Mabondia, Selemani Galile kushoto na Thomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano wao jijini Dar es Salaam jana, utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni hiyo Yasin Abdallah Mwaipaya.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao.

"Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.

Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa.

"Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.

Naye kwa upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani

Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled,David Haye, Waldmil Klitichiko,Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi

Zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia,mashabiki marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. jamani hata promota kumsaidia jamaa huyo wa kulia angalau kurekebisha nywele kidogo jamani za miguuni. Ila asitumie wembe kurekebisha.

    ReplyDelete
  2. JAMANI HIZI NJAA MTAKUJA HUA MTU KIMIZAMIZAA , HAWA JAMAA KWA MWANGALIO TU WANAONEKANA NI NJAA.

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  3. HUYU JAMAA MWENYE NYWELE KAMA KUKU ALIYENYESHEWA MVUA,AMECHOKA SANA HAWEZI HIYO KAZI ASIJE AKAWAFIA JAMANI.

    ReplyDelete
  4. BMT iingilie kati. Ngumi za kulipwa Bongo sasa ni usanii mtupu.

    ReplyDelete
  5. jamani mbona wapiganaji wenyewe afya zao haziridhishi? maafa yanaweza kutokea hapo ulingoni...

    ReplyDelete
  6. huyu jamaa wa kulia...sijui BMT wametumia vigezo gani kuruhusu apigane?hata bila maoni ya daktari,ni wazi ni mgonjwa achilia mbali kupigana!acheni njaa jamani,maisha ya mtu haya...!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...