Dr. Engineer Shabani G Kachua akijiandaa kuingia kwenye Professional Engineer Induction Ceremony nchini Canada
Hapa Dr. Kachua akionyesha moja ya Nishani aliyotunukiwa siku hiyo
Dr Kachua akiwa amesimama kwa nyuma na Mainjinia wenzake
Akipiga picha ya pamoja kwa kumbukumbu na mainjinia wenzake.Kwa niaba ya Watanzania ninapenda kukupongeza kwa kuipeperusha vema Bendera ya Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Eee bwana wee Shaban si ulikuwa Phonex?

    ReplyDelete
  2. Bwana Shaba Kachua.. Hongera sana kwa hatua kubwa na nzuri na yenye kufurahisha na kutia changamoto kubwa sana.

    sisi tupo pamoja na wewe ila tu usije ukawasahau wale wa nguvumali na kisosora kule kwenu kwa WAGHOSI -TANGA.

    Shirima

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Dr Kachua, ni matumaini yangu kuwa utakapoamua kurudi nyumbani utakuwa na malengo ya kuendeleza taaluma ya uhandisi na kuutumia utaalam kwa faida ya Taifa.

    Mjengoni tuachieni sisi.

    Mdau

    ReplyDelete
  4. Kachua I'm proud to call you a brother! Big up!- Dj

    ReplyDelete
  5. Safi sana doctar Kachura, fanya fanya urudi bongo uje tuijenge nchi yetu. Usiishie huko kubeba mabox kama wataalamu wetu wengine.

    ReplyDelete
  6. Hongera Eng. Shaaban G. Katua!

    Mzimu mkubwa unaotusumbua nchini ni kuwa Wanataaluma wengi hawapo kwenye Muundo wa uendeshaji wa mambo ,

    1.Mfano wengi wanatumika nje ya nchi, waliopo nchini hawashirikishwi ipasavyo ili kutoa mchango wao nchini,

    2.Huku wengi 'Wakibatizwa' na kuingizwa ktk Siasa (kama Ubunge) badala ya kuendelea na Taaluma zao kitu kinachosababisha mambo mengi nyeti kuendeshwa na Wanasiasa au kuwa mikononi mwa WANASIASA badala ya WANATAALUMA.

    ReplyDelete
  7. Asalale bora Injinia Shabani Kachua abalie huko huko Canada akiwa ktk Taaluma yake.

    Akija Tanzania nyumbani, moja kwa moja atavuliwa Ovalori lake la Uinjinia na kuvalishwa Koti la Uheshimiwa ndani ya mwaka mmoja utamuona Bungeni Dodoma!

    ReplyDelete
  8. Ahhh mambo ya Bongo Engineer Shabani Kachua akirudi kutoka Canada hutamwona ng'o ktk Karakana au Kiwanda, Utamwona Bungeni au Wizarani!

    ReplyDelete
  9. Wewe huyo habebi boxi huko anafanya kazi ya Profession aliyosomea na kachapewa uraia na kanunua na nyumba haji huku bongo kufanya nini serikali yenyewe wachawi tu huku.

    ReplyDelete
  10. Tanga Line, Changa Primary School... Safi saaana Dr. Kachua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...