MAREHEMU MWALIMU CONSTANSIA JOACHIM MSAKY
26.04.1948 - 19.02.2012
Familia ya Bw. Joachim Michael Msaky wa Upanga, Dar-es-Salaam wanatoa shukrani za dhati kwa wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine wakati wa kipindi kigumu cha msiba wa mke na mama mpendwa MWALIMU CONSTANSIA MSAKY aliyefariki tarehe 19 Februari 2012 na kuzikwa tarehe 22 Februari 2012 katika shamba la familia huko Kibaha kwa Mathias.
Shukrani za kipekee ziwaendee ndugu, jamaa na marafiki wa pande zote. Shukrani nyingine ziwaendee Jumuiya ya Mt. Theresa mtoto wa Yesu Upanga, Jumuiya ya Mtakatifu Gabrieli malaika mkuu Upanga, Paroko wa Kanisa la Mt. Imakulata Upanga, Nyumba ya maaskofu ya Bethania Upanga, familia na ukoo wa Msaky na Njau pamoja na majirani wote.
Ni vigumu kuwataja wote hata hivyo tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa kutufariji na misaada yenu ya hali na mali.
WOTE MNAKARIBISHWA KWENYE MKESHA WA AROBAINI TAREHE 28 MACHI 2012 IKIFUATIWA NA MISA YA SHUKRANI SHAMBANI KWA MAREHEMU KIBAHA KWA MATHIAS TAREHE 29 MACHI 2012 SAA 6 KAMILI MCHANA TUNAOMBA MSHIRIKI.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA – NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE – APUMZIKE KWA AMANI.
-AMINA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...