Ankal Salamaleko!
Nimerudi tena baada ya kimya kingi kilichotokana na kuzidiwa na maboxi huku niliko. Na kabla ya yote niruhusu nikupigie saluti kwa kuendeleza Libeneke letu kila siku kama huna akili nzuri vile. Unastahili pongezi wallahi!
Mie swali langu kwa wadau wa Blogu hii ni hili neno la king'eng'e la SOCIALIZING. Yaani naomba nifahamishwe kinagaubaga kama ni lugha gongana ama nimepatia ninaposema socializing ni kujamiiana. Kwa maana ingine naomba kutafsiriwa kwa kimatumbi nikitaka kusema socializing nisemeje??
Naomba kuwasilisha.
Mdau Ughaibuni

SOCIALIZING NI KUJICHANGANYA.NO DEFINITION ZAIDI YA HII!!!CHEERS MBEMA MADAFU UGHAIBUNI!!
ReplyDeletekujichanganya na watu/jamii au kujumuika
ReplyDeleteMdau.
ReplyDeleteKwa ufupi, kujamiiana ni kufanya kitendo cha ngono. Sio sahihi kulitumia neno hili ukitafsiri "socializing".
Neno lenye tafsiri ya socializing ni:-
KUJUANA.....hapo ndipo mnapo socialize.
Sawa mkubwa?
Mdau.

Siku ukikua utajiona mjinga sana.
ReplyDeletesocializing sio kujamiiana wewe. Kujamiiana ni matusi. Socializing linatokana na neno Social = kijamii kwa hiyo socializing ni kukutana kijamii iwe kwa mazungumzo, kinywaji, sherehere etc.
ReplyDeletekuingiliana ila naweza kusema kujichanganya..
ReplyDeleteMdau hujakosea hiyo ndio maana yake halisi,ila wabongo akili itawapeleka kwingine
ReplyDeleteKUJICHANGANYA ipo poa kabisa
ReplyDeleteKuna baadhi ya maneo ya Kiingereza hayawezi kutafsiriwa moja kwa moja, kama wewe unavyofikiri, lazima yabadilishwe kidogo ili kuendana na muktadha. Mfano, Waingereza cherehani wanaita 'Sewing Machine', sisi katuiti mashine ya kushonea. Nadhani umenielewa 'SOCIALIZE' ni 'JUMUIKA'
ReplyDeleteMnhhh zaidi imekaa 'kingono'!
ReplyDeleteMichuzi vipi? Mbona hupost majibu yangu??
ReplyDeleteKunani???
Anyway, kwa mara nyingine:-
Kujamiiana ni kuingiliana kimwili.... yaani tendo la unyumba.
Socialising kwa mtazamo wangu ni KUJUANA.
Unapo socialise ni kupata fursa ya kujuana...
Sawa wadau?
KwaMtoro.
ni kujichanganya na wenzie katika mambo mbali mbali yakiwemo kutoka kwenda out na mengineyo.
ReplyDeleteDaaah! We mdau kiboko. Haya jaribu neno kujumuika.
ReplyDeletekustareheeeeeeeee
ReplyDeletekujirusha na wenzio
ReplyDeleteKUJICHANGANYA
ReplyDeleteKuna watu wametaja Kujumuika,kujichanganya,Nadhani wako sawa.Halina uhusiano na kujamiiana wala kufanya mapnz
ReplyDeleteduh babu lugha ya watu sio lazima kuijua ukijua yakotosha mzee
ReplyDeleteNafikiri kujichanganya ina make sense, hili neno lipo sana kwenye somo la sociology na psychology kwa wanaosomea hayo masomo.
ReplyDeleteKujichanganya sio sahihi hapa.
ReplyDeleteIna maanisha to confuse or to have conflicting ideas. Hapo ndio mtu ana jichanganya.
Na angalia tofauti ya maana ya haya maneno:-
"kuJIchanganya" to get mixed up or get confused sio sawa na "kuchanganya" i.e to mix, specifically things, items etc..
Hiki ni kipindi cha zaidi ya dak 40, kukifupisha katika sentensi tatu ni rahisi kuchanganyikiwa!!
Upo mdau?