Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Yahya Khamis Hamad,kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, leo baada ya kumteuwa kushika nafasi hiyo. Hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Luteni Kanali Mohamed Mwinjuma Kombo,kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia  Zanzibar,jana baada ya kumteuwa kushika nafasi hiyo,hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na mdau Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. neno VALANTIA hapo juu lina maanisha nini wadau ??

    ReplyDelete
  2. Hilo ni neno lenye sili ya neno la Kiingereza 'volunteer' kwa maana ya 'anayejitolea'. Hata hivyo valanti hapa Zanzibar hufanya kazi zinazofanana na askario wa mgambo huko kwenu ingawa lenyewe siku hizi limepoteza maana halisi tofauti na zamani. Siku hizi valantia ni ajira yenye malipo. i.e. siyo kujitolea tena.

    ReplyDelete
  3. Hapo ndipo nachanganyikiwa, nani mkuu wa majeshi hapa Tanzania, na ili Valantia ni Jeshi chini ya Mkuu wa Majeshi? maana huyu Luteni Kanali ni Jeshi la Wananchi. Wadau ebu niweke sawa

    ReplyDelete
  4. Volunteer walipata sifa sina wakati wa miaka ya 70 kwa ukamataji wa wavaaji wa "Mabugaluu" na "Mini-skirt" na "Afro" na mikanda ya 007.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...