Baadhi ya Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania Marekani wakiwa naBalozi Mwanaidi Maajar kwenye picha ya pamoja na Naibu Gavana wa Jimbo la Wisconsin Rebeca Kleefisch mara baada ya kuwasili ubalozini hapo kwa chakula cha mchana tarehe 21.03.2012.

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar
akimkaribisha mgeni wake Naibu Gavana wa Jimbo la Wisconsin Mhe.
Rebeca Kleefisch alipofika kutembelea ubalozi kwa mara ya kwanza
katika kuendeleza mahusiano kati ya jimbo hilo na Tanzania.
akimkaribisha mgeni wake Naibu Gavana wa Jimbo la Wisconsin Mhe.
Rebeca Kleefisch alipofika kutembelea ubalozi kwa mara ya kwanza
katika kuendeleza mahusiano kati ya jimbo hilo na Tanzania.
Mhe. Rebeca Kleefisch, Naibu Gavana wa Jimbo la Wisconsin
akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani. Naibu Gavana Kleefisch alifika ubalozini hapo kwa mualiko wa
Balozi Maajar kwa nia ya kuendeleza mazungumzo ya ushirikiano baina ya
Tanzania na Wisconsin yaliyoanzishwa mwezi Februari, 2012 wakati
Balozi Maajar alipotembelea jimbo hilo.
Balozi Maajar akimuonyesha Naibu Gavana Kleefisch baadhi ya
vivutio vya utalii ambavyo vinapatika Tanzania tu, wakati Naibu Gavana
alipotembelea ubalozini hapo tarehe 21.03.2012.
Balozi Maajar akimuelezea mgeni wake kuhusu zawadi ya kanga
aliyompa inayotangaza Tanzania na sherehe za miaka 50 ya uhuru. Naibu
Gavana Kleefisch na familia yake wanatarajia kutembelea mbuga za
wanyama Tanzania.
Balozi Maajar na Mgeni wake Naibu Gavana Kleefisch kwenye
picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania, Washington DC
muda mfupi kabla ya kuagana na Naibu Gavana huyo aliyetembelea
ubalozinihapo na kula chakula cha mchana.
Balozi Maajar na Naibu Gavana Kleefisch wakiwa ofisini kwa
Naibu Gavana huyo mjini Madison kwenye Jimbo la Wisconsin wakati
Balozi alipomtembelea ofisini kwake kwa mara ya kwanza mwezi Februari
mwaka huu 2012.
Naibu Gavana huyo mjini Madison kwenye Jimbo la Wisconsin wakati
Balozi alipomtembelea ofisini kwake kwa mara ya kwanza mwezi Februari
mwaka huu 2012.
(Picha na Maelezo na Mindi Kasiga)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...