Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb) akiwa katika mazungumzo na ujumbe wa wabunge wanaounda Tume ya utumishi wa Bunge la Uganda Ofisini kwake leo jijini leo. Ujumbe huo umewasili nchini jana kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania katika maswala mbalimbali. Kutoka Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara huo Mhe. Emmanuel Lumula Dombo(Mb), Mhe, Okupa Elija (Mb), Mhe. Dk. Chriss Buryomunzi (Mb) na Mhe. Dintu Jalia Lukumu Ngonzi (Mb).
Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda Mhe. Dk. Chriss Buryomunzi (Mb) (katikati mwenye nyeupe) akifafanua jambo mbela ya wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania (Hawapo pichani) wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu maswala mbalimbali katika utawala wa Bunge Jijini Dar es Salaam leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu na Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania katika maswala mbalimbali. Wa kwanza kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo Mhe. Emmanuel Lumula Dombo(Mb), akifuatiwa na Mhe, Okupa Elija (Mb), Mhe. Dk. Chriss Buryomunzi (Mb) na Mhe. Dintu Jalia Lukumu Ngonzi (Mb). Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...