Mimi naitwa Miriam, 
Ninawatunza watoto  watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 30 .Watoto hawa wana umri  kati ya miaka 4-13. Nimefanikiwa kufungua kituo cha watoto maeneo ya Mbezi Mwisho ambapo watoto 10 (wa kike) wanakaa hapo kwa sasa kwani hawakuwa na mahali pa kukaa kabisa. 


Nimeshindwa kuwaweka wote kwenye kituo kwa sababu sina pesa ya kuwahudumia wote kwa wakati mmoja wakiwa hapo kituoni na mimi lengo langu ni kuwasaidia waweze kupata maisha bora.


Pamoja na kufanikiwa kufungua kituo nina changamoto za mahitaji kama vitanda, magodoro hayatoshi, sare za shule za watoto, mashuka,chakula, simtank la maji,nguo za watoto, meza na viti vya kusomea na mahitaji mengine madogomadogo. Pia tunaomba kama kuna mtu ataguswa kutusaidia fridge ili tuweze kuhifadhi  chakula na vitu vingine kwa wingi ili kupunguza gharama ya kununua vitu kila siku.

Kwayeyote atakayeguswa kutusaidia wasiliana nasi kwa  namba 
+255757 855 858 au +255655 855 858
 Watoto wanaolelewa kituoni hapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. naomba unitumie email kwenye hii address. kokodemelo@yahoo.com

    asante
    pat

    ReplyDelete
  2. UNCLE KWA SIE TULIO NJE YA NCH TUTACHANGIA VIPIIIIIIIIIIII, SHUKRAN

    ReplyDelete
  3. mimi sina uwezo ila tu imenitachi sana jitihada yako ya kuwatunza hawa watoto na Mungu atakusaidia na ataleta heri zake. Usikate tamaa kwani unayoyafanya ni ya maana sana tena sana.NIPO PAMOJA NAWE MORALLY

    ReplyDelete
  4. Habari yako dada! nitumie email, rumishael@acaciagems.co.nz

    ReplyDelete
  5. Uchangiaji unahitajika Wandugu, tuache anasa zisizo na maana na tufanye mambo kwa kuwaangalia hawa Watoto.

    ReplyDelete
  6. Wale wenzetu wa Ugiriki, fanyeni mambo ya maana sasa. Sio tu kujisifia huko maisha ni bomba. Katibu hamasisha watu wako sasa mtumieni huyo mama msaada. Tena kuna wengine wameacha watoto waliozaa huku Bongo bila hata kuwasiliana nao. Wakati ni huu sasa, si kujisifia kuwa Easter tunajirusha na Matonya. Easter mjirushe na yatima na Mungu atawabariki.

    ReplyDelete
  7. Mnaweza pia kutupata kwenye blog www.guardianangeltz.blogspot.com

    ReplyDelete
  8. mnaweza pia kutupata katika Blog ya www.guardianangeltz.blogspot.com

    ReplyDelete
  9. Kwa kweli nami nimeguswa sana na ombi la dada huyu ambaye amejitoa kwa moyo kuwasaidia watoto hawa ambao kweli ni watoto wa Mungu.

    Mimi ninamhakikishia kwamba Mungu hatawaacha watoto hawa kuwasaidia kwa chakula na mahitaji mengine anayoyahitaji. Mungu anao watu wengi duniani kama hao walio nje ya nchi na hapa nyumbani ambao wanahitaji kuwasiliana na dada huyu kwa email na nina imani atapata mahitaji haya.
    Nami ninaomba awasiliane nami kwa email yangu: ak_abduel@yahoo.com.
    Nitatoa japo si kikubwa kwa watoto hawa.
    Be blessed. Anna

    ReplyDelete
  10. jamani tuache kuchangia harusi tuchangie mambo kama haya, una m-pesa dada nitachanga nitakachojaaliwa.

    ReplyDelete
  11. Mbona watu mnataka kukompliketi mambo, binti Miriam ameweka namba yake ya simu, halafu nanyi mnampa e mail zenu, mpigieni simu au mumtumie e mail zenu kwa text.

    ReplyDelete
  12. KWA WALE MNAOTAKA KUMSAIDIA,
    EMAIL YAKE NI mirium0280@gmail.com.
    Nimeipata kwenye blog yake aleyo post hapo juu. iko mkono wa kulia wa blog yake.KUTOA SIO MPAKA UWE TAJIRI. nawaomba hao ndugu zangu hapo juu wamwandikie email hiyo hapo.Badala ya kusubiri waandikiwe email.Shukran.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...