Ubao wa Matangazo ukionyesha matokeo ya mchezo wa leo
  Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Es Satif
 Marefarii na Manahodha wa timu zote mbili.
 Mkono wa kheri kabla ya mtanange kuanza.
 Mshambuliaji wa Timu ya Simba,Salum Machaku (kulia) akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Es Satif katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda bao 2 - 0.
 Mshambuliaji wa Simba,Emmanuel Okwi (kulia) akimtoka beki wa timu ya Es Satif ya nchini Argeria,Farouk Belkaid katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda bao 2 - 0,mabao yaliyopatikana kipindi cha pili cha mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi na Haruna Moshi.
 Ameir Maftah wa timu ya Simba (kulia) akiachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Es Satif.
 Beki wa Es Satif (alielala chini) akiondosha hatari langoni mwake wakati Salum Machaku akitaka kujaribu kufunga goli.
 Holaaaaaa..........
 Hatari langoni mwa Es Satif.
 Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Fredrick Sumaye (mwenye suti),Waziri wa Afrika Mashariki,Mh. Samuel Sitta (kulia),Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe pamoja na Mbunge wa Tabora Mjini,Mh. Aden Rage wapo uwanjani hapa kuisapoti timu ya Simba.
 Kocha wa Timu ya Shimba,Milovan Cirkovic (kushoto) akipeana mkono na Kocha wa timu ya Es Satif,Alain Geiger mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho,uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijinin Dar es Salaam.Simba imeshinda bao 2 - 0.
Mashabiki wa timu zote mbili wanavyoonekana.
Mashabiki wa Es Satif wakiwa na huzuni iliyopitiliza.
Onyo kali uwanjani.
 Mashabiki wa Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kumbe huyu shangazi mwanamkasi Salama Jay kumbe Simba luwala !?

    ReplyDelete
  2. SAFI SANA VIJANA

    ReplyDelete
  3. Big up 2 simba s.c.

    ReplyDelete
  4. Aungurumapo Simba Mcheza Nani?

    ReplyDelete
  5. Hawa ndio Simba bwana, wanajulikana kote Afrika

    ReplyDelete
  6. mko juu kama povu la bia. simba safiiiiiiii. watani mko wapi na club yenu mpya ya ndondi mlioanzisha? nataka niwadhamini.

    ReplyDelete
  7. Big up SSC hakika mnyama anatisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...