Amiri Jeshi mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange(kushoto) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,(kushoto)Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha mkuu huyo mpya wa JKT ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mzee Albert Ndomba(85),baba mzazi wa Mkuu Mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba(wapili kushoto) baada ya halfa ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni mke wa Meja Jenerali Ndomba na waliosimama nyuma ni wanafamilia.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi mkuu mpya wa JKT meja Jenerali Samwel Ndomba wakati wa hafla ya kumuapisha iliyofanyika leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria.
JKT:
ReplyDeleteNi muhimu kufikiria kuirudisha upya kwa ajili ya heshima, dira na mwelekeo wetu kama Watanzania.
-Ni dhahiri kuwa Utaifa, Uzalendo na Utu vimeanguka kwa kasi ya ajabu.(hatufanyi vizuti ktk michezo kama mpira, waajiriwa hawajitumi, wafanya biashara wanahujumu, wakulima hawawajibiki, kila mmoja anawaza ufisadi hujuma na kunufaika peke yake, maslahi ya Taifa na Nchi hayazingatiwi kabisa!)
-Ni dhahiri kuwa kwa hivi sasa idadi kubwa ya Vijana ni magoigoi.
-Ni wazi kuwa idadi kubwa ya Vijana hawajitambui kabisaa.
-Ni wazi kuwa maadili yameanguka zaidi kwa kutokuwepo na Jeshi hili.
-Ni wazi matatizo kama ya Vijana kukosa ajira na Uhalifu vitatatuliwa na urejeshaji wa Jeshi hili.(Mfano uwepo wa Usafiri wa Bodaboda angalau umepunguza kasi ya Uhalifu Mitaani)
-Ni wazi kuwa madhara makubwa kabisa ya Kijamii yaliyopatikana nchini kwa kusitishwa Jeshi hili yanalingana na Uimarikaji uliopatikana wa kupunguza Bajeti na Matumizi ya Serikali?
-Ni wazi kuwa IMF (Shirika la Fedha la Kimataifa) halikutupa ushauri sahihi wa kulisitisha Jeshi hili mwaka 1994, eti ili kupunguza Bajeti na matumizi ya Serikali, sasa je kama jeshi lilifutwa Matatizo ya matumizi ya Serikali hadi leo yalitatulika?
mimi nimepitia JKT na sioni umuhimu wa chombo hicho. mapesa yanayotumika kuendesha jeshi hilo yaelekezwe kwenye kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vyuo vya ufundi.
ReplyDeleteJKT kila mtu alikuwa anatafuta mbinu ya kukwepa kazi. huwezi kumlazimisha mwanafunzi wa form 6 kulima kwa jembe la mkono.
Mdau Anonymous wa Mon Mar 19, 06:13:00 PM 2012
ReplyDeletemwanafunzi wa form 6 kulima kwa jembe la mkono.
Kwani kuna tatizo gani kulima kwa jembe la mkono?
Si ndio ukakamavu wenyewe huo?
Je kulima kwa mkono na madhara ya kuanguka kwa Jamii kwa kuwa na idadi kubwa ya
-Mashoga,
-Mateja na Vibaka
-Wasichana machangu
-Matapeli
-Machinga
Ni nini bora kati ya kuacha kuwaweka kundi hilo la Jamii walioathirika kwenda ktk huduma za JKT na kukwepa wasileime kwa jembe la mkono?
Hivi Mwamunyange ni Meja Jenerali, Luteni Jenerali au Jenerali? Tujtumie titles kwa uhakika.
ReplyDeleteDah mke wa Meja!
ReplyDelete