Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge Bw. John Joel (kushoto) akijadili jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Teknologia ya Mawasiliano Bw. Didas Wambura kabla ya makabidhiano rasmi ya jengo la nyumba atakayokuwa anatumia Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo eneo la Uzunguni nje kidogo ya mji wa Dodoma leo.
Mshauri Mwelekezi (consultant) wa Pacha Building Construction Company ( ambayo ndiyo imejenga jengo hilo) Bw. Shaban Mwatawala (kulia) akitoa maelezo ya ujumla kabla ya kuwapitisha viongozi wa Ofisi ya Bunge katika jengo hilo. Kulia kwake ni Mhandisi wa Miradi wa Pacha Bw. Johanes Maganga, Mkurugenzi wa Mipango na Teknolojia ya Mawasiliano wa Bunge Bw. Siegfied Kuwite, na Mkurugenzi wa Sgighuli za Bunge Bw. John Joel.
Bwana Mwatawala akimkabidhi Msanifu Majengo M. F. M Msangi (kulia) anayewakilisha Wakala wa Majengo ya Serikali. Wakala wa Majengo Tanzania ndiye Meneja wa Mradi huu.
Muonekano wa nyumba hiyo kwa mbele. Jengo hili ambalo litakuwa makazi ya Spika yeyote atakayeliongoza Bunge la Tanzania lilianza kujengwa Disemba 2009 na limegharimu takriban sh. 1.5 bilioni. Hapakuwahi kuwa na nyumba rasmi ya Spika wa Bunge Dodoma.
Mlango wa mbele wa jengo.
Ngazi ndani ya jengo ambalo lina vyumba vinne vya kulala, sehemu ya mapumziko, sehemu ya chakula, maktaba na jiko.
Upande wa nyuma wa jengo.
ati sh ngapi tena?...kwani nyumba ya mil mia mia mbili spika hawezi kukaa?mmh hongera spika
ReplyDeleteWIZI MTUPU, NGOJA MADAKTARI WAONE HII ALAFU MTAKUJA KUTUAMBIA HAWANA HAKI YA KUGOMA.
ReplyDeleteMDAU
kweli Mwl. Nyerere angefufuka leo, angekufa ghafla.
ReplyDeleteLimetulia,lakini tumeshaambiwa bungeni kuna umaskini.....
ReplyDeleteDavid V
kuleni nchi wakubwa
ReplyDeleteHalafu oooooh, Tanzania ni nchi masikini?
ReplyDeleteImejengwa kiofisi ofisi na sio ki residential residential.
ReplyDeleteHaya ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi; kuna haja ya kujenga jumba la kifahari namna hiyo kwa Spika wa Bunge ili hali Hospitali zetu madaktari wanalia na mishahara midogo kila siku. Hakuna dawa wala vitanda mahospitalini...shame on them! mtakuja kulipa kwa dhambi zenu hizo... huu in upuuuzi mtupu; haya tuonyesheni hilo jumba la spika akiwa Dar es Salaam. 1.5bil ni pesa ambayo ingefanya mambo makubwa kwa zahanati zote zilizoko nchini... hii ni laana kwa kweli
ReplyDeleteNi wazo zuri kuwa na jengo la Spika, na jengo si baya linaridhisha.
ReplyDeleteIla hiyo gharama sijui inalingana na jengo?
PIA hivi kumbe bado wabongo wanakubali ukoloni mambo leo?
kwanini hilo eneo waliite Uzunguni?
Waache ushamba, laiti wangejua wazungu walivyokuwa na shida na vijumba kama matundu ya njiwa.
Tujivunie Uafrika na majina yetu.
DAA SAFI SANA 1.5 BIL KWENYE NYUMBA KWELI SERIKALI INA UCHUNGU NA WAFANYAKAZI WAKE...HEKO KIKWETE..DAAAAAAAAA...LOL
ReplyDeleteAisee, vizuri sana.
ReplyDeleteHow much did it cost?
GOD KNOWS.
haya tena mkuu,nyumba 1.5 billion wakati madaktari wana goma kwa vitendea kazi. kwani sasa hivi mama Anne Makinda anaishi Hoteli?na kabla yake walikuwa wakiishi wapi? kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kupanga.
ReplyDeleteHizo ngazi hivi wamezingatia spika akiwa mlemavu (disable in wheel chair)?
ReplyDeleteWanaoshangaa hizi gharama hawajui hali halisi ya gharama za maisha! Kumbuka hii ni sura ya nchi kwa mhimili wa Bunge. Tuache kulalamika ndg zangu. Bora jengo limejengwa na linaonekana. Tulukuwa hatuna pa kuwakaribisha wageni wa kibunge Dodoma sasa tumepata. Kwa naomba nawaomba tuungane kwa ni fedha hii haijaenda mfukoni mwa mtu. hata aje spika kutoka vyama vingine ataishi hapa!
ReplyDeleteNyumba ni Nzuri in a Hadi ..swimming pool.....ofisi ya spika inastahili.....ni muhimu na minimill mingine nayo ipate makazi stahili ...ie official residents za jaji mkuu...,na wakuu wa vyombo vingine......pia kwenye local government ...kuwe na official residents za mayors......ambao tunaamini katiba mpya utawaala mamlaka mapya kuchukua kazi za wakuu wa wilaya na mikoa......na Tukabana matumiizi kwa wao kutumia nyenzo wanazotumia wakuu wa wilaya na mikoa sasa .....
ReplyDeleteAnonymous said...
ReplyDeleteWanaoshangaa hizi gharama hawajui hali halisi ya gharama za maisha! Kumbuka hii ni sura ya nchi kwa mhimili wa Bunge. Tuache kulalamika ndg zangu. Bora jengo limejengwa na linaonekana. Tulukuwa hatuna pa kuwakaribisha wageni wa kibunge Dodoma sasa tumepata. Kwa naomba nawaomba tuungane kwa ni fedha hii haijaenda mfukoni mwa mtu. hata aje spika kutoka vyama vingine ataishi hapa!
Sun Mar 11, 10:34:00 AM 2012
Anonymous said...
Nyumba ni Nzuri in a Hadi ..swimming pool.....ofisi ya spika inastahili.....ni muhimu na minimill mingine nayo ipate makazi stahili ...ie official residents za jaji mkuu...,na wakuu wa vyombo vingine......pia kwenye local government ...kuwe na official residents za mayors......ambao tunaamini katiba mpya utawaala mamlaka mapya kuchukua kazi za wakuu wa wilaya na mikoa......na Tukabana matumiizi kwa wao kutumia nyenzo wanazotumia wakuu wa wilaya na mikoa sasa .....
Sun Mar 11, 11:06:00 AM 2012
Nimecopy na kupaste hapo ili nikueleze kuwa inawezekana wewe hujui unaloliongea au ni mmoja wa wakandarasi mliopewa kutafuna hizo pesa au ni mmoja wa wale mnaotafuta jasho la walipa kodi, hivi we kama una akili unaweza ukashabikia nyumba ya kulala ya one billion? tena ina vyumba vinne tu alafu unafanganya hapa eti tulikuwa hatuna mahali pa kukaribishia wageni mweh, kweli nimeamini kuwa uyaone.
mdau
KINACHOFUATA BAADA YA MATUMIZI HAYA YA BILIONI 1.5 HUYO MAMA MARA MOJA AHAMIE DODOMA NA AWE ANAKAA HUKO.
ReplyDeleteDuhh acheni Mungu aitwe Mungu, kauli ya kusema eti 'Bungeni umasikini' hata mwezi haujapita tokea itolewe leo hii huyo huyo mtoaji kauli anaandaliwa jumba la hekalu la Bilioni 1.5...!!!
Je, Masikini anaweza kukaa nyumba yenye thamani ya Bilioni?
Sio matumizi yafanyike halafu mara zote tunamuona mama Samora Avenue, Oysterbay na Masaki!.
Viongozi wa Tanzania sijui wamerogwa na nani hadi kila kitu Dar Es Salaam, Dodoma hawakutaki kabisa licha ya uendelezaji uliotugharimu sana nchini!
Hela hiyo bora tungewatumia tiketi za ndege Watanzania waliokwama Ugiriki kurudi nyumbani kwa shida na maisha kuwakataa huko Majuu!
ReplyDelete