Mashabiki wa timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam,wakiwa wamefurika kwa wingi ndani ya uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuishangilia timu yao inayoingia dimbani muda mfupi ujao kumenyana na timu ya Kiyovu ya nchini Rwanda katika mashindano ya Kombe la Shirikisho ikiwa ni mchezo wa pili mara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa awali huko nchini Rwanda.
Baadhi ya Wanahabari wakiwapiga picha watu waliokuwa wamevalia kinyago cha mfano wa mnyama Simba.

Wachezaji wa Simba wakipiga jalamba kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa Kiyovu ya nchini Rwanda wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo.

Globu ya Jamii inakuwa bega kwa bena na Wewe Mdau kuhakikisha inakuletea kina kinachojiri uwanjani hapa na pia Mchezo huu unatangaza Live kupitia Radio Clouds Fm
hivyo BOFYA HAPA kusikiliza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mbona uwanjani hakuna watu a lot of emo\pty seats. Ni watu hawana fedha or wamekataa tamaa na soccer la bongo

    ReplyDelete
  2. Yanga ya RWANDA ni Kiyovu S.C ndio maana Simba S.C. wamewapiga bao!

    ReplyDelete
  3. Inapendeza kuona siku hizi watu wanavyoshabikia soka la nyumbani, sio kutwa nzima game za kigeni, utumwa huo na ukoloni mambo leo.
    Afrika socca oyeeeeee!!!1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...