Timu ya Azam Fc Tanzania inaonyesha uwezo wa kumiliki mpira kama Barcelona FC ya Spain au Swansea Fc ya England ktk premier league.

Tuone Azam Fc ya Mbagala-Chalambe, Dar-es-Salaam ikitandaza soka la kitabu na pengine mwaka huu inaweza kushiriki ktk mashindano ya kimataifa Africa na kufanya maajabu zaidi ya timu kongwe za Dar na Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MICHUZI SUALA SIO WINGI WA PASI.ILA PASI ZINATENGENEZA MAGOLI?KAMA KULEMBA TU PASI NYINGI ZISIZO NA MALENGO HATUFIKI POPOTE.TUNAISHIA KUSEMA TUMEFUNGWA ILA CHENGA TUMEWALA

    ReplyDelete
  2. Kufungwa twafunga lakini chenga twawala. Hii mechi pamoja na kupiga pasi na chenga nyingi matokeo yalikuwa Simba 2 na Azam 0. Azam bado wana safari ndefu.

    ReplyDelete
  3. Bado mpira wao ni wa kishamba ila wanaonyesha uwezo zaidi ya Simba na Yanga. Nasema mpira wa kishamba kwa sababu sioni wanafanya nini zaidi ya kutoa pasi tu. Pasi zinatolewa kwa lengo la kutafuta bao/mabao ila wao wanatoa pasi tu. Ushauri wa bure kwa soka lisilokuwa na maendeleo (bongo), msiwaige Barca ama Swansea chezeni mpira kwa uwezo wenu ili nanyi mjitafutie jina si kuiga tu bila malengo. Mnatoa pasi tu kutafuta magoli hamjui, si ujinga huu

    ReplyDelete
  4. Azam yaweza kututoa Watanazania kama tutaacha U-Yanga na U-Simba. HONGERENI SANA AZAM juhudi twaziona ingawaje vikwazo na mizengwe ni mingi kuelekea mafanikio.

    ReplyDelete
  5. waliosifia ni wao na walio ponda ni wao, azam hatuna neno tunapanda tu, yanga katulia, simba bado anatusumbua sumbua lakini atatulia tu. hamieni huku! huko hakuna mpira kuna upinzani wa jadi!!
    Azam fan (tangia mazoezi uwanja wa magereza ukonga)

    ReplyDelete
  6. Simba na na Yanga hamna kitu zaidi ya upuuzi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...