JINA LA KITABU: MALIPO NI HAPAHAPA
      MTUNZI:  ADELA DALLY KAVISHE 
Adela Daly Kavishe (pichani)   ni mtangazaji wa radio passion FM ambayo inarusha matangazo yake jijini Dar es salaam Ninayofuraha kukamilisha kitabu cha simulizi cha MALIPO NI HAPAHAPA ambacho kimebeba simulizi tatu za kusisimua ikiwemo simulizi inayoitwa DADA YANGU,MAMA MDOGO pamoja na simulizi iliyobeba jina la kitabu MALIPO NI HAPAHAPA 
 Kitabu cha Malipo ni Hapahapa na simulizi nyingine za maisha kinaonyesha hali halisi ya maisha tunayoishi, matatizo tunayokutana nayo na namna ya kutatua matatizo tunayoyapata kwa wakati huo. Pia kwa kusoma kitabu hiki utajifunza mengi kwani kinatoa  picha halisi ya maisha yetu ya kila siku.
Ndani ya kitabu hiki nimezungumzia maisha na mapenzi katika mtazamo halisi na pia kinaonyesha namna mapenzi yanavyoweza kuyageuza maisha kuwa machungu na mafupi. 
Ukianza kusoma kitabu hiki hutakiacha hadi ukimalize kwani hadithi zilizomo zimesheheni matukio ya kusisimua ambayo moja kwa moja yanalenga maisha yetu ya kila siku.
Kupitia vitabu vya simulizi za maisha kama vile kitabu hiki, tunajifunza mambo mengi ambayo yanatusaidia kuishi katika mazingira tofauti ikiwa ni katika shida au raha na hata kujua namna ya kuishi na watu wanaotuzunguka.
Utapata kitabu hiki kwa  bei ya sh 5000 tu.
 Kwa mawasiliano kuhusu upatikanaji wa kitabu hiki.
Tafadhali tumia no zifuatazo +255652343430 au +255752817444
Au kavisheadela@yahoo.com  Unaweza pia kuingia humu http://www.adeladallykavishe.blogspot.com 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. HICHO NI KITABU AU JARIDA? KWA MTAZAMO WA JINSI KILIVYOTENGENEZWA NAONA MUUNDO WA JARIDA SIO KITABU.

    NWAY HONGERA KWA KAZI.

    ReplyDelete
  2. hicho ni kitabu kipeperushi?

    ReplyDelete
  3. Asanteni wadau kitabu kina kurasa 101 labda muonekano katika picha ila kina simulizi nzuri ambazo zinalenga maisha yetu ya kila siku kitafute na ukione kilivyo nadhani utapata picha halisi kuwa ni kitabu nashukuru sana tuko pamoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...