Ankal Salamaleko!


Nimerudi tena baada ya kimya kingi kilichotokana na kuzidiwa na maboxi huku niliko. Na kabla ya yote niruhusu nikupigie saluti kwa kuendeleza Libeneke letu kila siku kama huna akili nzuri vile. Unastahili pongezi wallahi!


Mie swali langu kwa wadau wa Blogu hii ni hili neno la king'eng'e la SOCIALIZING. Yaani  naomba nifahamishwe kinagaubaga kama ni lugha gongana ama nimepatia ninaposema socializing ni kujamiiana. Kwa maana ingine naomba kutafsiriwa kwa kimatumbi nikitaka kusema socializing nisemeje??


Naomba kuwasilisha.


Mdau Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. SOCIALIZING NI KUJICHANGANYA.NO DEFINITION ZAIDI YA HII!!!CHEERS MBEMA MADAFU UGHAIBUNI!!

    ReplyDelete
  2. kujichanganya na watu/jamii au kujumuika

    ReplyDelete
  3. Mdau.
    Kwa ufupi, kujamiiana ni kufanya kitendo cha ngono. Sio sahihi kulitumia neno hili ukitafsiri "socializing".
    Neno lenye tafsiri ya socializing ni:-
    KUJUANA.....hapo ndipo mnapo socialize.
    Sawa mkubwa?

    ReplyDelete
  4. Mdau.
    Kwa ufupi, kujamiiana ni kufanya kitendo cha ngono. Sio sahihi kulitumia neno hili ukitafsiri "socializing".
    Neno lenye tafsiri ya socializing ni:-
    KUJUANA.....hapo ndipo mnapo socialize.
    Sawa mkubwa?

    ReplyDelete
  5. Siku ukikua utajiona mjinga sana.

    ReplyDelete
  6. socializing sio kujamiiana wewe. Kujamiiana ni matusi. Socializing linatokana na neno Social = kijamii kwa hiyo socializing ni kukutana kijamii iwe kwa mazungumzo, kinywaji, sherehere etc.

    ReplyDelete
  7. kuingiliana ila naweza kusema kujichanganya..

    ReplyDelete
  8. Mdau hujakosea hiyo ndio maana yake halisi,ila wabongo akili itawapeleka kwingine

    ReplyDelete
  9. KUJICHANGANYA ipo poa kabisa

    ReplyDelete
  10. Kuna baadhi ya maneo ya Kiingereza hayawezi kutafsiriwa moja kwa moja, kama wewe unavyofikiri, lazima yabadilishwe kidogo ili kuendana na muktadha. Mfano, Waingereza cherehani wanaita 'Sewing Machine', sisi katuiti mashine ya kushonea. Nadhani umenielewa 'SOCIALIZE' ni 'JUMUIKA'

    ReplyDelete
  11. Mnhhh zaidi imekaa 'kingono'!

    ReplyDelete
  12. Michuzi vipi? Mbona hupost majibu yangu??
    Kunani???
    Anyway, kwa mara nyingine:-
    Kujamiiana ni kuingiliana kimwili.... yaani tendo la unyumba.
    Socialising kwa mtazamo wangu ni KUJUANA.
    Unapo socialise ni kupata fursa ya kujuana...
    Sawa wadau?
    KwaMtoro.

    ReplyDelete
  13. ni kujichanganya na wenzie katika mambo mbali mbali yakiwemo kutoka kwenda out na mengineyo.

    ReplyDelete
  14. Daaah! We mdau kiboko. Haya jaribu neno kujumuika.

    ReplyDelete
  15. kustareheeeeeeeee

    ReplyDelete
  16. kujirusha na wenzio

    ReplyDelete
  17. KUJICHANGANYA

    ReplyDelete
  18. Kuna watu wametaja Kujumuika,kujichanganya,Nadhani wako sawa.Halina uhusiano na kujamiiana wala kufanya mapnz

    ReplyDelete
  19. duh babu lugha ya watu sio lazima kuijua ukijua yakotosha mzee

    ReplyDelete
  20. Nafikiri kujichanganya ina make sense, hili neno lipo sana kwenye somo la sociology na psychology kwa wanaosomea hayo masomo.

    ReplyDelete
  21. Kujichanganya sio sahihi hapa.
    Ina maanisha to confuse or to have conflicting ideas. Hapo ndio mtu ana jichanganya.
    Na angalia tofauti ya maana ya haya maneno:-
    "kuJIchanganya" to get mixed up or get confused sio sawa na "kuchanganya" i.e to mix, specifically things, items etc..

    Hiki ni kipindi cha zaidi ya dak 40, kukifupisha katika sentensi tatu ni rahisi kuchanganyikiwa!!
    Upo mdau?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...