Hi uncle, 
Heshima yako kwanza kwa kulisongesha libeneke inavyotakikana.
huo mzinga nimeushuhudia jana maeneo ya Moroco mbele kidogo ya bonjor burgers pale kwenye best burgers in town.jamaa aliesababisha ajali ni mwenye gari namba SU T777 ambae alikimbia.Alimchomekea huyo jamaa mwenye Raum (gari ndogo) ambae kwakuwa alikuwa speed aliloose balance na gari ikapanda ile road separator na kuigonga hiyo costa.

Nahisi dereva wa dala dala nae hakuwa na leseni maana hakuwa na makosa ila alisepa baada tu ya mzinga.hawa madereva wa gari za SU,STJ,STK sijui wanaringia nini na wanaendesha rafu kama nini. mi nadhani serikali badala ya kutoa vibanzi kwenye macho ya wananchi itoe gogo kwenye macho yake kwanza,maana siku zote inaonekana ajali zinasababishwa na less qualified drivers sasa hawa madereva wa sirikali nao ni less qualified drivers au?

 Huu mzinga wa pili naushuhudia hawa jamaa wanasababisha baada ya ule wa kwanza kuntokea mwenyewe na askari magereza aliekuwa kapiga maji ya ilala.

Mdau.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Naungana na wewe mdau, madereva wa magari ya serikali wanaendesha vibaya sana, wanajiona wako juu ya sheria na vile hawasimamishwi na wanatetewa na maofisa wa usalama barabarani basi ndo sie mahohehahe tunakoma.

    ReplyDelete
  2. Wee mdau embu check taarifa zako kabla ya kwenda hewani. Hizo namba za SU hazipo duniani!

    ReplyDelete
  3. INASIKITISHA UZEMBE WA WACHACHE UNAONDOA WENGI EH MWENYEZIMUNGU TUEPUSHE NA HAYA MABALAA.

    ReplyDelete
  4. Tatizo kubwa la hapa tanzania hatuna sheria kamili za barabarabi kila dereva anafanya anavyo jua mwenyewe pia kwa sisi wanzania wenzangu atuheshimu kazi inayo kuletea mkate wa kila siku sasa huyu amesababisha ajari amekimbia kwa uzembe wake kumbe angekuwa mwangalifu ajari kama hizi zisingetokea

    ReplyDelete
  5. SU, STK, SM, JW na zote za sirikali ukigongwa usisumbuke trafik wala bima nenda zako ili mradi uko salama basi shukuru Mungu, katengeneze kigari chako. serious advise.

    ReplyDelete
  6. huyo mdau anaesema SU haipo duniani si kweli kachunguze magari ya tanesco,posta na maji zina SU.
    Usibishe kitu bila kuwa na evidence.....Na DFP utasema hamna?

    ReplyDelete
  7. SU maana yake shirika la umma sasa anakataa nini anakaa wapi tanzania?

    ReplyDelete
  8. Na hato mabasi ya kwenda kasi sindio yatamaliza watu na madereva wetu hawa leseni wanaletewa baa

    ReplyDelete
  9. Huyo anaesema namba za SU hazipo tena nadhani ni mvivu wa kufikiri na kujua mambo ,..serikali yetu kwa kupitia idara ya maji,tanesco,ttcl,tanapa,ncaa na nk..bado wanatumia namba za SU. Usikurupuke kucoment kama huna uhakika na unachoongea.

    ReplyDelete
  10. Hakuna namba inayoanza na SU halafu ikawa na herufi T! Huo ndio ukweli.

    ReplyDelete
  11. Kwa taarifa ya mdau wote wanamakosa. Aliyesabisha ajali na aliyegonga na aliyegongwa. Kosa la aliyesababisha/aliyekimbia ni kutosimama baada ya tukio la ajali. Aliyegonga alikuwa anakimbia wakati speed limit barabarani zipo na hazijawekwa kwa mapambo. Speed limit zina madhumuni yake makubwa tu. Aliyegongwa kuna nini anaficha cha kumfanya akimbie wakati kosa si lake. Ni day worker au anamiliki leseni halali?
    Tasmini fupi tu kutokan na taarifa ya mdau hapo juu.

    ReplyDelete
  12. Duuh halafu ukute kagari kenyewe ni KAMKOPO,na kana third party bima,yaani ni kilio tu hapo daaah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...