Naibu  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa New York, Dr Asha Migiro (kati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar (kulia) na Kaimu Balozi Mhe Lilian Munanka wakiwa kwenye Hafla ya kumuaga Mhe. Balozi Ombeni Sefue iliyofanyikia Millenium UN Plaza Hotel New York , Nchini Marekani. Mhe. Sefue anarudi nyumbani kushika wadhifa mpya wa Katibu Mkuu Kiongozi.
 Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Los Angeles, California, Abdul Majid (kulia) na Radia Dahal.
 Mhe. Balozi Ombeni Sefue (wa pili toka kulia) akipiga picha ya pamoja na Mwambata wetu wa Jeshi Ubalozi wetu Nchini Marekani Brigedia Jenerali Maganga (kushoto) pamoja na Mama Maganga wakiwa pamoja na Mke wa Balozi wa kudumu wa Somalia Umoja wa Mataifa Dr. Elmi Ahmed Dualeh.
 Kutoka kushoto ni Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Mhe. Kaimu Balozi Lilian Munanka, Mama Sefue, Naibu Katibu mkuu Umoja wa mataifa, New York, Dr Asha Migiro na Tully Malecela.
 Kutoka kushoto ni Given Malecela, Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Mama Sefue, Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, New York, Dr. Asha Migiro na Dr Crispin Semakula.
 Kutoka kushoto ni Edward Taji, Love Maganga, Mariam Mkama, Naibu katibu Mkuu Umoja wa Mataifa New York, Dr. Asha Migiro na Mayor Mlima.
 Kutoka kushoto ni Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Brigedia Jenerali Maganga na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar.
 Kutoka kushoto ni Mugendi Andrew Zoka, Love Maganga, Mariam Mkama, Mama Sefue na Afisa Ubalozi, Edward Masanja
 Kutoka kushoto ni Dr.Crispin Semakula, Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Dr. Asha Migiro na Ndaga Mwakabuta
 Wafanyakazi na maafisa wa Balozi za Tanzania, Washington, DC na New York wakipiga picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Balozi Ombeni Sefue na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar.
 Kutoka kushoto ni Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar, Naibu Katibu Mkuu umoja wa Mataifa, Dr. Asha Migiro na Mhe. Balozi Tuvako Manonge ( msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Safi sana..'Chapeni kazi chapeni' kazi watanzania tuna 'vichwa vizuri' kweli kweli tatizo hatujitambui ndiyo maana tupo hapa tulipo.

    Keep well all.

    David V

    ReplyDelete
  2. 100% confidence levelFebruary 25, 2012

    Direct thanks for your excellence the retired permanent Tanzanian ambassador to the United Nations for your virtually recognized contributions to the world Institution.We are sure the same contributions and more capabilities and abilities you have,will at the large extent be utilized for the sake of the Tanzanian Public Service collateral to the Presidents Directives.

    ReplyDelete
  3. Ndugu Michuzi, Asante mkuu, na kaza buti kuiendeleza blogi yetu tutkufu, ila tafadhari nakuomba hata sisi wa chini na masikitiko yetu usitusahau sana , tuwekee malalamiko yetu humu ili hawa watu wa mikoti na vibegi kwapani waone na wasikie tunavyoteswa. Mimi niko Magomeni Mapipa nimekatiwa umeme makusudi kwa sababu zao wenyewe hawa Tanesco , bili zangu za kila mwezi huwa nalipia bila kuchelewa au kuzidisha siku, sasa imekuwaje mwezi huu wameniletea bili ya millioni 19 ??? kwani mimi ni Baharessa au kiwanda cha chuma ?? nina biashara ya Kimgahawa tu na siku zote bili huwa inakuja laki 6 , laki 7 kwa mwezi na zinalipwa zote.Jamani risiti zote ninazo kwenye faili langu, nalia jamani sina umeme,imebidi nitupe kuku na nyama kwenye friza langu maana waliharibika . kwa nini hawa tanesco badala ya kutufanya wateja wao marafiki wanatufanya maadui zao ?? kwa nini wasiige mfano wa TRA ??? au ndiyo kutunyanyasa kwa vile wao ni shirika pekee nchini la kutoa umeme ?? Ndugu zangu wapenda amani , wale mlioko majuu na sisi hapa nyumbani, nawaombeni msaada wa maoni, kama kuna mtu mwanasheria au mwenye ufahamu zaidi , mnieleze wapi niende ili nikatendewe haki. Mungu tubaliki na ibaliki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Hizi Mheshimiwa kichwas Akili sana.

    ReplyDelete
  5. Michuzi tafadhali - Huyo Ndaga Mwakabuta ni (Dr Ndaga Mwakabuta) naomba usahihishe hilo kosa Asante.

    ReplyDelete
  6. michuzi huyu demu haitwi radia dahl bali anaitwa rabia dahal na alikuwa jirani yangu sana dar mtaa wa gerezani. na ku miss rabia, salaam kutoka new york

    ReplyDelete
  7. sasa kila mtu akiweka cheo chake mbele ya jina lake patatosha humu? Dokta Ndaga, Mhudumu Japhet, Dereva Lusajo, Kondakta Bakari, Mesenja Bwire, Balozi Sefue, Mpiga Picha Michuzi, Opereta wa simu Kajala, Mhandisi Byabato. Hakuna ulazima wala umuhimu kwa nyie Engineers na Doctors kutaka kazi zenu zitangulie mbele ya majina yenu na wala sio haki yenu. Cheo chako kazini kwako tu.

    ReplyDelete
  8. Jamani naomaba tuelimishane Dr sio cheo au kazi ya mtu. Sasa kama hujui tofauti ya hivyo vitu viwili naomba leo ufanye utafiti juu ya hizo tofauti. Ni vizuri kujielimisha ili ukitoa mchango wako mahali kama hapa usionekane unaongea "pumba". Na kwa ufafanuo huyo Dr Ndaga ni engineer sio tabibu -- Ndo maana ni muhimu kujua hizo tofauti.

    ReplyDelete
  9. Isipokuwa kwa 'Heshima' ni vema wanao stahiki watambulike kwa 'Uzito wa Makoti yao'!

    Eng. Galusi Kapakapa na sio Galusi Kapakapa.

    Dr.Bahati Safari na sio Bahati Safari.

    SHEIKH.Hassan Bakari na sio Hassan Bakari.

    Mch.Ernest Kasubi na sio Ernest Kasubi.

    NI VILE,

    PANA TOFAUTI KUBWA SANA KATI YA MTU ALIVYOKUWA BADO HAJASOMA NA WAKATI AMESHAKUWA AMESOMA!

    ReplyDelete
  10. ELIMU MCHEZO?

    Wako watu wangapi wenye Akili nyingi,Juhudi,Wepesi wenye haraka (Ma sharp,Madaraka,Fedha na Ujanja wao lakini kusoma wameshindwa?

    Wajameni wenye Elimu zao wacheni waitwe kwa Viashirio vya Ustahiki wao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...