Jiji la Dar linazidi kupendeza siku hadi siku na kulifanya lizidi kuonekana ni la kimataifa zaidi,Hili ni eneo la Kariakoo ambalo kila siku zinavyozidi kwenda na ndivyo vikwangua anga vinavyozidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu huku nyumba za chini zikiendelea kupigwa nyundozz.najua wadau hamtaacha kuosha vinywa ila ukweli utabaki pale pale kuwa maendeleo katika nchini yetu yanakwenda kwa kasi ya ajabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kadri ufisadi unavyoongezeka ndivyo majengo yanavyoongezeka. mafisadi wote wameamua kuwekeza katika majengo na ardhi bila kuulizwa fedha wamepata wapi, ila wananchi walio wengi ambao hawapati fedha hizo hali inazidi kuwa mbaya zaidi ndio maana maendeleo haya si rahisi kuyaona kwa watu.

    ReplyDelete
  2. Hivyo vikwangua anga vijengwe kwa mpangilio. Mamlaka huska iweke utaratibu wa nyumba zilizo mtaa mmoja kupaka rangi inayofanana. La sivyo majengo hayo yanakuwa kama uchafu vile.

    ReplyDelete
  3. Nyumba zimesongamana kiyama!Mwenyezi Mungu atuepushilie mbali gharika kama la tsunami maana likipiga hapo hatubakii hata mmoja, hata hivyo vichochoro vitakuwa havionekani.

    Ile ya Japan bora nyumba zilikuwa kama tu za temporarily,maana livyokuwa zikielea katika maji ilionyesha kweli ni kama mabox hata yakikuangukia unaweza ukapona,sasa hilo zege na nondoo Eeh Mungu atuepushe kabisa!
    Inabidi kufikiria sana kwa huu UJENGAJI WA VIKWANGUA ANGA,ILIVYO KAA KARIAKOO VERY DANGEROUS.TUNAISHI HUMO LAKINI KWA RISK SANA!!!!

    Ahlam UK

    ReplyDelete
  4. Ngoja niwe wa kwanza kuosha kinywa. Ni vizuri na inapendeza ila sambamba na kujenga hivyo vikwanguaanga, juhudi ziende vilevile katika kuboresha miundombinu kama barabara zipitazo hapo, menejimenti ya maji machafu, upatikanaji wa maji na pia umeme. Ningetegemea majengo hayo yangejengwa kwa kuzingatia hayo kwa mfano katika umeme kujenga jengo ambalo linaweza kutumia mionzi ya jua kufua umeme n.k.

    ReplyDelete
  5. We mshamba kweli unafikiri maendeleo ni kuwa na vikwangua anga kariakoo?

    ReplyDelete
  6. Asante sana. kama tunaweza kupata na ya zamani ingekuwa vizuri zaidi...ili tulinganishe

    ReplyDelete
  7. Lakini maji na umeme je navyo vinaenda na mpangilio wa mji au ndo toka enzi za mkorono!!!!?????

    ReplyDelete
  8. katika majengo yote uliyapiga picha huwezi amini hayana parking sasa sijui nani aliyetowa vibali itafika stage tutaingia njini na beskeli kwakukosa parking

    ReplyDelete
  9. hapo sijaona cha kujivunia kwani hakuna mpangilio wowote wa majengo hayo utadhani kila mwenye vijisent basi ruksa kujenga atakavyo.

    wapanga miji kwetu wamelala tu. kama upangaji wa miji ungekua mzuri basi hayo majengo, barabara, huduma za maji-safi na maji taka, open space nk zingeonekana katika hali ya kupendeza sana.

    ReplyDelete
  10. mipango miji..mpange basi na vi garden , sehem za parking , nk sio mabo ya bandika bandua jumba

    ReplyDelete
  11. Hapa ni hopeless bin zero!!! Eti maendeleo, maendeleo gani ya kujenga nyumba bila mpangilio maalum huku wagonjwa Mhimbili na Bugando wakiangamia kwa kukosa matibabu??? "Maendeleo" my foot!!

    You guys need to think outside the box before it's too late.

    Kalagabaho Watanzania.

    N.B. Najua Team Michuzi (or whoever is updating this portal) mnaweza mka-withhold hii coment. But I won't care the less! Because even if you don't publish my message to the public, y'all will have got it one way or the other. Kila siku nasema humu, Wacheni kuwadanganya Watanzania - Hizi siyo enzi za Nyerere - Watanzania wameamka sasa. We know what's going on inside and outside the country - everything!!

    Peace.

    ReplyDelete
  12. Hivi haya ndio mnayaita maendeleo huko Tanzania? Kwa haraka haraka, kuna baadhi ya majengo hapo makubwa yakishika moto magari ya zimamoto yatashindwa kuingia...Ndio maana mfalme suleimani alimwomba Mungu ampatie wisdom.

    ReplyDelete
  13. Inawezekana ni maendeleo kwa karne ya Mtanzania aliyeachwa nyuma huko na asiyefahamu lolote katika ulimwengu huu.

    Hata hivyo, bado ipo haja ya kujifunza mengi tu kutoka kwa wenzetu huko duniani kuanzia ujenzi, mpangilio, huduma na usalama wa wananchi.

    ReplyDelete
  14. Unapoelezea maendeleo sio kuwa na majumba kariakoo hayo sio maendeleo wakati kuna sehemu hata nyumba ya mabati,umeme,maji hakuna sasa hayo unayoyasema ni maendeleo ya nchi sio kweli unachokizungumzia ni kutuonyesha jinsi gani ufisadi unavyoimaliza nchi mji ni mbovu kupita hata ule wa zamani mnajenga mji mpya hakuna hata sehemu za kupumzikia,za kuchezea watoto siku nyingine toa maoni ya kusaidia ni nini tunapaswa kufanya kwa maendeleo ya nchi yote kwa ujumla maendeleo sio kwa ajili ya watu wa mjini tu je wanaoishi vijijini wao hawataki maendeleo?

    ReplyDelete
  15. Finish zake hayo majengo ndani na nje ni mbaya na baada ya miaka kumi wenye nayo watatamani kuyavunja tembeeni duniani muone majengo .

    ReplyDelete
  16. sana vikwangua anga jamani watz watz sijui ni lini tutafika hata tukiwa na elimu bado.
    NO HOUSE PLAN HAKUNA MVUTO JAMANI HATA SIJUI NISEMEJE.ILA LILE LA BABU LOLIONDO LIMEDHIHIRISHA UDHAIFU WETU SINA MENGI;

    ReplyDelete
  17. Wachora majengo Tanzania sio wabunifu wazuri wanajua kudesign mabox finish za ndani pamoja na design mbaya hawataki kutembelea miji iliyoendelea dunia na kujifunza bado washamba wanawashauri wateja wao kupaka rangi za mafuta ndani wakati Dar ni joto . Majengo mabaya hayana mvuto.

    ReplyDelete
  18. I second the guy who said Quoted King Solomon... Dar needs urban planning... The Local government should be held accountable for such a mess.. If I was the mayor or minister of local government I will be ready to pay the price for taking down this kind of shoddy "development".... Some time tough decisions have to be made no matter the political price we pay but at the end of the day the person who will make this decision will be remembered in the long run.... Wahenga walisema usipoziba ufa utajenga ukuta...

    Singing out

    ReplyDelete
  19. hivi mmeenda kimara, mbezi kwa yusufu, mbezi beach segerea, kurasini watu walivyojenga majumba ya fahari, tena unaambiwa huyu alkuwa anauza
    handkerchief barabarani. Hapo kariakoo wanadhihirisha uwezo wao wengine wamejificha. watu hawajengi wanafanya kufuru.

    ReplyDelete
  20. UJENZI TATA NDANI YA KARIAKOO:

    Uyoga na Utitiri wa Majengo marefu mengi ya Ghorofa ktk Kariakoo mengi yamejengwa kwa viwango vya chini (TBS ipo chini kabisa na OSHA)...!!!.

    Ndio ule ule Ujenzi wa Makandarasi kwa mtindo wa TUWE NDUGU CONSTRUCTION CO.LTD. kama hizi CHANGANYIKENI BUILDERS LTD. kama FUNGU LETU ARCHITECT CO.LTD. na NAFUU CONSTRUCTION CO.LTD. ambazo utakuta mfuko mmoja wa Simenti kwa KUFYATUA TOFALI 200 au 300...!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...