Jason Russel
Mkurugenzi wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayomshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inaelekea amepata ugonjwa wa akili.
Shirika la "Invisible Children", lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Bwana Russell.Shirika lilofanya filamu hiyo, liitwalo "Invisible Children", limesema kuwa Bwana Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa.
Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana hakujistri sawasawa, akipiga kelele mabara-barani, mjini San Diego, California.
Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. mnh huu uandishi,kuna shirika la invisible children au filamu ndio inaitwa invisible children...yaani ukisoma habari yote unahisi haijaandikwa na mtu 'profesheno'....

    ReplyDelete
  2. kisha somewa hala badri unafanya mas khara kujifanya mbabe kila kitu

    ReplyDelete
  3. Kony kaaga kwao! We unaleta mambo ya justice na freedom wakati watu wameaga vijijini kwao

    ReplyDelete
  4. HANA ADABU WALA HAYA ALITAKA KUFANYA BIASHARA KWA JINA LA KONY,ALE SASA HIZO PESA NA UCHIZ WAKE.

    ReplyDelete
  5. voodoo hiyo lazima

    chezea waafrica.

    Hope he recovers soon

    ReplyDelete
  6. Jamani hizi Google translator inabidi ziwe edited.

    Michuzi nawe sio unaupload tu habari yoyote, jaraibu kuipitia!

    Kumbe wazungu nao wanalogeka? Namtaka huyu mganga

    ReplyDelete
  7. Mdau wa maoni ya kwanza kwani shirika haliwezi kuwa invisible children na likatoa filamu ikaitwa invisible children?

    ReplyDelete
  8. Huyu jamaa ni Scam katengeneza peza Vibaya sana, KONY alikuwepo kweli na kufanya hivyo Vitendo ila Zamani sana Jamaa sijui kama yupo UGANDA tena, Huyu Mjinga Documentary alichemsha na njia za kupatia pesa hajafanyiwa Uchawi ila tu kuna wale wanaitwa FREEMASON washampiga Sindano sasa wanamsingizia kawa chizi baada kuona kachemsha Game la kuingiza pesa, FREEMASONS watu wabaya kuwa makini nao Jamani, Khalfan.

    ReplyDelete
  9. JAMAA NASIKIA KACHANGANYIKIWA ILE MBAYA. LAKINI INAELEKEA NI DRUGS.

    ReplyDelete
  10. Marekani wanarusha madege ya CHUMA yasiyo na marubani kushambulia maadui zao,,,,Mwafrika anarusha NDUMBA kwa mavumba YASIYO YA CHUMA kufanyiza Marekani !

    NANI ZAIDI?

    ReplyDelete
  11. DUNIANI HAKUNA JAMBO UTAKALO FANYA WATU WOTE WAKAKUPONGEZA NADHANI NI VIZURI KUJUA FACT KWANZA KULIKO KUSEMA MANENO BILA UHAKIKA,KWANZA NI AIBU KUONA MTU KAMA KONY BADO YUPO MPAKA LEO. ANYWAY I GUESS THAT'S OUR AFRICA.

    ReplyDelete
  12. wala hafi watamtafuta mpaka wachokehawampati.

    ReplyDelete
  13. Kony ni sawa na viongozi wa Tanzania kutumia ubabe kupitia uchawi kila kukicha. Na inasemekana kaanza kwa huyu jamaa kisha atamalizia kina Michuzi na wasomaje wake wote waliosoma habari za Kony. Inatisha na najuta kwa nini niliona ile documentary maana nawashwa kweli mwilini toka jana.

    ReplyDelete
  14. Yamemkuta!

    Haya ni matokeo ya Hela za Haraka Kuliko M-Pesa Vodacom, angetafuta wauaji wa kwao Marekani wanaotuma Madege nchi zingine kuendesha vita atengeneze Sinema zao na sio Afrika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...