Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wakifurahia pamoja na watoto yatima walipofika katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini jijini Dar es Salaam,msaada wa vyakula na vitu mbalimbali uliokuwa na thamani ya shilingi Milioni 10 ulitolewa na U-turn blog kwa ushirikiano wapamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa amebeba mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es salaam.Wakati wa blog ya U-turn kwa kushirikiana na wasomaji wake wakuu walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo vyenye jumla ya thamani ya shilingi Milioni 10.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiwa na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Kurasini jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa U-turn blog Mange Kimambi na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wakifurahia pamoja na watoto yatima walipofika katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Kurasini jijini Dar es Salaam,msaada wa vyakula na vitu mbalimbali uliokuwa na thamani ya shilingi Milioni 10 ulitolewa na U-turn blog kwa ushirikiano wapamoja na wasomaji wakuu wa Blog hiyo.
Mkurugenzi wa U-turn blog,Mange Kimambi akizungumza na Watoto hao
Huyo Dada ni Mdogo wake Mwamvita mbona wanafanana sana?
ReplyDeleteMange na Mwamvita,
ReplyDeleteAhsanteni kwa Msaada na Ubinaadamu wenu!
Mwenyezi Mungu Mkuu atawazidishia!
Mmmmmh!
ReplyDelete"Mkurugenzi Mkuu" wa Blog?!?
Hivi mnaelewa nyinyi maana na hadhi ya hilo neno au munajiandikia tu?
Hebu nendeni kule BRELA wawafafanulie maana ya "Mkurugenzi"
Mweeh!
Nataka nipeleke posa kwa Mzee Makamba. Je Mwamvita yupo "single"?
ReplyDeleteMwanvita huyo mtoto uliyempa miwani amependeza sana..Tuwapende watoto siyo siri.Baada ya miaka 30-50 hao ndiyo watakuwa wanaongoza nchi yetu tuipendayo.Vodacom mkipata faida si vibaya mkawapeleka pale xxxx barabara ya Nyerere.kuna michezo yao mingi sana,watafurahi sana ila 'bei'!!?
ReplyDeleteDavid V
hONGERA sana wadau wa u-turn na Mange kwa kufanikisha hiyo siku. mmeonyesha moyo na upendo mkubwa sana kwa hao malaika. mbarikiwe wote na msiishie hapo. na hii iwe changamoto kwa wengine wenye nia ya kufanya kama wana u-turn. Ujumbe; EDUCATION IS SEXY
ReplyDeleteMbarikiwe sana kwa kuwapa yatima upendo
ReplyDeleteMdau wa 3 hapo juu Mlevi,
ReplyDeleteUkurugenzi wa Kampuni sio kuwa na koti kubwa au muonekano wa kuwa na kitambi, kinachotakiwa ni uenezi wako hata kama umevaa Gunia!
Wapo Mabosi wangapi ambao hata Shs. 100/= yao ni vigumu kuitoa kwa Wahitaji katika Jamii yetu?
Hawa Madada Mange na Mwamvita kazi wameifanya!
ReplyDeleteSio mchezo kukusanya kiasi hicho cha fedha Mil. 10 na ukazifikisha kunako husika, yataka jitihada na moyo safi!
Kwa wengine kwa mtaji huo wangezitia kibindoni na kuwahi kwenye Yadi kununua gari!
Kweli wameteuliwa!
Hivi hapa nani anamsaidia nani???? TAFAKARI
ReplyDeletewewe david v Acha mambo yako Mwamvita napeleka posa mimi
ReplyDeletetena ngoja niweke na mawasiliano hapa
jokalamdimu@@gmail.com
tuwasilane mwanvita usiogope kuolewa
mwamvita....mwanya au pengo?
ReplyDeleteWajamenituwe na moyo wa huruma kwa kutoa msaada!
ReplyDeleteIbada sio mpaka tuwe ndani ya majengo fulani, Jamii inayo tuzunguka ni moja ya HEKALU KUBWA sana la Ibada na Ibada yenyewe ni kuwajali kwa chochote watoto walio ktk mustakabali wa kimaisha na mazingira kama hawa.
TUACHE UTAMADUNI NA SILIKA MBAYA NA HARAMU KUTUMIA FEDHA NYINGI KWA ANASA NA ULEVI ILI TUELEKEZE NGUVU HIZO KWENYE JAMII YETU KAMA HIVI HAPA!
mwamvita....mwanya au pengo?
ReplyDeleteMdau huo kwa Mwamvita ni mwanya tena wa juu!
Kwa wanaojua mipango wanaelewa mtu akiwa na sifa hii anakuwaje?
Sasa basi inaelekea Wagombea Uraisi Wadau wetu wawili waliojitokeza hadi muda huu kwa Maoni yao kufika bei kwa Binti humu yaani 1.David V na 2.Joka la Mdimu,,,kati ya hao atakaye piga bao atakuwa amepata haswaaa!!!
Mpambano wa kusaka saka kati ya Wadau David V na Joka la Mdimu,,,inabidi Ankal awe ndio Refa wa Mchezo!
ReplyDeleteSisi wengine yetu macho tunasubiri kupewa kadi na kuitwa kwenye mnuso!
Haya Mashemeji watarajiwa Wadau wenzetu David V. na Joka la Mdimu,
ReplyDeletetunasubiri kete zenu kurushwa katika drafti tupate mbivu na mbichi!
Ila sio siri atakayepata atakuwa amepata!