Na Mwandishi Wetu,Dar es salaam.
WAKATI mjadala wa Mabadiriko ya Sheria ya Katiba Mpya ukiendelea Bungeni,baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wamewataka Wabunge kuacha kuwahadaa wananchi kwa kuyumbisha mchakato wa katiba mpya na badala yake waweke mbele maslahi ya Taifa.
Viongozi hao walitoa kauli hiyo kufuatia misuguano iliyopo baina ya wabunge wa Chama tawala CCM kwa upande mmoja na CHADEMA kwa upande mwingine kuhusu Mabadiliko ya Sheria ya Marekebisho ya Katiba mpya yaliwasilishwa bungeni na Serikali.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia yeye alisema mchakato wa marekebisho ya sheria hiyo lazima umalizike kwa wakati ili kutoa nafasi kwa utekelezaji wa sheria hiyo.
Alisema kuwa, malumbano yanayoendelea ndani ya Bunge yanahatarisha mustakabali wa utekelezaji wa sheria hiyo kwa wakati.
Mwenyekiti wa chama cha UPDP Fahamy Dovutwa yeye alisema, wabunge waweke maslahi ya taifa mbele badala ya kuangalia itikadi zao huku Peter Kuga Mziray wa APPT Maendeleo akiwataka wabunge wa CCM kuunga mkono mabadiliko hayo ili mchakato huo uanze.
Hata hivyo baada ya malumbano ya siku mbili, wabunge walipisha mabadiliko ya sheria ya uundwaji wa tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu uandikwaji wa katiba mpya.
Kufuatia hatua hiyo sasa Rais Jakaya Kikwete anaweza kuunda tume hiyo, ambayo itakuwa na kazi ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu uandikwaji wa katiba hiyo.
Mkiangalia maslahi yenu binafsi tutawafukuza kazi wote, subiri uchaguzi ujao na tunaka tuone hayo mabadiliko kabla hayajasainiwa kuwa sheria. Sasa hivi wananchi hatutaki mchezo tutawaendesha kama bado mnafikiria kufanya mambo kwa maslahi yenu binafsi sisi wananchi ndo tumewatuma lazima mtutetee sio mnatetea posho zenu wenyewe!
ReplyDeleteJamani Watanzania wenzangu tuwe makini wala hakuna tunakokimbilia kuweka katiba mpya.Shida yetu kuwa na kitu cha manufaa kwa vizazi vyetu.Tamaa zisitukimbize.
ReplyDeleteWakowengi wanatuendesha mbio kwa maslahi ya familia zao si kwa sababu ya nchi.Hiyo dhambi.
Twende pole pole kwa kukubaliana watu wote na pande zote ziwe na roho kwatu.Tusipeleke hoja za kusaidia nyoyo zetu na kufaidisha watoto wetu.Kwani dead line lazima hata kama mambo hayajawa sawa na shwari?
Acheni kutafuta sifa katika hili.Nani mnamlaumu mnapoongea kwa jazba?Hii ndo katiba tulokuwa nayo siku zote sasa nani tunamlaumu!Tunatakiwa tujadiliane kwa tulivu na ukomavu maana tunataka kitu kipya kwa kuendana na wakati wetu.SaS TUNAPOONGEA KWA LAWAMA TUNAMLAUMU NANI.Acheni sifa za majukwaani.Kuongea saaaaana nako kunafichua ujinga tulionao katika hoja.
Hata kama tukienda miaka mitano saba shida ni nini tunakimbilia wapi!Kwamba tu tumalize wakati fulani yupo au kwa kuwa mbunge fulani awepo bado jimboni watu wake wasikie!
Mipango ya nchi yaweza kuenda hata miaka 20 si lazima katika kipindi cha wabunge watoa hoja.