Ofisa wa Shirika la Maendeleo Japan (JICA), Minako Yamamoto (kulia), akijadiliana jambo na Ofisa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Irenius Ruyobya huku akiwa amejifunga kitambaa kuziba mafua aliyonayo asiambukize watu wengine, leo wakati wa mkutano wa kukusanya maoni kwa wadau juu ya sensa inayotarajiwa kufanyika nchini Agosti, mwaka huu. Mkutano huo ulifanyika Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Albina Chuwa (katikati) akijadiliana jambo na Kamishna wa Sensa, Amina Said (kushoto) pamoja na Mshauri wa Matokeo ya Takwimu, wa Taasisi ya DFID, Phillip Cockerill wakati wa mkutano huo.
VIPI TENA, MBONA MDAU WA JICA ANAZIBA MDOMO NA PUA!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteKUNA MAGONJWA YA MLIPUKO (KUAMBUKIZA ) KATIKA HUO UKUMBI AU NI ''MTU NI AFYA''
KAMA NI HIVYO
MBONA OFISA WA TAKWIMU BWANA RUYOBYA HAKUVAA????
MBEBA BOX WA KUDUMU
Wajapani wana utamaduni mzuri sana wa kujali afya za watu wengine.
ReplyDeleteKama huyo dada hapo pichani alivyovaa hiyo maski usoni ili asiambukize wengine mafua aliyo nayo yeye.
Sisi waafrika tukipata UKIMWI tunataka tufe na wengine kwa kuusambaza.
Inbgekuwa sisi Wakonongo ndio kwanza mtu anapenga kamasi tena bila kujali!
ReplyDeleteJamaa kachafua hali ya hewa nini?
ReplyDeleteMichael Jackson (R.I.P.) alipofanya hivyo acha mumpigie kelele, wakati nyie wenyewe mnaziba pua mkikatiza mitaani.
ReplyDeleteOna mtu Mstaarabu anavyomjali mwingine!
ReplyDeleteAnakukinga dhidi ya Maambukizi ya Mafua.
Angekuwa mtu mjinga hata Virusi vya Ukimwi anakumwagia tena bila wasi wasi huku akijua kuwa amesha athirika kitambo tu!