanaotaka matokeo ya mechi za epl, wangepata ive commentary toka ot kwenye yaho sport, bbc sport you name it.
ReplyDeletemambo ya karne za kina jongo, hillary, kitojo kwenda cairo, lagos na kupata matokeo ya mechi ya jana leo, yamepitwa na wakati.
sasa michuzi aweke matokeo wakati anajua fika watu kibao wanafuatilia kila kona. mobile internet, internt cafe, LUNINGA, sijui niseme nini. UVIVU NA LACK OF KNOWLEDGE
Jamaa alinyimwa nini ndo maana anazitolea macho. Zimeshauzwa watu wamejigawia kibao kama kina mama Sitta na mumewe kila mtu ana yake maeneo ya Oysterbay mtaa wa Bongoyo sa unafkiri zitarudishwa hizo. Wa kumtimua ni Rostam anayekaa nyumba iliyokua ya Serikali pale pembeni ya switch ya Voda na wakati hajawahi kufanya kazi serikalini.
ReplyDeleteIngekuwa inawezekana basi tungemuomba Raisi JK aendelee kwa miaka kumi mingine ili arekebishe mambo mengi ambayo yameachwa na uchafu.Kwakweli tunampa pongezi Raisi wetu na wenye kumchukia ni wale wenyekufaidika na mafisadi kwa upande wa kushoto.Wanamchukia kwasababu amewadhibiti kwa kiasi fulani japokuwa nanihii hawampi upenyo lakini angewakomesha.JK tunaomba tuletee katiba nzuri itakayomlinda mwananchi kwa viongozi mafisadi.
ReplyDeletesio za serikali tu hata za TTCL zote zimezama na kuna watu walichukua 2,3,hata 5..wana uhusiano na serikali ya awmu ya tatu...
ReplyDeletetatizo moja tulilokuwa nalo cc watanzania hasa viongozi wa serikali ni kwamba siku hizi watu wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi kwa familia zao na ndugu zao lakini kazi kwa umma lahasha hakuna kiongozi yeyote anayefanya kazi kwa maslahi ya umma wengine ni wanapretend kwa kujifanya wanafanya kwa maslahi ya taifa ngoja wapewe nafasi na wenyewe wanaanza ufisadi.
ReplyDeleteMm cntomsahau marehemu sokoine hakika tungepata watu kama sokoine wattano tu viongozi wa juu taifa letu lingeendelea sana kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata kiteknolojia.
Nawasilisha wadau.
baba yangu mimi pia hapo sea view alikuwa mkubwa wa serekali naanasiri nyingi za serekali yetu ni yule wa enzi za nyerere,lakini aliondolewa kwenye nyuma ya serekali kama mbwa hapo sea view.
ReplyDeleteMIMI SHAURI LA UUZAJI WA NYUMBA ZA SERIKALI LINANIKERA KAMA MSIBA WA TAIFA.
ReplyDeleteHATA LIJE JUA NA MVUA IKANYESHA. HATA SENDEKA ATOWEKE BADO TUTAZIDAI NYUMBA HIZI KWA NGUVU TU.
HILI NI DENI KWA CHAMA/SERIKALI YANGU.
MAINA OWINO.
CCM UK
kinacho niuma mimi baba yangu hameishi oysterbay kwa miaka mtaa wa msasani road na hamelitumikia taifa kwa moyo wote bila wizi bali kumuhudumia raia wa nchi kwa moyo muda ulipofika mkapa hata kumuhuliza kama hanataka nyumba no bali wakina nanihii ndio walipewa hiyo nafasi na mawazili walio tumikia nchi kwa mwaka kupiyia ubunge hambao walikua sio wafanyakazi wa taifa before bali ni nanihii ndio wakapewa nafasi wakati mzee wangu kafanya TRAnatulikula ugali mpaka tulichoka na alikua na uwezo wa kuchukua mamilioni hapo TRA kwa nafasi yake mungu mlaze pema peponi kwa uhaminifu wakena mkapa hakajibu hayo maswali huko mbeleni
ReplyDeleteserikali ina uwezo wa kurudisha hizo nyumba kama wanataka wala hakuna tatizo lolote
ReplyDeleteNyumba za obay ni msala tena,watu wane invest sn leo kila nyumba inathamani kubwa kuwatoa hiyo pesa si bora kujenga nyumba Mpya tu
ReplyDeleteHongera mzee
ReplyDelete