Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza leo na Madaktari kufuatia sakata la mgomo wao uliodumu kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili sasa wakati alipofika kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kukutana nao na kusikiliza malalamiko yao.Pia kutokana Malalamiko ya Madaktari hao ya kutokuwa na imani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt. Deo Mtasiwa.Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda amesema amewafuta kazi wakuu hao kuanzia leo hii kutokana na kuonekana kuwa wao ndio kiini cha mgogoro huo ambao umekuwa ukisababisha matatizo makubwa kwa taifa.Waziri Mkuu amewataka Madaktari waunde kamati maalumu ambayo itakusanya mapendekezo ya madaktari wote na kumpelekea yeye ili aweze kuyafanyia kazi,huku akiwataka Madaktari hao kurudi kazini na kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa hapo awali.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (katikati) akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Memejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela wakisikiliza kwa makini malalamiko na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na madaktari leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Baadhi ya Madaktari wa Muhimbili wakizungumza huku umati wa madaktari wengine ukiwa umetulia kusikiliza.
Sehemu ya Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda wakati akizungumza nao leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hospitali hiyo leo.
Waziri Mkuu akiagana na baadhi ya Madaktari wa Muhimbili waliokuwa nje ya ukumbi wakati akiondoka.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick mara baada ya kuzungumza na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.












He, makubwa, siasa jamani, Mh! Kumbe Waziri Mkuu anaweza kumsimamisha Katibu Mkuu wa Wizara kazi? Mbona alishindwa kumsimamisha Jairo aliyekuwa Katibu Mkuu nishati?
ReplyDeleteChonde tufanye haraka makubaliano maana ndugu zetu wanaumia kwa maumivu bila huduma mahotelini.
Tatizo sio katibu mkuu wala mganga mkuu wa serikali, bali ni Pinda mwenyewe. Ikiwa angelikwenda kuonana na madaktari Starlight hotel, je mgomo huu ungelifika leo? Iweje leo amewafuata? Kwa nini atafute mchawi katika mazingira haya?
ReplyDeletesafi sana sasa kinaanza kueleweka, blandina nyoni mwisho wa ubabe sasa kafanyie ubabe huu kwenu, ulizani unaburuza watoto sio umeona nguvu ya umma?
ReplyDeletemdau majuu
ILISHINDIKANA NINI TANGU MWANZO KUKAA NA KUONGEA PAMOJA MPAKA HALI IMEKUWA MBAYA KIASI HICHO. SAFI SANA KATIBU MKUU NA MGANGA MKUU NJE NDIO CHANZO CHA MGOMO HUU. HUYU MKUU WA MKOA NI JOTO AU STAILI NINI KUACHA KIFUA WAZI NAMNA HIYO?
ReplyDeletejamani du?pamoja na umaskini hata kufukunza ni shida,hivyo ndiyo waziri mkuu anatakiwa awe tena wote waondoke ,waziri na naibu wake kwani safu yao yote ni moja kuwaacha hapo watakuwa bado tatizo tu,uongozi wa afrika au kiongozi wa afrika anatakiwa awe na maazi ya haraka ,sisi ni maskini ok,hata tukifanya makosa hatupendi kukubali ;pinda piga msumari mwingine kwa walio baki please
ReplyDeleteSafisana, Fukuza na hao wengine, huyo Mponda na Mwenzake L.Nkya. Timua wote.
ReplyDeleteAibu kubwa waziri mkuu,umeweza kumfukuza KATIBU MKUU AFYA Nyoni ilikuwaje sheria haikukuruhusu kwa katibu mkuu NISHATI NA MADINI MR.Jairo.usituchanganye mtoto wa mkulima.
ReplyDeleteANY WAY,
Any people anywhere, being inclined and having the power, have the right to rise up, and shake off the existing government, and form a new one that suits them better. This is a most valuable - a most sacred right - a right, which we hope and believe, is to liberate the world.
Abraham Lincoln
Mmh! Makatibu wakuu ni wateule wa Rais, je waziri mkuu ana uwezo wa kuwafuta kazi?. Naungana na mtoa maoni wa mwanzo, mbona kwa issue ya JAIRO,waziri mkuu-Pinda yeye alisema hana mamlaka ya kutoa maamuzi kwa kua ni mteuliwa wa Rais?
ReplyDeletePili "kufutwa kazi" kwa maana ya CCM ni nini? kusimamishwa, kuamishiwa wizara/idara nyingineor kufukuzwa kazi? Isije kesho tukasikia ameteuliwa kuwa balozi Ughaibuni!!
Je waziri wa Afya na naibu wake bado wataendelea kuwa kazini? mpaka lini?Hawa nao wanatakiwa kutimuliwa mara moja.
Kumbe Pinda una makali??Walikuwa wanakudharau hao..Kula vichwa mtoto wa mkulima usiogope.Tuko pamoja
ReplyDeleteDavid V
Mapaka ndugu zetu wameumia kiasi hicho ndoi tamko linatoka? Hivi huyu Blandina ni mwanamke kama wanawake wengine au aliwahi kuzaa akasikia uchungu? Inasemekana hata alipokuwa katibu mkuu maliasili mambo yalikuwa hivyo hivyo yake ni kununia manaibu waziri, anaelimu gani?
ReplyDeleteKwanza inatakiwa kuanzia katibu na manaibu katibu lazima wawe ni madaktari la sivyo hawataweza kujua ugumu wa fani hii.
Jamani wadau naomba kujua CV ya Blandina Nyoni.
ReplyDeleteMkuu wa mkoa Dar anadhalilisha VIFUA VYA WANAUME hata Vest
ReplyDeleteulikuwa wapi siku zote pinda saivi ndio umeona haifai ukaja hapo hospital, nahuyo ni joto au kutuachia kifua wazi khaaaaaaaaa watu wengine bwana mkuu wa mkoa
ReplyDeleteHapo sasa mtoto wa mkulima unaongea. Timua hata huyo Dr. Mponda na Dr. Nkya wakalime mihongo huko Ifakara na Moshi. Ikiwezekana huo uongozi wote unatakiwa uchukuliwe hatua mara moja na hata kuepelekwa mahakamani. Wakajibu kesi ya mauaji maana watu wengi sana wamepoteza maisha kwa ajili ya ubabe na uzembe ambao usiovumilika. Hata huyu mama Dr. Mary Njerekela alikuwa daktari wa kansa za matiti (MEWATA) halafu gafla incharge wa Muhimbili. Huyu naye anatakiwa atimuliwe kazi. Fumua uongozi wa Wizara ya Afya wote na mweke Dr. Ulimboka awe Mganga mkuu wa Wizara.
ReplyDeletekwa maana nyingine, waziri mkuu kala matapishi yake mwenyewe!
ReplyDeletejamani huyu mkuu wa mkoa kama kakurupushwa kutoka bafuni heee makubwa ....
ReplyDeletesasa huyu mkuu wa mkoa kuonesha kifua hivyo ndio nini?? loooh, mbele ya mkuu wako, ndio vazi la kazini jamani?? au Dar joto??
ReplyDeleteYule mama Nkya nilikuwa namuheshimu sana, jana alini kwanza mpaaka basiii! sikuamini kama ndio jana alikuwa anahojiwa, nilihisi ni rekoded. SHAME ON HER! na pia hii inaonesha jinsi gani viongozi wetu wanaona kuwa bado wanaweza kuwa juu ya sheria, too bad.
ReplyDeleteHUYU WAZIRI MKUU SIMUELEWI KABISA SASA KUWAFUKUZA HAWA VIONGOZI WENGINE KWANI ONGEZEKO LA MISHAHARA LINATOKA KWA HAWA NI LINATOKA SERIKALINI NA SIO KWA MGANGA MKUU
ReplyDeleteKwa nini ilichukua muda wote huo kama suala lilikuwa rahisi ki hivyo?
ReplyDeleteSafiii mtoto wa Mkulima. Likiisha hili tunataka kuona la posho za wabunge nalo serikali inaonyesha makeke yake. Tumechoka kuchanganywa akili na kuzinguana.
ReplyDeleteHii serikali kichekesho fulu. Pinda Mamlaka anayo, alikuwa anasubiri nini!!! Nilisahau pia kuwa Blandina Nyoni ndiye aliyekuwa Katibu wa wizara hiyo; ki ukweli huyo mama ni nuksi, alifanya ubabe wizara ya mali asili na utalii akamezewa tu, this time amefikwa. Go ahead pinda ila ulichemsha last time ulipotishia madaktari, hauoni ulijidhalilisha!!!! tuko nyuma ya wananchi wanaoteseka hosipitalini na soi wanasiasa waongo kama nyie Pinda na CCM yenu!!
ReplyDeletegd job baba Pinda,mungu bariki Tz, msimamie waziri wetu mkuu ktk maamuzi yake ya busara ambao ameutoa, ndugu zanguni madaktari basi sasa inatosha rudini makazini kuwahudumia wale wote wanaotaka huduma zenu, mbarikiwe wote.
ReplyDeleteSUALA SI KUISHIA KWENYE KUFUKAZA WAKUU WATENDAJI NI KUTATUA MATATIZO TA MADAKTARI
ReplyDeleteHivi madaktari wakigoma hivi kwa wiki mbili na watu wamekufa sana bado wanalipwa full salary kwa siku ambazo hawakufanya kazi? Kama mtu amegoma kwa wiki mbili atalipwaje mshahara wa mwezi mzima? Kuna mtu anaweza kufafanua hilo? Mdau-NYC, USA
ReplyDeleteTulisha sema humu Blandina Nyoni asiendeshe Wizara kama anavyompelekesha Mumewe nyumbani kwake sasa mnaona?,,,
ReplyDeleteYamesha mkuta anaenda chemsha mahindi na kukaanga mihogo!
Tena tafadhali awe 'black listed' hana sifa za Uongozi asipate kazi nyingine Serikalini!
Pinda kiungwana alitakiwa na yeye kujifukuza, kwani yy pia alichochea huu mgomo kwakukataa kukutana na Madaktari pale starlight na kuwatishia kuwa wasipo ripoti kazini wote wamefukuzwa kazi.Kwa kuwa ajajiuzuru Sasa inabidi Rais amuadabishe PM.
ReplyDeleteSi kwamba Blandina na Mganga Mkuu walikuwa wakitekeleza maamuzi ya Waziri na Naibu Waziri? Au inammanisha walikuwa na kiburi?
ReplyDeleteBLANDINA amevurunda sehemu nyingi wizara ya utalii ndio akifisadi sana.alitakiwa siku nyingi atolewe nje na mtandao wake wa watu wa Kusini.hata wabunge walilalamika sana kikao cha bunge kilichopita jinsi blandina na yule kigogo aliyestaafu walivyojaza ndugu zao wizara ya maliasili na Utalii.
ReplyDeleteJP mtu wa blandina sijui leo atakuwaje pale kwenye kona ya Jasmine.Mtaa wa Samora.
Hivi Tanzania hii ukisema ukweli ni kosa la JInai?, kukamatwa kwa ANANILEA NKYA inashangaza ila yana mwisho.
ReplyDeleteMGOMO: Mimi sijapendezwa na hatua iliyochukuliwa na serikali kwa sababu wamechelewa na watu wamekufa na hakuna njia yoyote ya kurejesha uhai wa watu hao.
tuungane Watanzania kudai vipande 26 vya keki. Refer DVD YA UPUUZI WA MASOOD KIPANYA.
KWA NINI HII IMEKUWA ISSUE MBONA BABU WA LOLIONDO HAJA OMBA NYONGEZA YA MISHAHALA YA WAFANYAKAZI WAKE. PIA 90% YA WATANZANIA WAMEKUNYWA KIKOMBE SASA KWA NINI WAFE MUHIMBILI? MIMI NAONA UTALATIBU WA KWENDA LOLIONDO UENDELEE WATU WAKATIBIWE NA NABII BABU.
ReplyDeletesiasa za bongo bana kazi kweli kweli sasa mi nakuomba sana mama nyoni mungu ndio anajua kua uliweza kuwasaidia watanzania walalahoi waliweza kwenda kutibiwa nje ya nchi tofauti na wengi wanavyajua sasa waachie waendelee kuwatibu hao madaktari vimeo wetu hili vifo viendelee kwa walalahoi mi nakuomba usikubali kurudi kwa heshima na moyo ulionao hiyo wizara umeosaidia sana tofauti na hao maktari wetu wanaoishia kutibu km wanganga wa kienyeji
ReplyDeletealiyewakemea kama watoto madaktari ndo wa kumtimua maana yeye ndo alitia petroli kunakofuka moshi..wote tunamjua wala hamna haja ya kumsema!!
ReplyDeleteHuyo mama KATIBU MKUU MFUKUZWA aende zake Jikoni nyumbani kwake akachambue Mbaazi na kukuna nazi!
ReplyDeleteKazi ya kufua na kumpikia Mumewe ndio anayoweza na sio Wizara ya Serikali!
Imetosha, sasa basi hawezi kuiendesha Wizara ya Serikali kuigeuza kama jikoni kwake nyumbani!
Mambo ya bangusilo hayo, mbuzi wa kafara. Watu waliomwagia petroli moto wa mgomo huo ni wengi zaidi ya hao, akiwemo mmoja aliyegoma kwenda mkutanoni Starlight.
ReplyDeleteYaani kwenye kazi' wanaleta mchezo, hapana jamaani, watu wanaumia, watekeleze kazi zao, sio kuleta mchezo, viongozi wasio faa, ni kutimuliwa tu ndi dawa yake, na serikali nayo iwangalie madaktari, kimaslai' kwani madaktari wana kazi kubwa, kuliko hata hao viongozi jamaani, daktari ni mtu muhimu sana naye katika kila jamii zetu, wanatakiwa wapewe kipaumbele, na serikali, kushinda hata sekta zingine, madaktari na walimu, nawakilisha.
ReplyDeleteVioja hivi!. Hatimae simba amekubali kunywesha chai. Ni huyu huyu aliwangurumia paa na p/milia akiwa porini leo waungwana wammywisha chai tena mkia kaufyata.
ReplyDeleteHongera madakitari na wananchi kwa ujumla kilio chenu kimesikika mpaka simba angurumae kuwala wenziwe.
Msh. M/mkoa bausa.
NAOMBA SANA MADAKTARI WACHUKULIWE HATUA KWA KUGOMA KINYUME NA SHERIA NA KUSABISHA VIFO VYA WATU ZAIDI YA MIA MOJA, SHERIA NA HAKI IFUATWE
ReplyDeleteWAZIRI MKUU AJIUZURU KWA KUTOA KAULI ISOO YA KWELI "KWAMBA ASIERUDI KAZINI SIKU ALIYOAGIZA AMAJIFUKUZISHA KAZI ATEKELEZE HILO AMA AKANUSHE
Ah!yale yalee..historia inajirudia,naibu waziri,katibu mkuu,mganga mkuu na mhe nanilii wote ni wale wale wenzetu wa mavumbini!
ReplyDeleteHuyu Blandina Nyoni ndio chanzo kikuu cha kuchochea mgogoro, hafai tena kurudi kazini, aliivuruga Wizara ya Maliasili na kaja kuivuruga Wizara ya Afya. Ndio haya mambo ya kupewa wadhifa kwa kujuana, uongozi zi kutetemesha watu bali ni maelewana na wale unaowaongoza
ReplyDeleteyani siku zote hizo mkurugenzi, katibu mkuu , mganga mkuu hata waziri wa afya walikuwa hawajui tatizo la madaktari...huu ni kuwandanganya watu..kufutwa kazi na kesho kuajiliwa sehemu nyingine ndiyo itakavyo kuwa. Wa kufukuza kazi siyo hao wawili kwani wakubwa weingine wa muhimbili walikuwa hawaoni shida zote hizo..Ni aibu imechukuwa watu kugoma kwa wiki mbili lakini wabunge mwajipa pesa bila shida na malalamiko . Nchi yetu inaelekea pabaya wakuu wanafanya vyao haraka na kutesa watu wa maana kama madaktari. Lakini tunaelewa kwani wengi wao hawatibiwi hapo muhimbili so next year inaweza tokea tena.Poleni sana kwa walio poteza maisha kwa shida hizi za mgomo ambao kiini chake ni wakubwa wetu so kama kufutana kazi basi iianzie huko juu.
ReplyDeleteBalozi za nje zinasubiri hao waliofukuzwa. Maana watapatiwa ubalozi. Tooobbaaaa! Hapakaliki hapo! Timua timua iendelee mpaka NEC ya CCM kULIKO JAA MAFISADI, isiishie kwa hawa wawili tu!
ReplyDeleteKwa wale wanaomlaumu Waziri Mkuu kuwa mbona kwa Jairo alishindwa wao ndo hawaelewi. Maamuzi ya jana aliyatoa baada ya kushauriana na 'Serikali'. Hivyo alikuwa na baraka zote kufanya hivyo. Big up mtoto wa mkulima tuko pamoja.
ReplyDeleteHuyo anayesema Blandina anakwenda kuchoma mahindi na kukaanga mihogo anachekesha. The woman is a billionaire.
ReplyDeleteBlandina Oyeeeeeee,utakoma kuringa. Ukitudharau sana sisi watu wa chini
ReplyDeleteMK angEkuwa mwanamke ningesema anaonyesha SN.... sasa hii bwanaa yawezekana alikuwa na haraka akaondoka bila ya kuvaa vest au aliogopa ze komedy wangemuiga.
ReplyDeletehahahahaha,comment zinafurahisha sanaaaaaaaaaaaa.anyway.mtoto wa mkulima alichemsha mwanzo lakini waliompotosha amekula nao sahani moja.yeah nyoni 40 zake zimefika,mkuu wa mkoa ana shida gani kifua nje bila aibu?
ReplyDeleteALUTA CONTINUA!
Huyo mkuu wa mkoa wa Dar kifua nje utafikiri Gbagbo aliposhikwa na wafuasi wa Wattara.
ReplyDeleteMdau wa Fri Feb 10, 06:31:00 AM 2012
ReplyDeleteTuna Vijana wengi wenye sifa wanahangaikana na makabrasha makwapani kutwa, wakitafuta kazi!
Wengine wakiwa na chupa za maji safi wakipoza njaa na kiu wakiingia ofisi moja hadi ingine kutwa kazi hawapewi!
HATUWEZI RUHUSU AJIRA KWA 'MAGALASA' KAMA HAWA TENA SERIKALINI!
Waliofukuzwa HAKUNA KAZI ZA UBALOZI NJE,,,,waelekee moja kwa moja kwenda kukata mkaa Kaliuwa Tabora!
Blandina Nyoni arudi nyumbani Bomba Mbili Songea akalime maharage!
ReplyDeleteOne down Two to go.....
ReplyDeleteMama mwenye kiburi Blandina amekula 'kisu' watu wanasonga mbele, kwa heri ya kuonana safari njema kwenda Nantumbo Songea kwenu unakwenda kuwa Mama Ntilie au Muuza pombe za kienyeji wa Wachimba madini Migodini!
Mamaa ulicheza na Madakitari enhee?
ReplyDeleteHahaha umeula wa chuya!
Sema tu ulipata bahati ya Kisiasa kwa kazi uliyopewa ingawa uliongoza watu wenye akili zaidi na iliyotulia kuliko wewe!
Jamaa Madakitari wana akili sana na wana roho ngumu balaa ona sasa wamekupiga 'kisu cha Upasuaji',,,chali na UHASIBU WAKO!
UMEFANYIWA UPASUAJI NA MADAKITARI KAMA VILE BILA GANZI!
ReplyDeleteBlandina Nyoni,
Ulilewa na Madaraka ulipopelekwa Chumba cha Upasuaji kwa Madakitari ulipigwa sindano ya Ganzi na Usingizi kama ilivyo taratibu lakini kwa ajili ya Hulka yako ya ulevi ganzi haikufanya kazi!...MKASI WA DAKITARI ULIUSIKIA KWA MAUMIVU ULIVYOPITA WAKATI WA UPASUAJI...WEWE SI NDIO BABA YAKO ALIKUSHAURI UWE MHASIBU?,,,UGUA POLE, HAO NDIO MADAKITARI!!!!
Blandina umekoma sasa na Madaktari kwa kufanyiwa Upasuaji bila GANZI!
ReplyDeleteRC anakumbuka ujana na pia mkumbuke kuwa Mwanaume hazeeki!
ReplyDeleteCha msingi ni Mawe /Kisu au PESA!
Kazi ya Utawala inabidi uwe Mbabe kidogo utunishe kifua!
Pia muelewe Mwanaume kuwa kifua wazi sio ishu sana, ndio Mtalimbo wenyewe, ndio 'mabunduki' yenyewe, (ndio Ujabali wenyewe),,,kumbukeni INKOSI KAZI NA SHOKA LA CHUMA,,,UMSOLOPAGASI.
Kuanzia juu ya kitovu kwa Mwanaume ruksa angalau kufunika milima ya maziwa kidogo tu ila bonde la kifua kwa Mwanaume kama MK hakunaga shida!
I like it!
ReplyDeleteAs MK way big up!
Kifua wazi kwa Mwanaume si ndio Urijali wenyewe huo, sasa nini?
Man u have to walk in mockery with boasting!
Ahhh acheni hizo raha ya Mwanaume shuruti uende kifua mbele mustarehe hakuna wasiwasi, hamuoni kuwa hiyo ndio raha ya u Jogoo?