Uongozi na Wafanyakazi wote wa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (Consolidated Holding Corporation - CHC) wanasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi mwenzao mpendwa, Bwana .Joseph William Hellela, ambacho kilitokea ghafla nyumbani kwake Kiluvya kwa Komba, Wilayani Kinondoni Jumamosi Tarehe 11/02/2012.
Bwana Hellela alikuwa Mkurugenzi wa Madai na Miliki (Director of Loan Recovery and Estates).
Mazishi yamepangwa kufanyika Jumamosi tarehe 18/02/2012 shambani kwake Kibaha.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHAlI PEMA PEPONI.
AMINA.
R.I.P Mzee wetu Mzee Helella.
ReplyDeleteBwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe.
Rest in peace Dad, We miss you so much.
ReplyDeleteEdda, Azda and William Hellela
Mr.Hellela tulikupenda sana lakini mungu amekupenda zaidi.Hakika CHC tumepata pigo., my condolesence to your family na mungu awatangulie katika kipindi hiki kigumu, may your beautiful soul rest in eternal peace.AMEN.
ReplyDeleteR.I.P our dearest uncle, we will always miss you. still can't believe you are gone. we loved you but God loved you more. Lucy, Lilian and Godfrey.
ReplyDeletesi rahisi kukubali lakini imeshakuwa, pamoja na kwamba ulikuwa bosi wangu tukikutana kila siku iitwapo leo j3-ijumaa ukipita ofcn kwangu tukisalimiana na kuingia ofcn kwako, lakini ulikuwa kama ni baba yangu, mbali na kazi tuliongea mengi pamoja na hasa yahusuyo maisha na hata nilipokuwa na tatizo ulinisikiliza, mara ya mwisho tuliwasiliana ijumaa asubuhi ukiniambia kuwa unaendelea vzr, najihisi ofc imepwaya, nitazikumbuka daima busara na hekima zako kwangu, ulinichukulia kama mtoto wako. Nitakukumbuka daima katika maisha yangu yote ya uwahi wangu.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu ameamua kuvuna shambani mwake, basi tunamuomba akakuwekee kwa Amani.
Tulikupenda lakini Mungu amekupenda zaidi pumzika kwa Amani Mr. Hellela. Amen
Rest in peace Mr. Helella, u were so good to us (CHC). We will always remember you.
ReplyDeleteNimemfahamu mzee huyu kwa kipindi takribani miaka minne iliyopita, alikuwa ni mzee asiye mnafiki, ukikosea atakushirikisha katika kukosoa, ni mtaratibu asiye na makuu. Ule usemi wa kuwa watu wema hawana maisha nafikiri unaweza kuwa na ukwelikabisa, hakika ni kipindi kigumu tunachosubiri mazishi ya mzee huyu. Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi na kama kuna mahala aliteleza kiubinadamu basi ampe msamaha na apumzike kwa amani. Amina.
ReplyDelete